Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

hivi huyu ndo aliyeombewa kupewa PHD ktk Uzi Fulani?
 
Naam hapo ndipo pembe za mnafiki zilizogundishwa kwa gundi zinapodondoka na kumuacha akiaibika. Ama kweli mnafiki hana aibu. Watu wanapanga njama za kuabisha wenzao kwa dhana za kutunga!!
 
Achi...
Inatosha mie si mtu wa ubishani.
 
Vita ya majimaji,chini, ya uongozi was kinjekitile ngwale,wale wa piganaji walikuwa wa Islam???,kweli!!!,ushaidi pls
Juan,
Mada hii tumepata kuizungumza kwa kirefu hapa jamvini.
Nakuwekea majibu yangu hapo chini:
Khalidoun,
Haijapata kutokea mnakasha kama ule katika JF.
Hivi ndivyo nilivyofahamishwa na wenyeji walioipokea
barzani.

Wanamajlis,
Naona ukumbi umepoa.

Yuko aliyesema ana maswali kuhusu Nyerere anataka kuniuliza.
Kapotea sijamsikia.

Yuko aliyekuja na mpya kuwa Waislam sio walioanza harakati dhidi
ya ukoloni akataja Maji Maji.

Nikaweka jibu.

Hakuridhika akadai kuwa majibu nimejinukuu mwenyewe kwa hiyo
ni ajua.



Chief Songea Mbano

Nikaja na jibu kutola nyaraka za Wajerumani wenyewe waliopigana
na Chief Abdul Rauf bin Songea.

Najua kapata mshtuko kwa kuwa hajapatapo kumsikia Sultan Abdul
Rauf bin Songea
katika Vita Vya Maji Maji ingawa inawezekana kuwa
kasikia Chief Songea Mbano.

Najua ametatazika kama wengi wanavyotatazika hivi sasa wakinisoma.
Hawa ni watu wawili au ni mtu mmoja?

Abdul Rauf bin Songea ndiyo huyu Songea Mbano?
Kuchakachua historia kuna hatari zake na hii ni mojawapo.

Hakuwa anajua kuwa Vita Vya Maji Maji Waislam walisimama dhidi ya
Wajerumani.

Majemadari 60 Waislam walinyongwa na kuzikwa kaburi moja Mahenge,
Songea na kumbukumbu ya iko hapo kwenye kumbukumbu ya Maji Maji
Songea.

Katika kaburi la peke yake amezikwa Sultan Songea Mbano.
Je huyu ndiye yule Abdul Rauf bin Songea?

Kuna mahali Abdul Rauf bin Songea anaitwa kwa jina la ''Chief Songea
Luwafu Mbano.''


Soma hapo chini:
One of these is Chief Songea Luwafu Mbano, from whom the town takes its name. As the most famous of the Ngoni resistance leaders, the Germans honoured ...





Hii ''Lwafu,'' ndiyo Rauf?
Huyo hapo juu kwenye picha ndiye Chief Abdul Rauf Songea Mbano

Jemadari Muislam wa Vita Vya Maji Maji.
Angalia hapo chini ghafla majina ya hawa Waislam hayaonekani badala
yake kuna majina mengine lakini ni ya wale wale Waislam walionyongwa:




Nani huyu anaepotosha haya majina mazuri ya Waislam katika historia
ya Maji Maji?

Sasa soma hapo chini:
Islam has always been the ideology of resistance against colonial rule or any other authority which tried to subjugate Muslims. Consequently, no government in power either indigenous or foreign has ever been kind or supportive to Islam, and likewise Muslims have always been engaged in a continuous struggle to preserve their faith and fight for their rights. Christianity was resisted by Muslims right from the beginning. In any uprising against the colonial government, Muslims took the opportunity to attack missionaries and Christian establishments. Muslim perceived both missionaries and the colonial government as fellow collaborators and therefore enemies to Islam. Islamic radicalism has therefore a long history in the struggle against colonial rule and Christianity. Christianity became a reactionary force siding with the colonial authority. One needs only to read the letter written by the Chief Songea bin Ruuf at the time when he was mobilising his people for war while at the same time trying to cement alliances with other chiefs in Southern Tanganyika and across the River Ruvuma in Mozambique. This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga reads:


''Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin Hamis Massaninga. Greetings, etc. I am sending you a letter through Kazembe. We have received an order from God that the Europeans must leave the country. We are in the process of fighting them here. I believe that we have long since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an alliance. I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to do so, as the war which God desired is continuing. Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).

I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the means for conquering the Europeans. Have no doubt about it, it possessed great power. And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on the Nyasa together, you and I. Now, let us forget our old quarrels.

This bottle, with a da’wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war leader. He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.

If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you many of the holy things.

Hassan bin Isma’il greets you.
Many salutations,

Sultan Songea bin Ruuf.” [1]

A point to note here is that this letter, beautiful as it is, it is being doubted by Becker, who maintains that the origins of the letter are dubious.[2] This is the stand which many Christian researchers have taken when faced with the realities of Islam in Tanganyika.


[1] C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’, Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p.58.

[2] Ibid.

Angalia jina la Kazembe no. 51 na Hassan bin Ismail no, 53 majina ambayo Chief Abdul
Rauf bin Songea
kayataja katika barua yake.

Angalia neno ''bin'' katika baadhi ya majina kisha jiulize na wapi likawekwa neno ''bin,'' kwa
asiyekuwa Muislam.



Kaburi la Chief Abdul Rauf Songea Mbano katika Maonyesho ya Taifa ya Maji Maji
Mahenge, Songea ambae kazikwa kwa jina la Songea Mbano.

Kutoka: Mohamed Said, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of The Muslim Struggle Against British Colonialism in Tangnayika, Minerva Press, London 1998."[/TD]

Sultan Songea bin Ruuf huyu hapo juu ndiyo huyu anayoelezwa tena hapa chini kama Chief
Songea Mbano?:


"Anasema hali hiyo ilitokea kwa sababu Chifu Songea Mbano alikuwa ndiyo Jemedari Mkuu wa Jeshi la Wangoni na alikuwa ni hodari sana asiyeogopa lolote kwa hiyo Wajerumani walitaka abakie ili wamtumie kwa malengo yao.

"Yeye Chifu Songea alidai na yeye anyongwe kama walivyonyongwa ndugu zake, basi alinyongwa na Wajerumani ambao waliondoka na kichwa chake wakiwa wamekiweka ndani ya kasha kwenda Ujerumani ambako hakijarudi hadi leo na kiwiliwili chake kuzikwa katika kaburi la peke yake."

(Kutoka:Historia Ya Vita Vya majimaji.)
Wanajamvi,
Naamini mnaiona tofauti iliyopo.

Au hawa ni machifu wawili tofauti?
Nani anahusika na uchakachuaji huu wa majina haya ya Kiislam katika historia ya Vita Vya Maji Maji?
 
Kumbe anayofanya Trump yapo nchi mbalimbali kama za Saudia Saudi Arabia puts 30 Shias on trial for spying for Iran - World - DAWN.COM , Qatar, USA, Bahrain, Tanzania, Germany, Turkey, Australia n.k kuwa ukienda nchi Fulani (Iran, Sudan, Yemen) basi tegemea kupata mahojiano ya ziada na usalama wa taifa/uhamiaji ktk viwanja vyao vya ndege/balozi za nchi nyingi kama nilizozitaja hapo juu kwa uchache.

Hapa Mohamed Said anatufahamisha kuwa alifadhiliwa na Marekani ktk baadhi ya safari zake bila kufahamu kuwa inawezekana pia Marekani inatumia mbinu ya ''kumkumbatia '' mtu ili wamuelewe zaidi (intelligence collection) na hata kutuma taarifa zake kwa nchi ''rafiki''.
 
Mkuu Maalim jee ya kweli haya?!. Japo Vatican ni nchi na ina ubalozi wake nchini, uliwahi kusikia kuna viza ya kuingia Vatican?!. Immigation wanaangalia mtu umetoka wapi, visa ni ya Italy, na nadhani ndio nchi iliyokuwa ikiongoza kuuza mihadarati ulaya nzima biashara ikimilikiwa na the Mafia na wote ni Wakristu!.

Nimewahi kusafiri kutoka Tanzania na mzungu fulani lakini ni raia wa Tanzania, tukafika Marekani, wote wawili tukaonyesha passport zetu za Tanzania, mwenzagu akaruhusiwa, mimi nikazuiliwa nikachukuliwa picha na alama za vidole ndipo nikaruhusiwa!. Uhalifu ni uhalifu tuu, hauna dini, rangi wala kabila, japo wanaojilipua wengi ni watu wa dini fulani, hatuwatambui kwa dini yao, bali kwa uhalifu wao!, japo magaidi wengi ni watu wa dini fulani lakini hatuwatambui kwa dini yao bali kwa ugaidi wao!.

Ingefanyika sensa ya dini za wahalifu wote walioko magerezani, amini msiamini, watu mngeshangaa humu na kusema mnazingiziwa!. Tembelea hapa
Mapapa 560 wa Madawa ya Kulevya watajwa. Wamo
Kwenye list hii kati ya majina haya 560, majina 120 ni ya asili ya kizungu, majina 320 ya asili ya Kiarabu, majina 119 ni asili ya Kiafrika na jina moja ni la number ya gari.
Jee wajua what does this mean? .
NB. Naombeni sana msichanganye asili ya majina na dini za watu, majina ni majina tuu na dini ni imani, mtu anaweza kuwa na majina ya asili ya Kiarabu na akawa Mwislamu, au Mkristo na mtu mwenye jina la asili ya Kizungu akawa Mwislamu au Mkristo na wenye majina ya asili nao vivyo hivyo.

Mtu ukiisha tanguliza mawazo hasi ya kunyanyaswa kwa sababu ya dini yako, hata pale utakapofanyika ukaguzi wa ziada wa halali kabisa kwa ajili ya kujiridhisha, utaona una nyanyaswa!. Please stopuni hizi negativity, think positive, hata ukiwa treated harshly, lakiwa ukiwa positive kuwa hilo jambo linafanyika in good faith and not an ill motive, utakuwa na amani ndani ya moyo wako.

Mtu yoyote akiwa ni frequent flyer na safarri zenyewe za nchi za mashaka mashaka, kushukiwa ni kawaida!, mimi siamini ulisachiwa kwa ajili ya dini yako..

Hata hivyo pole kwa masahibu yaliyokufika!.

Paskali
 
Paschal,
Naongea kingine na wewe unaongea kingine.

Ugomvi wangu na Wamarekani ulitokana na paper niliyowasilisha
Chuo Kikuu Cha Ibadan.

Ile paper ilibadili hali ya mkutano na kuionyesha US kama nchi
dhalim na katika Tanzania kupitisha Sheria ya Ugaidi, sheria hiyo
imetumika kwa kuwakamata viongozi wa Waislam na kufunga
taasisi zao kwa uonevu.

Wasikilizaji wakaja juu wakasema sheria hiyo haiwezi kupita Nigeria
kwani hiyo itakuwa serikali imetangaza vita na Waislam.

Kutokana na hali hii Wamarekani wakataka kujua mwandishi ni nani
hivyo wakaleta taarifa Dar es Salaam.

Maafisa wa ubalozi wa Tanzania Nigeria walikuwapo pia kwenye mkutano
ule.

Hii ndiyo sababu ya mimi kukamatwa na kuzuliwa kuwa nasambaza u,nga.
Nia ilikuwa kunipa salamu kuwa, ''Big Brother is watching you.''

Kuanzia hapo ikawa kila safari yangu nje ya nchi napata, ''special tratment,''
''passport control,'' na katika, ''security check'' nikichukuliwa kama ''terrorist
sympathiser.''

Pasi yangu iliwekewa alama ya siri.

Ukipenda soma hii paper hapa:
Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT
 

Airport ipi duniani kupekuliwa mpaka uwe na shahidi?

Hujasafiri nini?

Hiyo ni nyumbani kwako au mitaani.
 
Sasa kama waislam walipigania vita ya uhuru sisi tuliozaliwa baada ya uhuru yanatuhusu nini? Yanatusaidia nini? Sisi tunajua hii nchi inaitwa Tanzania tutaishi hapa kwa Amani na upendo, Story zenu za mkoloni zimepitwa na wakati, Ongelea mambo ya teknolojia na maendeleo, Dini hizi ni propaganda za waarabu na wazungu, Wao wanakula bata mbaya na wanaenjoy maisha nyie wanawavisha makanzu na mabarakashia na Misalaba
 
Leloo...
Nimesema kuwa nitakuwekeeni kidogo maana ni mkasa mrefu.
Sikutaka kuwachosha wasomaji wangu.

Ila ikiwa unataka kujua nini kiliendelea naweza nikakuwekea
kipande cha mwisho In Sha Allah.
Leta kaka tujue kilichojiri
 
http://www.globalresearch.ca/non-mu...0-of-all-terrorist-attacks-in-america/5333619

Shindana na research na kupayuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…