Bagamoyo,
Hayo usemayo si kweli kuwa wanaoingia katika nchi kama Saudi Arabia, Iran nk
wanafanyiwa mahojiano.
Nchi zote hizo ulizotaja nyingi nimefika na sijayaona hayo.
Ikiwa hayo yatafanyika itakuwa makhsusi kwa sababu maalum.
Hao Wamarekani wao wana kawaida ya kutaka kujua kila kitu
duniani na mimi nilikuwa na elimu ambayo wao walikuwa hawana.
Kabla ya kualikwa Marekani nilikuwa katika mradi wa Harvard na
Oxford University Press, New York wa kuandika Dictionary of
African Biography (DAB) kuanzia 2008.
Mradi huu ulikuwa wa kuandika historia ya watu mashuhuri Afrika
waliofanya mambo ya kutukuka.
Waliniletea orodha ya wanasiasa wengi wa Tanzania na kutaka
niwafahamishe ikiwa katika hiyo orodha wao watu, ''remarkable,''
ambao lazima watambulike.
Kazi hii ilikamilika 2011 na buku likatoka lina volume 6.
Kipindi hiki nilikuwa katika mradi mwingine na
Oxford University Press Nairobi kuandika vitabu vya historia kwa shule za msingi.
Labda nnikufahamishe kuwa nilikuwa member wa Library of Congress
toka 1980s.
Makala zangu nyingi zipo hapo Library of Congress.
Kwa hiyo mimi na rafiki zangu Wamarekani hatukukutana barabarani
chembelecho
Edward Lowassa.
Urafiki wetu ni wa miaka mingi.
Tumegombana kwenye suala la Uislam baada ya mie kuandika hiyo
paper ya Ibadan.
Nitakuwekea link ya DAB hapo chini.
Sasa ndugu yangu wewe unajiandikia kwa dhana tu ukidhani kuwa
unajua.
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Library of Congress, Washington DC