Modus operandi ya Rais Magufuli ni ya ajabu!

Modus operandi ya Rais Magufuli ni ya ajabu!

Jukumu la ulinzi wa nchi ni la kila mtu ambaye ni raia wa nchi hii. Hili jukumu ni wajibu wa lazima siyo hiari. Kupata nafasi ya kuteuliwa ni moja ya haki yako ya kutekeleza jukumu la lazima la kuimarisha ulinzi wa nchi.

Kukataa nafasi ya uteuzi ni hatua mojawapo ya kuelekea kuhatarisha usalama wa nchi na kwa wale wenye miwani mikali kitendo hicho chaweza kufananishwa na uhaini. Kwa hiyo, uwe umepewa taaarifa ama la lazima utii wito wa kuteuliwa!
Kama aliyeteuliwa anajiona haiwezi hiyo kazi je?

Aikubali tu?

Mambo ya ajabu kabisa hayo.

Ndo maana tupo kwenye hali tulonayo.
 
Kuna mahala katiba ya JMT imetamka kuwa rais anatakiwa atoe taarifa kwa mtu atakae mteua?
Sijui.

Lakini kwa akili tu hizi za kawaida, kumteua mtu bila kufanya naye mazungumzo ni ujuha.
 
Umewahi kuishi vijijini? Unajua maisha ya mbwa huko vijijini? Wafuga mbwa vijijini huwa wanauliza mbwa wao kama watakubali kupewa chakula fulani? Basi kwa kifupi Magufuli ni rais mwenye kiburi na anajua kabisa hakuna wa kukataa uteuzi kwenye siasa za Tanzania. Anajua wanasiasa wote wako kule kushibisha matumbo yao hivyo hawawezi kukataa uteuzi wowote. Kuna wanaosema eti huenda amesema uongo na aliarifiwa kabla. Hao hawajamsoma vizuri Magufuli. Mimi naamini ni kweli kabisa huwa anateua na kutangaza bila kumuarifu mhusika.
Aisee!!

Vipi sasa kama mteuliwa haitaki hiyo kazi au anaona hana sifa za kuifanya hiyo kazi?

Ni lazima aukubali uteuzi, atake asitake?

That’s some weird shit, bruh.
 
Mzee na nawe unaamini kabisa kuwa Bashiru hakutaarifiwa kabla na taarifa za uteuzi wake kazikuta mitandaoni?
See, that’s the thing.

What Bashiru said strains credulity.

But, that’s what he said and that’s what I’m going by.
 
Matatizo ya nchi yetu na nchi nyingi za kiafrika ni kuendelea kutenda kama colonisers wetu walivyo tuelekeza! Ambayo tunaiita awe na experience! Akitokea kiongozi anayetenda kwa kutumia njia zake za kufanikisha jambo kwa haraka - tunakuwa wa kwanza kumuona hafai - kwasababu experience yetu amei side step! Bashiru amekuwa akifanya kazi kwa karibu sana na Magufuli, hilo ni jawabu tosha na mengine ni mazungumzo baada ya habari (yale ya hakujulishwa)! Hata kama hakujulishwa, anajua!
Mfano mwingine wewe mleta mada, naukubali uandishi wako sana, unavyowasilisha arguments zako n.k. Kama nikiambiwa kuteua mtu wa kufanya uandishi kwenye maswala haya unayokuwa unachangia, nitakupendekeza! Ukikataa, hilo swala jingine. Ila mimi naona unafaa. Baada ya kusema hayo, vyeo hivi vinakuwa vetted for, siyo for any Masanja and Marwa!
Kati ya watanzania wachache sana wenye upeo wa hali ya juu wa kufikiri wewe mkuu ni miongoni mwao! Hongera sana kuvuka kikwazo cha utumwa wa fikra!
 
Mwanasiasa usimuamini kamwe, akikwambia sitagombea cheo chochote hii kwake ni siraha kujiepusha na maadui huko mbele.
 
Na jamaa alishakiri kuwa hayupo tayari kutumikia cheo zaidi ya hicho alichokuwa nacho inamaana kama ni kazi ataifanya ile basi tuu kalazimishiwa
 
Taasisi ya uteuzi ipo kazini masaa yote! Wanajiridhisha kwanza kabla ya kupeleka jina kwa muhidhinishaji wa uteuzi. Kujiridhisha huko kunajumuhisha utafiti juu ya afya ya mlengwa wa uteuzi! Kwa hiyo, mkuu kaa mkao wa kuteuliwa tena bila wasiwasi; hofu zako taasisi ilishazifanyia kazi na inazizingatia kwa umakini mkubwa.

Kumbuka, lengo ni kuimalisha ulinzi wa nchi, Taasisi inazingatia hilo ndiyo maana mara moja ikishaona mushikeri inabadili uamuzi.
Sasa mizunguko yote hiyo ya nini?

Hiyo taasisi inachunguzaje afya ya mtu bila kumshirikisha wakati afya ni siri ya mtu? Je watajua kila kitu? Kuna magonjwa ambayo usumbufu wake huwa unatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Kama busara ya kumtaarifu mhusika tu haipo hiyo vetting yenyewe sioni kama itafanyika kwa weredi kwani wahusika bado hawajastaarabika.

Mnajaribu kupinda kona kutetea makosa. Mwisho lazima tutarudi palepale tu, ni busara kumshirikisha mteuliwa kabla ya kumtangaza.

Pia uteuzi sio lazima ukubalike. Huo uhaini wa kukataa uteuzi ndio nausikia leo.

NB: Naamini Bashiru taarifa alikuwa nayo.
 
JPM has too big of an ego to even care whoever he appoints is up to the duties and responsibilities pertaining to the job. JPM thinks he is G.O.D or maybe even Jesus Christ himself and every mere mortal he summons has to bow down to his demands.
 
Chai hii,ukitumbuliwa unapachua zile number za herufi,unaweka number za kawaida, magari ya viongozi yana number zaidi ya tatu kwa taarifa yako! Mfano (Waziri wa Maji) inasoma W M akitumbuliwa akiwa njiani, dereva wake anapachua ya W M wanaweka ya Kiraia kabisa au ya STL,STJ au STK acha chai mkuu
Mangungu sasa hapo umeelewa hata ulichokikanusha na pengine hujaelewa hata nilichokiandika

Njoo "tupachue" basi ashata na hii chai
 
Nikujuze tu! Post kubwa na nzito kama hizo lazima upewe taarifa kwanza! Kwamba je uko tayari?? Je uko fit kiafya? Unaweza teuliwa bila kuambiwa kumbe hutaki,au afya yako ni tete,ukafa baada ya mwezi mmoja!

Kuna watu wapo smart sana, Sumaye kabla jina lake kupelekwa bungeni na Mkapa alisema kabisa,kwamba aliitwa Ikulu na Mkapa akaambiwa nataka uwe Waziri Mkuu,the same na Pinda pia alisema,baada ya Lowassa kutema kitumbua,Mizengo Pinda aliulizwa na Jakaya! Sasa wewe sijui unataka kusema nini hapa! Au hujui maana ya vetting??
Kwa kukazia tuu, JK aliwahi twambia kuwa watu wengi wamekuwa na msaada sana katika chama au serikali unafikiria namna ta kumshukuru au kazi ya kumpa unamteua kuwa mkuu wa mkoa au wilaya lkn kwa mshangao mtu huyo anakwambia mzee nashukuru hiyo nafasi hapana. Haya niambie unamteua na kutangaza kabla ya kumjulisha baadae anakataa.
 
Unajua kuna ile assumption kwamba ukimtumpia mbwa pande la nyama hawezi kujivunga....

Probably Magufuli anaamini hawa watu hawana guts za kukataa posts kubwakubwa na hivyo hana haja kuwauliza kwanza kama wapo interested ama la.

Pia kuna repercussions zake kama mtu akikataa teuzi ya Rais. Kwa jinsi huyu mwamba anavyobehave, ukikataa unaweza kupewa kesi ya kuhujumu uchumi.
 
Simuamini uyo jamaa, maana kuna video ilisambaa alisema hatokubali nafasi nyingine yoyote atakayoteuliwa..look at him now
 
Ilishawahi tokea mara kadhaa kama tunavyoambiwa na wakongwe kuna baadhi ya watu awamu zilizopita wanapewa taarifa kuwa watateuliwa nafasi flani wanafanya sherehe kabisa, inabidi mamlaka za uteuzi ziachane na mhusika. Nadhani labda anakwepa mambo kama haya.
 
Nimesema kabisa dereva wake! Kaka hizi mambo kama hatujui tukubali kujifunza! Mwigulu Nchemba alifutwa kazi akiwa Kigoma! Maana yake alirudi dodoma na cheo cha ubunge! Maana yake dereva alitoa herufi za (WMNN) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nakuweka STL,STK au STJ nakuanza safari yakurudi kukabidhi ofisi! Na sio eti unaporwa gari,then wewe unarudi sijui na basi au fuso

Amos Makala pia alifutwa kazi akiwa njiani kwenda Dodoma,ikabidi wageuze gari kurudi Rukwa, dereva anatoa Herufi za RC nakuweka zakawaida tu!

Pia,Ukiteuliwa kupanda cheo ukiwa kwenye majumu yako,unaacha hapo hapo,Unakua sio na mamlaka tena, Mfano kutoka Naibu Waziri kwenda, Waziri Kamili,wanatoa herufi za Naibu Waziri,wanaweka number za kawaida,ukila kiapo cha cheo kipya,wanaweka herufi za cheo chako!

Wakuu wa taasisi kama TISS na TAKUKURU wana number zao nyingi nyingi tu!

Mwisho kabisa,wakati baraza jipya la Mawazi linaenda kuapishwa,magari yalienda na number za kawaida kabisa,baada yakula kiapo,dereva wakatoa number,nakuweka herufi za vyeo vyao!
Hahahaaa ulikuwepo hapo na huyo uliyemtaja?? Manaake mimi hata sijamtaja( Ndomaana nimekushangaa kuwa elewa nilichoandika na kwanini nimeandika vile)

Makalla hajawahi pia kutumbuliwa na kurudi Rukwa(kwa taarifa yako tu)

Baraza la Mawaziri likivunjwa utaratibu unajulikana. Hapo mimi niliongelea "extraordinary" zinazotokeaga au kwa lugha nyingine NN kaandika "cock a snook"...... Ukishaelewa hizo ndo utaelewa tuna choking Elea

Ntakueleza kitu kingine sijui kama ulifuatilia,kuna mama OCD Nyanda za juu alifukuzwa kazi na akaondoka kwenye mkutano wake anasikitika na baadae akarudishwa ndani ya nusu saa( Hayo ndo tunayaongelea kuwa Modus Operandi za huyu Mzee hakuna anayezielewa) anatufundisha " new normal"(Yeye anaitwa kutunyoosha)

Achana na hayo ya utaratibu wa dereva kufanya hivi na vile ambayo yako kwenye mafunzo. Kuna amri zinazotokea hakuna utaratibu huo unafuatwa ndugu yangu

Nitakukumbusha pia 2008 EL yalimkuta alijaribu kumtunishia JK kuachia ngazi( Tulikuwepo wakati huo) so najua sana hizo taratibu ulizoandika......nielekeze mpya na mimi nijifunze,sikatai kujifunza
 
Back
Top Bottom