Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohammed Dewji amerudi nyumbani salama. Nimezungumza naye kwa simu dakika 20 zilizopita. Sauti yake inaonyesha yu mzima bukheri wa afya. Shukrani kwa wote kwa dua na sala. Naenda nyumbani kwake kumuona muda huu.
Screenshot_20181020-052801.jpg
Screenshot_20181020-053241.jpg
 
Polisi wangemrudisha bila TBC kufika, hao ni wale wale wasiojulikana
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!?
Masharti hayo yanawekwa na nani? Mlipaji au anayedai? Hebu tuondelee ujinga wako hapa!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom.
Nani aliyewahi kuzungumza yaliyomsibu hapo kabla? Miongoni mwa wote waliowahi kufanyiwa umafia nchi hii, ni nani aliyewahi kuzungumza? Au hawakuzungumza kwa sababu walilipa ransom?
Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini.
Hiyo ni hoja yako na wana-Lumumba wenzako pamoja na genge lote la wahalifu kama wale ambao waliwahi hadi kuvamia studio! Hoja iliyo mbele ya wananchi ni je, baada ya kutoweka Ben Saanane na hatimae Mwandishi wa Mwananchi, kisha kutoweka kwa ROMA na baadae kuja kupatikana kabla hajatoweka Mo Dewji na kufuatiwa na drama za Kamanda Sirro; WHO'S NEXT! Usitake kuaminisha watu kwamba utekaji kwa sasa unalenga matajiri wakati utekaji nchi hii hivi sasa unaelekea kuwa ni jambo la kawida! WHO NEXT?

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.
Umejuaje kwamba huko kusini mwa Afrika huwa wanateka matajiro for ransom wakati umeshasema masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lolote?
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?

Sidhani biashara unayoongelea inafanana na Biashara yetu....angalia footprint na trend a nyuma!
 
Eeehh, alikuwa kwenye 'sabbatical' ya chama tukadanganywa katekwa?

Nchi hii imekuwa ya mazingaombwe na watu tumekuwa kama akili zimeturuka.

Keshokutwa si ajabu akawa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, kuongeza nguvu ya chama!
 
Back
Top Bottom