Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama


Eti ransom..

Acheni kutufanya mafala.....

Labda uniambie waliochukua ransom ni hao hao govt ila usidanganye eti alikua kidnapped na independent kidnappers!
 
Mo maneno yake ya Kwanza baada ya kuombwa aongee kidogo alisema "namshukuru Mungu kwa kuwa niko salama, pia namshukuru mh rais......."

Anamshukuru mh rais kwa kipi? Nimejiuliza maswali yasiyokuwa na majibu

Hili la kumshukuru Raisi labda ni kiwewe.
lakini pia Januari Makamba ana uhusiano gani wa karibu na Mo mbona inaonekana alikuwa wa kwanza kupigiwa simu na Mo?
 
Hakimu-Msomali
PP-msomali
Advocate-msomali
Mshitakiwa-Msomali
Je unategemea nani hapo ataehukumiwa?[emoji3]
 
Kwahiyo kale kamgomo baridi kakutishia kufunga viwanda vyote tarehe 20 ndio kamefanya kazi?
 
Hivi kuna nchi yenye mabwege kuliko Tanzania? Mtekwaji halalamiki katekwa na serikali bali anaishukuru, nyie mnamlazimisha aseme katekwa na serikali!
Sasa ulitaka alalamike ili wamrudie tena????Usiwe bwege hivyo unafikiri tu ndani ya box!Conspirqcy ziko za aina nyingi,nenda kasome mikasa iliyowahi tokea duniani ili upanue uwezo wako wa kufikiri!
 
NASUBIRIA ALIEPATA DAU LA BILLION MOJA
 
Kinachotuchanganya zaidi ni hao watekaji kutumia gari hiyo hiyo kumrudisha MO hadi Gymkana bila kukamatwa japo ulinzi umeimarishwa kila kona.
Hii haihitaji elimu yoyote ya upelelezi kung'amua kuwa kuna mchezo mchafu nyuma ya pazia.
 
Cctv yenye drone automated inayofukuzia Gari, yenye eyefish I aangalia ndani na inauwezo kutoa picha ya Techno!!

Tunaambiwa tuwapongeze kufanikisha kupatokana Mo! Just few steps kutoka ikuru! Eneo linalolindwa 24hrs that is why barabara hiyo saa 12 haoiruhusiwi kupita!Maajabu hayaishi nchi yetu hii!
 
Husikii aibu?
 
Chadema wamechukizwa mno na kupatikana kwa Mo maana kiki yao imebuna.

Shida na Matatizo yanayoipata Tanzania ndiyo ufahari wa Chadema!
 
Wanajitahidi kuua soo ionekane wabongo hawajahusika waliohusika Ni watu Wa nje Ila kwa wajanja tumeelewa mchezo mmeona mmejichanganya mkamuachia moo

Yaani Ni sawa na kuanzisha ugomvi afu ukimbie.. Pressure ya wachunguzi kutoka nje inayofanywa kimya kimya ndio imewapiga KO
 
Ndugu, wangejua kuwa wamebanwa hivyo wasingeendesha gari ile ile mpaka viwanja vya gymcana
 
Hivi jamaa hajaongea chochote tangu aongee siku aliyetekwa Mo???
 
Unaweza kuniambia sababu ya Mo kutekwa ni nini?
 
Ni imani yangu kuwa mpaka sasa familia imeshapoa na kujua angalau kwa juu juu kilichomsibu mtoto wao. Ikumbukwe kuwa familia iliitisha press conference na kuutaarifu uma kuhusu tukio la kupotea kwa Mo. Pia ilitoa ahadi ya tuzo (baunty) kwa atakayefanikisha kupatikana mtoto wao.

Ni maoni yangu kuwa familia ingeitisha PRESS CONFERENCE kuutaarifu uma kuhusu kupatikana kwa Mo. Pia ijibu angalau maswali machache ili kuondoa kelele zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii. Wana wajibu wa kuwaeleza watanzania ukweli wa haya mambo kwa faida yao na ya jamii kwa ujumla.

Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…