Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said

Mimi ni mkiristo niliwahi kusimamishwa hapo airport na kusachiwa kwa madai kwamba nasafari Sana na wanadhani ninajihusisha na madawa.

Nilikalishwa hapo masaa matatu kuulizwa maswali ambayo hayana kichwa wala miguu.
Ndungu zangu waliokuja kunipokea na wenyewe
Wakapigwa maswali ambayo hayana mbele wala nyuma.

Wakaniambia yakwamba watakuwa wanafuatilia mwenendo wangu. sababu hawakupata kitu walichokiwa wanatafuta. mpaka nimeichukia airport ya Dar .

Hata siku moja sijawahi kuwaza wanafanya hivyo sababu mimi ni mkristu. Nilichokuwa nawaza ni kwamba hawa watu wanahitaji elimu kwa vile mtu unasafiri Sana haimaanishi unafanya biashara haramu.-

Thread yako imekosa maana ulipoingiza udini .

Kwa yaliyokupata, ungeweza na wewe kujipigia promo kwamba umesimamishwa na kukaguliwa kwa sababu yoyote ambayo ungeitaja. Lakini nafikiri busara zako zilikuongoza kujua kuwa random check/inspection huwa ni routine kwenye viwanja vyote vya ndege. Wapo waislam na wasio waislam wengi tu wanaokaguliwa na kushukiwa kwenye viwanja hivyo. Na hilo linaweza kutokea hata ukiwa Riyadh au Teheran, Rome au London, Lusaka au DSM, lakini hautasema umeshukiwa kwa vile ni muislam au mkristo.
Huyu kaka anapenda ku-embellish stories kama vile yuko kijiweni. Mara ooh kwa vile ni muislam, mara ooh kwa vile niliwatibua wamarekani kule Ibadan. Hivi kweli Mmarekani angetaka ku-deal naye, angeshindwa kweli kumbambikiza kesi yotote? Si wangemuwekea hata kete mbili tatu ndege ilipokuwa kwenye transit?
Of course lengo lake siku zote limekuwa kuamsha chuki ndani ya jamii.
 
= kinachofanya

Hata historia hii anayotupa Alama Mohamed Said inawaudhi wengi.

Seuse FF anaekupa ilm ya bure.

Ni vigumu sana mtu aliyesomea ujinga kumfundisha akakuelewa - kumbuka hilo.

Seuse=sembuse

ilm=elimu

Asee ni kweli kabisa uyasemayo mwalimu wetu wa ujinga.
 
Kwa yaliyokupata, ungeweza na wewe kujipigia promo kwamba umesimamishwa na kukaguliwa kwa sababu yoyote ambayo ungeitaja. Lakini nafikiri busara zako zilikuongoza kujua kuwa random check/inspection huwa ni routine kwenye viwanja vyote vya ndege. Wapo waislam na wasio waislam wengi tu wanaokaguliwa na kushukiwa kwenye viwanja hivyo. Na hilo linaweza kutokea hata ukiwa Riyadh au Teheran, Rome au London, Lusaka au DSM, lakini hautasema umeshukiwa kwa vile ni muislam au mkristo.
Huyu kaka anapenda ku-embellish stories kama vile yuko kijiweni. Mara ooh kwa vile ni muislam, mara ooh kwa vile niliwatibua wamarekani kule Ibadan. Hivi kweli Mmarekani angetaka ku-deal naye, angeshindwa kweli kumbambikiza kesi yotote? Si wangemuwekea hata kete mbili tatu ndege ilipokuwa kwenye transit?
Of course lengo lake siku zote limekuwa kuamsha chuki ndani ya jamii.
Nanren,
Kifua chako kimejaa joto.
Hebu soma hapo chini wasomaji wapya wakufahamu na wanifahamu na mimi.
Nadhani unazo kumbukumbu ya hayo hapo chini:

Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo
akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.
 
Kwa yaliyokupata, ungeweza na wewe kujipigia promo kwamba umesimamishwa na kukaguliwa kwa sababu yoyote ambayo ungeitaja. Lakini nafikiri busara zako zilikuongoza kujua kuwa random check/inspection huwa ni routine kwenye viwanja vyote vya ndege. Wapo waislam na wasio waislam wengi tu wanaokaguliwa na kushukiwa kwenye viwanja hivyo. Na hilo linaweza kutokea hata ukiwa Riyadh au Teheran, Rome au London, Lusaka au DSM, lakini hautasema umeshukiwa kwa vile ni muislam au mkristo.
Huyu kaka anapenda ku-embellish stories kama vile yuko kijiweni. Mara ooh kwa vile ni muislam, mara ooh kwa vile niliwatibua wamarekani kule Ibadan. Hivi kweli Mmarekani angetaka ku-deal naye, angeshindwa kweli kumbambikiza kesi yotote? Si wangemuwekea hata kete mbili tatu ndege ilipokuwa kwenye transit?
Of course lengo lake siku zote limekuwa kuamsha chuki ndani ya jamii.
Nanren,
Narudi kwako tena kukupa habari za, ''random sampling.''
Hizi ni makhsusi kwa Mohamed Said pekee:

Mkasa huu ulinifika miaka sita iliyopita lakini hadi leo kovu la mkasa
ule limebaki katika pasi yangu.

Sielewi pasi yangu inaonyesha nini inapotiwa katika compyuta baada
ya mkasa huu kwani kama mara tatu husimamishwa kwa muda
nakuombwa nitoe maelezo ya ziada kuhusu niendako kila nisafiripo nje
ya Tanzania.

Nimeshuhudia hali hii Uwanja wa Ndege Amsterdam na Detroit, Marekani.

Berlin, Ujerumani niliambiwa mzigo wangu umepotea lakini hata kabla
sijatoka uwanjani nikatafutwa na kukabidhiwa mzigo wangu na kwa hili
sikuwa peke yangu nilikuwa na mwenzangu, jamaa wa Kiarabu kutoka Misri.

Sijui kama mizigo yetu ilikuwa imebakishwa nyuma kwa upekuzi zaidi.

Amsterdam, Uholanzi baada ya kupita sehemu zote muhimu za upekuzi
wakati naelekea kituo cha mwisho niingie kwenye ndege inayoelekea
Detroit, Marekani nikachopolewa kutoka kwenye mstari na nikawekwa
pembeni peke yangu kwa usaili wa ziada.

New York kadi yangu ya benki ilikataa kutoa fedha kwa siku nzima hadi
siku ya pili.

Nilikujafahamishwa baadae kuwa “system” ilikuwa inanichunguza kwanza.
Ilikuwa siku ya pili baada ya kuonana na maofisa wa benki ndipo kadi yangu
ikaanza kutoa fedha.

Geneva, Uswisi kadi yangu ilikataa kutoa fedha katika mgahawa.
Sikujua kama ni yale yale au haya yalikuwa mengine.

Lakini pasi hii afisa wa uhamiaji wa Tanzania alipoiingiza kwenye computer
yake alimwita mwenzake kuja kutazama kisha wakawa wanacheka.

Waliona nini kwenye pasi yangu Allah ndiye ajuaye.

25th February 2008

Nanren,
Hiyo hapo juu ni ''case study,'' nzuri ya ''random sampling.''
Au unasemaje?
 
Bafa,
Sasa nimekupata.
Hebu soma hapo chini:
Kilichobaki sasa ni kueleza sababu ya mimi kukamatwa. Mwaka wa 2006 Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria kilifanya kongamano la kimataifa hapo chuoni kwao kuzungumza kuhusu Ugaidi katika Afrika ya Mashariki na Maendeleo (Conference on Islam, Terrorism and African Development). Mimi ninlitoa mada iliyokuwa na anuani hii: Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience. Katika mada hii nilijikita mahsusi katika kuisema Marekani kwa udhalimu wao duniani. Nikaeleza kuwa huo udhalimu wao ndiyo unaopelekea wao kuchukiwa dunia nzima. Hapa ningependa kufahamisha kuwa mkutano huu wafadhili wakubwa walikuwa Iran na Marekani. Saudi Arabia ilikataa kuchangia mkutano ule. Wakati nasema maneno haya ya kuwakanyanga wenyewe Waamerika wapo hapo mkutanoni.

Baada ya kuwalani Waamerika sasa nikaigeukia serikali ya Tanzania na kuishutumu vikali kwa kupitisha Sheria ya Ugaidi. Hapa nikaeleza kuwa Waamerika wasione kuwa Tanzania imepitisha sheria hiyo ya ugaidi kwa haraka kwa sababu Tanzania ina tatizo na ugaidi. Nikaeleza kuwa sheria hiyo imepitishwa kwa sababu Bunge la Tanzania limehodhiwa na Kanisa na kupitishwa kwa sheria hiyo hakuna uhusiano wowote na ugaidi ila Wakristo wamepata fursa ya bure ya kupambana na Uislam wakitumia serikali ya Marekani kama upawa wao wa kuopolea chinyango ya moto kwenye chungu kinachotokota. Nikauchekesha mkutano kwa kuwaambia kuwa Wamarekani wamefanywa wajinga na Kanisa kwa kuchonganishwa na Waislam wa Tanzania ambao hawana ugomvi nao asilani. Baada ya kusema hayo nikahitimisha kwa kueleza nguvu ya Waislam Tanzania, kwanza kwa wingi wao na kisha kwa historia yao iliyotukuka iliyodumu takriban miaka mia wakipambana na ukoloni wa Wajerumani kwa silaha (1905 - 1907), kisha ukoloni wa Waingereza (1929 1961) na kuhitimisha kwa kuleta uhuru na kuanzia 1961 hadi sasa wanapambana na nguvu ya kanisa katika kupiga vita Uislam.

Kufikia hapa ukumbi ukawa umepata joto. Wanigeria wamesimama kutaka niwaeleze vipi Waislam watakuwa wamepigania uhuru kisha wako wengi nchini wanaruhusu wao kufanywa raia daraja la pili. Wakashangazwa kuwa hata historia ya mashujaa Waislam waliopigana Maji Maji na kunyongwa na wakoloni na mashujaa walipigania uhuru wa Tanganyika hawatajwi katika historia ya ukombozi. Nilitoa majibu kadri Allah alivyoniwezesha. Nakumbuka kitu kimoja walichosema wale ndugu zetu Wahausa. Walisema hali hiyo iliyoko kwenu haiwezekani kutokea Nigeria kwa kuwa hiyo itakuwa na sawa na kutangaza vita. Kisha wakanihakikishia kuwa sheria hiyo ya ugaidi haitapitishwa Nigeria hata siku moja.

Wapashaji habari wangu wakajanieleza baadae ni hili hitimisho langu ndilo lililosababisha Wamarekani kuleta taarifa Dar es Salaam kutaka taarifa zangu za “ugaidi” ikawa sasa sababu imepatikana ya mimi kushughulikiwa na vyombo vya dola. Ndipo ikatengenezwa hadithi ya kuku na ng’ombe dume (cock and bull story) kuwa Mohamed Said ni Mzungu wa Unga kwa hiyo akamatwe.
Ila mkuu, kwani sheria dhidi ya ugaidi inalenga magaidi au inalenga uislamu? Mimi sioni tatizo la iyo sheria as long as inawalenga magaidi, kwa sababu kama ingekua inalenga waislamu kura za bungeni zingekua 50% kwa sababu almost idadi ya waislamu na wakristo bungeni inakaribia kua sawa. Kama sheria inalenga magaidi, haijalishi kwamba uyo gaidi ni mkristo, mpagani, myahudi au muislamu, wote watashughulikiwa.
 
Ma sha Allah, Alama mwaga darsa.

Wanakuja na wanakusoma, kukosa hawawezi na wanashangaa, hawakuyajuwa yote hayo.

Nnamuuliza Sooth juu hapo, hivi huyu Mohamed Said anatwambia Songea Mbano eti anaitwa Abdul Rauf , simuelewi-elewi
Kwa fikra kama hizi, mtu mweusi atausikia ukwasi redioni na kwa wazungu. Jifunze tofauti ya utajiri na ukwasi ndipo utaelewa maana ya kutumia fursa.


Msalimie Al Haj Dangote.
 
hahahaaaa!

i read you, h*a*r*l*o*t....


What a great title.

You know in the holy bible harlots are saints and very fortunately (or is it unfortunate) they are the ancestors of Jesus in the so called "genealogy of Jesus", Imagine a man without a father who was born miraculously given a genealogy of all males except one woman who is a harlot according to THE bible. You know her name?
 
What a great title.

You know in the holy bible harlots are saints and very fortunately (or is it unfortunate) they are the ancestors of Jesus in the so called "genealogy of Jesus", Imagine a man without a father who was born miraculously given a genealogy of all males except one woman who is a harlot according to THE bible. You know her name?
google baby....google!

i love you! mwaaa!
 
Sijuwi ni nani alikubagua?

Maana katika historia ya kivukoni sikuona "hawa wazee" waliokuwa "kitu kimoja" kutajwa bali niliona superman mmoja tu akitajwa kuwa ndiye aliyekuwa mdai uhuru pekee wa Tanganyika. Au wewe uliwaona?

Bado hujajibu swali langu, jee, uliwahi kumsoma Mshume Kiyate?

Ukimaliza unaweza kutupa kidogo historia ya vita vya maji maji? Maana nnaona huyu Mohamed Said anatupiga porojo tu eti anadai kuwa Songea Mbano anaitwa Abdul Rauf! mimi simuelewi-elewi, vipi wewe?
Tanzania ni zaidi ya Kariakoo. Tokeni Kariakoo muende huku na kule muifahamu nchi yenu. Faiza na Mzee Said mnapenda kuonyesha ubaguzi wenu waziwazi kwa watu wasiohusika na shutuma zenu. Kwa nafasi zenu ktk jamii na watu mnaofahamiana nao mnaweza kurekebisha yote mnayonung'unikia bila kujenga chuki za kidini.
 
google baby....google!

i love you! mwaaa!

I love you too and I love google more than you.

Yes its me, many have told me before "you are a walking encyclopedia". Calling me google is new but isn't google an open encyclopedia? Does not surprise me at all.

Believe you me, I will never cease to amaze you.

Keep it up.

Jee, umewahi kumsoma Mshume Kiyate?
 
Ila mkuu, kwani sheria dhidi ya ugaidi inalenga magaidi au inalenga uislamu? Mimi sioni tatizo la iyo sheria as long as inawalenga magaidi, kwa sababu kama ingekua inalenga waislamu kura za bungeni zingekua 50% kwa sababu almost idadi ya waislamu na wakristo bungeni inakaribia kua sawa. Kama sheria inalenga magaidi, haijalishi kwamba uyo gaidi ni mkristo, mpagani, myahudi au muislamu, wote watashughulikiwa.
Pragizzle,
Ahsante sana kwa mchango wako.

Uzuri wako wewe ni kuwa huna ulijualo katika hili somo ndiyo maana umeweza
kuandika kuwa hata Yahudi anaweza kuwa gaidi katika mada hii ambayo ingekuwa
makini kidogo ungejua inahusu Tanzania na Waislam wa Tanzania na serikali yao na
wala usingechanganya na mambo ya kura, uchaguzi nk.

Inaelekea hujui chochote katika hayo unayoandika mathalan idadi ya Waislam na
Wakristo katika Bunge na mengi mengine.

Hivi unajua kuwa hakuna hata Musilam mmoja aliyepelekwa mahakamani na hukumu
ikatolewa katika kesi zote hizo za ugaidi?

Lakini mimi ningependa uelimike katika haya ambayo unachangia lakini huyajui.
Hii ni post niliandika miaka mitatu iliyopita hapa JF:

Rajab Omar Mtana alikuwa ni mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake kuuza hiliki. Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara ya hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia. Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru. Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote. Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka. Hii ikapelekea kwa wakusanya ushuru kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapo atakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe. Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano. Katika mapigano hayo, mgambo ajulikanae kwa jina la Mbwana ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa. (Kisa hiki kipo humu na kimeelezwa kwa ufasaha na Sheikh Chambuso wasomaji mnaweza mkakisikiliza kupitia ''gallery.'' Tunatayarisha muhtasari wake na tutauweka hapa In Sha Allah). Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa Madina na kuvunjwa kwa misikiti na vijiji ambavyo vilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wake Waislam. Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu ile kuwa makazi kwa kisingizio kuwa hizo ni kambi za ugaidi. Huyu bibi alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika kuwa ni uongo mathalan kuwa kuna Al Shabab, mahandaki ya vita, silaha za kutungulia ndege nk. nk.

a8w2NBNWF2QNINF3Oo4CmAtwSZVrn-X4OCuXNwG1ots=w571-h576


Chiku Galawa Mkuu wa Mkoa wa Tanga

Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana. Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje. Mwezi uliopita Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake. Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu. Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake. Lakini nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake. Akiwa nyumbani kwa dada yake usiku alifatwa na watu wa serikali ya kijiji wakiongozwa na mgambo wawili, Salimu Magingu na Salimu Mnyendo, akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga. Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akifukuzwa. Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana. Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika. Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika ''mahakama'' ya hapo kijiji na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000. Kosa lao ni kumleta kijiji mtu asiyetakiwa. Sasa ni mwezi mmoja Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake. Ndugu yetu Rajab ametafutwa kote hadi leo hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi. Wakati Sheikh Chambuso alipokuwa akinighadithia mkasa huu ilinijia picha ya kisa cha vijana watatu waliouliwa na Klu Klux Klan Mississippi katika miaka wa 1960 wakati wa ubaguzi wa rangi Marekani. Waliuliwa kama vile mtu kauwa paka msumbufu na hakuna lolote lililofanyika hadi zilipotiwa juhudi za ziada kutoka nje ya Mississippi ndipo wauaji wakatiwa mbaroni. Mauaji ya Madina yamepita hivi hivi hakuna aliyesimamishwa mbele ya vyombo vya dola. Uwezekano mkubwa ni kuwa na mauaji haya yatafata mkondo ule ule. Jambo la kusikitisha ni kuwa mauaji haya yamelenga watu wa dini moja. Je, viongozi wetu wako hadhiri na mbegu hii wanayoiacha imee?

Fatilia kisa hiki kuna mengi ya kusikitisha...

Msikilize Sheikh Chambuso akikieleza chanzo cha kadhia iliyopelekea yote haya - Waislam kuhamishwa kwenye vijiji vyao, kuchomwa moto misikiti na mauaji yanayoendelea hivi sasa:

 
Back
Top Bottom