Modus operandi ya Rais Magufuli ni ya ajabu!

Ahaaa. Sio utaratubu mkuu,bora hata leo mtu anapata taarifa kupitia mitandao.

Wakati wa mwalimu mtu alipata taarifa ya uteuzi kupitia radio (RTD).
Taja kabisa na jina la huyo mwalimu wako, unawachanganya watu hapa.
 
Mimi naamini kwa 💯% alikuwa na taarifa.
 
Bashiru ni muongo, uteuliwe bila taarifa alafu uambiwe asubuhi utaapishwa? pia kabla ya uteuzi mtu anapewa barua ya siri siku 14 kabla, je wale viongozi ambao walialikwa kuhudhuria nao waliakwa kupitia mitandao? kuna mambo mawili uteuzi na kutangazwa yeye alitangazwa kwenye public siku hiyo lakini uteuzi ulishafanyika 14 before na alikuwa anajua vizuri sn.
 
Katika hotuba yake hiyo ambayo aliitoa bila kusoma,
Naona anakikaratasi mkononi! Au mpaka aelekeze macho kwenye kikaratasi hicho ndipo ajulikane kuwa alikuwa anasoma?
jioni ya siku ile aliyoteuliwa, alikuwa yupo sehemu [nahisi labda alikuwa nyumbani kwake] akisoma mafaili ya kazi zake za ukatibu mkuu wa CCM, ndo eti akapata taarifa kupitia kwenye mitandao [ya kijamii] kwamba kateuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.
Kwa hiyo alikuwa kwenye mitandao au alikuwa akisoma mafaili?
Sasa kama Dkt. Bashiru alizipata taarifa za uteuzi wake huo kupitia kwenye mitandao kama tulivyozipata sisi wengine, ina maana hakukuwepo na mawasiliano kati ya mamlaka ya uteuzi na mteuliwa.
Umesema kwa "...akili yako ya ..."; lakini ukaficha uteuzi mwingine wa aina hiyo ili uhalalishe lengo la mada yako?
Teuzi zote afanyazo huo ndio utaratibu wake ambao huufuata?

Unao uhakika gani kwamba hao wawili Bashiru na mteuzi wake hawakuwahi hata mara moja kugusia jambo la uteuzi wa nafasi hiyo?
Unajua mahusiano kati ya wawili hao?

Ulaghai na hadaa za awamu hii zinajulikana, na watu kama wewe ni kiungo muhimu katika kuzieneza hadaa za aina hiyo.
 
"Damn, a nigga's style is unorthodox" -The Nororious B.IG "Niggas".

Kuna mtu siku moja atamuaibisha rais kwa kumwambia ana shughuli nyingine na hawezi kukubali uteuzi ambao hata hakuulizwa.

Kuna jamaa aliteuliwa kuw DC bila kuambiwa, alikuwa tayari ana kazi zake za kimataifa, kwa heshima tu alienda kuripoti kazini akakaa wiki chache, akasepa.

Mtu akikuteua kazi halafu usikie uteuzi kwenye vyombo vya habari maana yake kakudharau sana, hajaona hata haja ya kukuuliza kama utapenda hiyo kazi ama la.

Nimetoka kusoma kitabu kipya cha rais mstaafu wa Marekani Barack Obama "A Promised Land", anaeleza jinsi alivyofanya kazi kubwa kuwashawishi Joe Biden kuwa makamu wa rais na Robert Gates kuendelea kuwa Waziri wa Ulinzi. Ilibidi akutane kisiri na Robert Gates kwenye some fire brigade station kumshawishi abakie kuwa Waziri wa Ulinzi.

SenatorJoe Biden alijiona kama mtu aliyechaguliwa na wananchi na anaye report moja kwa moja kwa waliomchagua huko Delaware, aliona kukubali kuwa makamu wa rais ni kama kujishusha kuwa mtu wa pili, badala ya kuwa anaripoti kwa wananchi moja kwa moja, awe anaripoti kwa Obama. Mwishowe akakubali.

So, kwangu mimi naona kuteuliwa halafu kusikia habari redioni ni dharau sana.

Lakini kwa nini Dr. Bashiru amesema hili? Is this a naive case if "too much information" from Dr. Bashiru? Or is there a political calculation?

Dr. Bashiru aliwahi kusema kwamba, Ukatibu Mkuu wa CCM ni kazi yake ya kwanza na ya mwisho katika siasa. Alijinadi kama mtu asiye na ambition ya kupanda ngazi kwenye vyeo vya siasa/ civil service. Sasa, naona kama anataka kujibu swali kabla halijaulizwa, imekuwaje amekubali kazi hii ya Ukatibu Mkuu Kiongozi? Naona anajibu kwamba hakuwa hata na nafasi ya kukataa, alisikia tu kateuliwa kwenye vyombo vya habari.

Inawezekana pia aliyemteua Dr. Bashiru alimuuliza kabla, na hii habari ya kusikia kwenye vyombo vya habari inatumika kama geresha ya kujibu watu watakaouliza imekuwaje Dr. Bashiru asiyependa vyeo, aliyesema hatafanya kazi nyingine zaidi ya Ukatibu Mkuu wa CCM, amepewa uKatibu Mkuu Kiongozi?

Kuna maudhui yanayojirudia kwa Magufuli, ametoa matamko kadhaa kwa watu anaowaona wanapenda vyeo, hususan wakuu wa mikoa wanaogombea ubunge (kina Makonda na RC mwingine aliwataja).

Kwa upande wa pili, hapa tunaona anamzawadia mtu aliyejinadi kwamba hataki vyeo.
 
Mfano mwingine wewe mleta mada, naukubali uandishi wako sana, unavyowasilisha arguments zako n.k. Kama nikiambiwa kuteua mtu wa kufanya uandishi kwenye maswala haya unayokuwa unachangia, nitakupendekeza!
Bila shaka unavyo vigezo fulani unapokubali "uandishi" wake; na unatumia vigezo hivyo kama nguzo ya kumpendekeza.

Halafu angalia mkanganyiko ulioanza nao:
"Kutenda kwa kutumia njia zake"? Njia hizo ni za majaribio? na alizitumia wapi zikaleta "kufanikisha jambo haraka"?

Maana yako ni kwamba nchi zetu za kiafrika tuache kufuata taratibu zilizokwishaonyesha mafanikio kwa vile pengine zilibuniwa na wakoloni?

Si ni bora basi tutunge taratibu zetu na tuzijaribu kama zinafaa na kuleta mafanikio kuliko kutegemea 'whims' za mtu mmoja!
 
Ulienda shule? Kusoma kikaratasi ndio kusoma hutoba iliyochapwa?

Mtu huwezi kufanya kazi huku unapitia mitandao? Kisa tu unapitia mafaili!

Kama mtu mwenye akili usingechangia hii mada. Ni mweupe kabisa kichwani.

Habari ya mteuliwa na mteuzi kugusia mada ni assumptions za kishamba.
 
Kuna possibility jamaa alipewa taarifa ila akakosa cha kuhutubia akaamua aongee hayo na kuna possibility ni ukwel

Kama ni kwel najiuliza tu, what if unamteua mtu kumbe kakata moto home kwake?😰

Ila sidhan kama Raisi hakuwaza hili. Bashiru katutia kapuni aiseee😂
 
"Kwa akili zangu hizi za kidato cha 4"

Mimi wa form 6 nasema "Jambo ambalo huna taaluma nalo usiliandikie chapisho"

Kwakuwa kuzungumzia jambo ambalo hulifahamu ni kujidhalilisha na upotoshaji.
 
"Kwa akili zangu hizi za kidato cha 4"

Mimi wa form 6 nasema "Jambo ambalo huna taaluma nalo usiliandikie chapisho"

Kwakuwa kuzungumzia jambo ambalo hulifahamu ni kujidhalilisha na upotoshaji.
Nimezungumzia ninachokijua.

Na ninachokijua ni nilichokisikia toka mdomoni mwa Bashiru Ali.

Hakuna nilipojidhalilisha wala kupotosha.
 
Uajabu wake ndio umefanya kuwa na misimamo hiyo aliyonayo kwenye corona ambapo hata mleta mada anakubaliana nayo.
 
Unahangaika bure na kunitafuta nikukumbushe ulivyo mtupu kichwani.

Kazi hiyo nilishaikamilisha zamani na ukanielewa vyema.

Sihitaji kukukumbusha mara kwa mara juu ya hilo.
 
Naomba nikumbushe ile hali ambayo mtu anayejua namna ya kutatua tatizo halafu watu wakaa kimya inatitwaje kwakimombo
Duh!

Kiswahili kinakupiga chenga. Kimombo utakiweza kweli wewe?
 
Mimi nadhani hawa viongozi wanatuyeyusha tu, kwa cheo hicho lazma aliambiwa kabla. Kwa wakuu wa wilaya labda unaweza kushtukizwa bali uwaziri au post nyingine kubwa napata shida kuamini kuwa ni surprise.
 
Kuna kipindi Rais mwenyewe wakati anawaapisha wakuu wa mikoa alikiri kwamba aliwateua bila kuwauliza.
Aidha kuna jamaa mmoja alikuwa meneja wa kanda wa Tigo aliwahi kuukataa uteuzi.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Kawaida ya "mitume"..... yule aliyekuwa na wanafunzi 12, si unakumbuka wengi alikuwa anawaambia tu "nifuate" na wanamfuata?

Hivi Kangi Lugola yupo wapi siku hizi?
Baada ya kupita miaka elfu mbili na ushee,bado nchi inaendeshwa kimangumashi?.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Nimezungumzia ninachokijua.

Na ninachokijua ni nilichokisikia toka mdomoni mwa Bashiru Ali.

Hakuna nilipojidhalilisha wala kupotosha.
We sijui ni nyani wa msitu Gani? Vyovyote iwavyo Elimu yako ya kidato cha nne unazungumzia habari za uteuzi wa Rais.

Ili uweze kuzungumzia habari zile ungetuambia wewe ni mwanasheria, au ni miongoni mwa wasaidizi wa Rais! Angalau ungekua na weledi.

Hebu endelea kuuza viwanja Mbopo mzee achana na masuala yaliyokuzidi kimo.
 
Maamuzi ya mtu mmoja iwe ktk familia, ukoo,kijiji au tarafa hayajawahi kuwa na tija duniani. Sembuse ktk nchi never!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…