Kwa yaliyokupata, ungeweza na wewe kujipigia promo kwamba umesimamishwa na kukaguliwa kwa sababu yoyote ambayo ungeitaja. Lakini nafikiri busara zako zilikuongoza kujua kuwa random check/inspection huwa ni routine kwenye viwanja vyote vya ndege. Wapo waislam na wasio waislam wengi tu wanaokaguliwa na kushukiwa kwenye viwanja hivyo. Na hilo linaweza kutokea hata ukiwa Riyadh au Teheran, Rome au London, Lusaka au DSM, lakini hautasema umeshukiwa kwa vile ni muislam au mkristo.
Huyu kaka anapenda ku-embellish stories kama vile yuko kijiweni. Mara ooh kwa vile ni muislam, mara ooh kwa vile niliwatibua wamarekani kule Ibadan. Hivi kweli Mmarekani angetaka ku-deal naye, angeshindwa kweli kumbambikiza kesi yotote? Si wangemuwekea hata kete mbili tatu ndege ilipokuwa kwenye transit?
Of course lengo lake siku zote limekuwa kuamsha chuki ndani ya jamii.
Nanren,
Kifua chako kimejaa joto.
Hebu soma hapo chini wasomaji wapya wakufahamu na wanifahamu na mimi.
Nadhani unazo kumbukumbu ya hayo hapo chini:
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu
Salum Abdallah.
Hakuwekwa kwa ajili ya dini.
Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955
Kasanga
Tumbo akiwa katibu.
TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.
Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.
Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.
Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na
Makhan Singh Kenya.
Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.
Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.
Kuwekwa kwao ndani ilikuwa
Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.
Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu
Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.
Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962
Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.
Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.
Nyerere hakufurahishwa na yeye.
Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.
Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa
Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.
Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.
Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.
Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.
Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.
Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.