Tanzania ni zaidi ya Kariakoo. Tokeni Kariakoo muende huku na kule muifahamu nchi yenu. Faiza na Mzee Said mnapenda kuonyesha ubaguzi wenu waziwazi kwa watu wasiohusika na shutuma zenu. Kwa nafasi zenu ktk jamii na watu mnaofahamiana nao mnaweza kurekebisha yote mnayonung'unikia bila kujenga chuki za kidini.
Sooth,
Una joto la kifua linakuzonga.
Huu ni mjadala wa historia ya uhuru wa Tangnayika na mfano wa hayo.
Huna cha kuchangia katika mjadala huu unaleta yasiyokuwapo.
Unadhani siijui nchi yangu unaandika kwa dhana tu.
Mimi nina kitabu kizima kuhusu historia ya Tanganyika na it is ''the book.''
Mimi nilikuwa Mtafiti Msaidizi wa
Dr. Harith Ghassany wakati anaandika
kitabu chake cha historia ya Zanzibar, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''
Harvard wameniletea orodha ya majina ya watu mashuhuru wa toka enzi
ya Tanganyika niwashauri ni majina gani yaingie katika Dictionary of African
Biogrpahy (DAB).
Bado niwe sijui mjuaji uwe wewe?
Ati nitoke Karikaoo...
Naujua ulimwengu.
Nimekuambia soma zile rejea
Sivalon kamtaja mbaguzi.
P van Bergen kamtaja mbaguzi na wala si sisi.
Njozi kaeleza ubaguzi unavyotendeka umeita, ''myth,'' na ''conspiracy
theory.''
Katika kitabu cha
Sykes kuna topic ya ''conspiracy theory,'' ungependa
niweke hapa Majlis wana jamvi wasome nini nimesema?
Ushamsoma
Sheikh Suleiman Takadir na ukajua ni nani katika kupigania
uhuru wa Tanganyika?
Mimi na
Maalim Faiza tuko hapa kutoa Elimu Bila Khiyana.