Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Kuna kutekwa na kujiteka!

Matajiri hutekwa, masikini kama Roma hujiteka!
Kitakachoondoa mashaka ni Mo kuongea na vyombo vya habari na kujibu maswali. Kama hataongea itakuwa ngumu sana

Kila mmoja atakuwa na theory yake ambayo si lazima iwe sahihi au makosa

Kwa hiyo unaamini akina Roma walijiteka? Akina Ulimboka walijiteka?
Akina Ben walijiteka? Azory amejiteka?

Haya mambo mnayajua nyie sisi mbumbumbu tunawasikiliza.
Jambo jema tunauwezo wa kusoma aeio na hadithi japo tunaweza tusielewe.

Hata gazeti la uhuru tunasoma vichwa vya habari, ndiyo faida ya shule hasa sisi wa std VII
 
Afu MTU alotokwa kutekwa kwanini haraka haraka aende nyumbani badala ya kuripoti kituo cha polisi.

Ambapo angeandikisha maelezo yake, kisha aende HOSPITALI.

Kwa sasa nilikua natarajia MO angekua hospitali kwa uchunguzi zaidi
 
Hongera sana Jeshi la polisi huu ni ushahidi mwingine wa weledi wenu wa hali ya juu
 
Taarifa zilizotufikia asubui ya leo ni kupatikana kwa Mo Dewji. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kupatikana kwake akiwa hai na salama salimini. Swali langu kwa wataalamu wa mambo. Je? jeshi la polisi litamchukua tena Mo kwa ajili ya uchunguzi zaidi au litamuacha apumzike na aendelee na shughuli zake za kawaida?

Sababu ya swali hili ni kutokana na maswali mengi yasiyokua na majibu yaliyo sababisha na taarifa ya vyombo vya dola katika tukio hili. Tukianza na Wazungu wawili, CCTV inayotembea kufuata gari, taarifa za kupatikana kisha kufutwa ghafla, gari la msumbuji na maswali mengine kedekede. Ambayo kwa namna fulani hayawezi kupingana na mawazo ya wengi juu ya uhusika wa serikali katika tukio hili.

Je tutegemee polisi kumtwaa tena Mo kwa siku kadhaa kwa uchunguzi zaidi? au tukio hili ni kubwa kidogo kwao hivyo watampotezea na maisha yaendelee tu?

Maoni binafsi:
Mo hata hasipotueleza nani walimteka fresh tu, maana hata wao watekaji wanajua tunawajua
 
Hahahaha ushamba wa jiwe utamcost siku moja

Cover story hapa itakuwa ni nini ? Maana hata mtoto mdogo anajua Mo alichukuliwa na kina nani .

Halafu watu wa aina hii ndio wakakae meza Moja na kina Prof Thontorn wa Barrick tutegemee kulipwa na Accasia matrilioni ??

Tutakesha tukisiburia hilo
hahaha
 
Kitakachoondoa mashaka ni Mo kuongea na vyombo vya habari na kujibu maswali. Kama hataongea itakuwa ngumu sana

Kwa hiyo unaamini akina Roma walijiteka? Akina Ulimboka walijiteka?
Akina Ben walijiteka? Azory amejiteka?

Haya mambo mnayajua nyie sisi mbummbu tunawasikiliza. Jambo jema tunauwezo wa kusoma aeio, tunauwezo wa kusoma hadithi japo tunaweza tusilewe. Hata gazeti la uhuru tunasoma vichwa vya habari, ndiyo faida ya shule hasa sisi wa std VII
Hawez kueleza chochote kuhusu watekaji forget it kama unategemea mo ajitokeze kuzungmzia utekaji wake just sleep
 
Hahaa Aibuuuu(. booooooooo) ccm mnaona mwenye kiti wenu anavyo waaibisha "... Muwage na utaratibu wa kuwapima watu akili kabla yakuwapa mamlaka
 
Mungu ni mwema, karibu sana MO uraini.
Pole sana kwa yote yaliyokusibu, Poleni ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi na mashabiki wa MO kwa kipindi chote.

Tuombe Mungu mambo mabaya kama haya yasijitokeze tena kwenye taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania
 
Tuna mshukuru Mungu kwa wema wake mkuu kwani amejibu maombi ya waja wake. Asante Mungu wetu.
 
Back
Top Bottom