Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Status
Not open for further replies.
tuache ujinga sasa ,sisi sote ni ndugu hakuna dini,kabila wala tabaka bora ktk jamii yetu ,tupambane Na uchumi tulionao
Muislamu ndugu yake muislamu! Hicho ndicho waliambiwa, hata siku moja usifikiri muislamu ndugu yake atakuwa mkristo(kama unanielewa, ila kutokana na maisha yalivyo hawana jinsi tu)
 
Unabii hautafsriki hivyo Mkuu. Basi unabii mwingine unasema nchi zote zinazotegemea mafuta zitakuwa mufilisi muda siom mrefu sana. ZITAKUWA CHOKA MBAYA. Kwa mabadiliko ya teknolojia na magari ya umeme na nishati mbadala we unaonaje ? SIO NDIO MWELEKEO, hata Saudi Arabia ameanza kuwekeza kwenye bishara tofauti. Hiyo nguvu wakati wako mufilisi choka mbaya itatoka wapi au kwa Ibilisibin Shetuani bin lucifer

Kuna mahali nimeandika hayo maneno "choka mbaya"? What have you been drinking?
 
Nyerere hakuanzisha chama. Nyerere alikaribishwa na Wazee wa Dar. Akina Sykes. Chama aanzishe Nyerere jina la chama atowe Abdul Wahid Sykes na Ally Sykes?
Sasa huyo nyerere aliwazidia wapi hadi kuja kuwaongoza humo chamani?
 
Ni Biblia gani hiyo ya wapi inatumika katika dini gani au dhehebi gani iliyoutaja uislamu kwenye maandiko yake?
Kumbuka uislamu upo mwaka 1440 sasa ukristo una miaka zaidi ya 2000.
Katika Ukristo sisi ni watu wa uzima hatuneni mauti tena wala dhambi Kristo Yesu alishayashinda hayo na sisi watu wa mataifa tumekombolewa kupitia damu yake.
Huwezi kumsikia Mkristo anaongea au anawaza kuchinjwa, kupigwa mawe, ama kufa siku atakayorudi Messiah ama sasa! kwa sababu hatuna Torati tena tuna habari njema Kristo katuweka huru.
Ukristo hauna maandiko popote yakumlazimisha mtu kuwa Mkristo kwa vitisho Mungu huwa anajipambanua kwa namna yake Kama alivyofanya kwa mzee wetu Remy Ongala.

Rudia tena kusoma nilichoandika kwenye hiyo post yangu uliyoijibu. Hakuna nilipoandika kuwa Wakristo watachinja au watalazimisha watu wawe Wakristo.
Btw; soma vitabu nilivyovitaja.
 
Kuna mahali nimeandika hayo maneno "choka mbaya"? What have you been drinking?.
No No No sijasema wewe umesema mi ndio nakuambia hao waarabu wataakavyo filisika mafuta yatakuwa sio dili tena I drink only water. Have a good day
 


Kwanza napenda ifahamike kuwa dhumuni la kuipandisha clip hii hapa ni kumpinga huyo anaejiita "Sungura Media" aliyeipandisha clip hii youtube na kuandika kuwa eti ni "video ya siri". Haya mafundisho ya historia ya Alama Mohamed Said siyo siri, yapo mtandaoni, yapo kwenye tovuti yake na yameshajadiliwa sana hapa JF.

Mfahamu Alama Mohamed Said:

Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe 25 Februarikatika mwaka wa 1952 huko Gerezani jijini Dar es Salaam - ambapo ndiko kulikokuwa na asili ya upinzani dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini Tanganyika katika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways. Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa Nyerere kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere. Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika Chuo Kikuu cha Wales huko mjini [[Cardiff, Uingereza na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).


Utafiti juu ya historia ya uhuru wa TangayikaEdit

Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi. Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa. Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).


Tazama piaEdit



Viungo vya Nje

Chanzo: https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Mohamed_Said

cc: Mohamed Said

Halafu baada ya kuwa chama cha kiislamu ikaishiaje?
Sterling akafa kabla movie haijaisha?
 
Chama ni cha waislamu, ila anakuja mkristo anawaburuza humo alafu mpo tu mnabaki kulialia!yaani ni sawa na leo gwajima aongoze bakwata na kuwaburuza
Yani mtu anajitapa kabisa kwamba "TANU kilikuwa chama cha Waislamu" kama hiyo ni sifa nzuri ya kujivunia?

Mtu anaona udini ni sifa nzuri?

Wale wazee wa TANU wa Pwani walikuwa na akili sana kujua kwamba, ingawa wao wengi walikuwa Waislamu, walihitaji kiongozi mwenye elimu dunia pana na upeo wa kwenda nchi nzima kuhamasisha watu, na kwenda UN kudai uhuru kwa hoja za kifalsafa zitakazoeleweka kimataifa.

Hawakukosea kumchagua Nyerere, licha ya kwamba hakuwa Muislamu mwenzao.

Ukimsikiliza Nyerere na hoja zake za "Enlightenment Philosophy" za watu kama John Stuart Mill, utaona alijua kuongea lugha ya falsafa ya wakoloni na kuwazidi kwa hoja katika kudai uhuru, kitu ambacho wazee wa Kiislamu wengi wa Pwani (sio wote, wengi) hawakuweza.

Wazee walikuwa na akili ya kujua kwamba tofauti za dini hizi, dini za kuletewa na wageni, zisitufanye Wwaafrika tugawanyike.

Nyerere naye alivyopata madaraka ya kuendesha nchi, akasema hataki kujenga nchi yenye matabaka ya watu, tabaka la waasisi wa TANU na tabaka la wengine, tabaka la machifu na tabaka la wengine. Akavunjilia mbali Uchifu. Akaondoa habari za waasisi wa TANU kujiona wako juu ya wengine. Aapotezea waasiskataka kujenga jamii yenye usawa kwa wote. Hapo ndipo wengine wanatafsiri kwamba aliwapotezea waasisi wa TANU.

Msikilize Nyerere anamwaga madini kipindi cha former first lady wa US, Eleanor Roosevelt, mwaka 1959 katika safari zake za UN.

Sasa wazee wa Kiislamu wangapi wangeweza kujichanganya kimataifa hivyo wakati huo?

 
Kwa mfano vimondo angani ni mizinga anayotumia allah kumzuia shetani asiingie mbinguni..
Jua kuzama kwenye dimbwi la maji machafu,mohamed kupasua mwezi vipande viwili,mohamed kupaa na farasi hadi mbinguni
Hahaha hahahaha.........!

Ila tuache Utani Mudy alikuwa Mjinga sana
 
Rudia tena kusoma nilichoandika kwenye hiyo post yangu uliyoijibu. Hakuna nilipoandika kuwa Wakristo watachinja au watalazimisha watu wawe Wakristo.
Btw; soma vitabu nilivyovitaja.
Umetaja kitabu cha Daniel ambacho ni agano la kale na Ufunuo wa Yohana ambacho ni agano jipya hivi vyote havina neno uislamu.

Na Bible nzima haina neno uislamu na haijawahi kutabiri ujio wa Nabii mwingine zaidi ya Kristo Yesu alivyotabiriwa.

Leta ushahidi wa Mstari wa Bible ulioutaja ama kuutabiri uislamu simple
 
Moja ya mambo muhimu sana katika masuala mazima ya imani tena ndani ya nchi yetu hii,nafikiri inatupasa tukiwa tunayajadili basi tuwe makini sana kwani sisi watz wengi wetu tumekuwa ktk mazingira ya ukaribu sana between ukri/uisla.hata familia zetu zinaingiliana kwa namna moja au nyingine, basi ombi langu upendo na umoja wetu ktk imani ndio uliotufanya tunaweza kuishi nyumba moja,kazi moja,tunakula pamoja na tunashirikiana kwa mengi tu.Tumlani shetani kwa kuachana na malumbano ya kidini.
 
Ndiomana Narudia kusema..
Dini inawafanya watu kua mambumbumbu yakutupwa..Dini imewageuza watu misukule na watumwa wa akili na miili yao..

Dini/Cults ni vyama vya siasa..waliojimilikisha umungu
 
Wazee waasisi wa TANU si ndio wazee wa DSM ambao wanatambulika hadi leo.?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom