Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Status
Not open for further replies.
Naomba unipe huo ushahidi wa upuuzi ndani ya Quran baada ya wewe kuisoma kwa kina, ili niufahamu na kuutafakari.
Kwa mfano vimondo angani ni mizinga anayotumia allah kumzuia shetani asiingie mbinguni..
Jua kuzama kwenye dimbwi la maji machafu,mohamed kupasua mwezi vipande viwili,mohamed kupaa na farasi hadi mbinguni
 
Mkuu jitahidi kuinua kiswahili na kiingereza chako, nadhani hoja yako itaeleweka vizuri zaidi.
Hicho Kingereza ni "Copy n paste" kutoka Google, muhimu kuwa umefahamu kwanini Waislam wanasema Mtume yote ilikuwa Waislamu, Uislamu umeanzia tangu mwanzo wa Dunia..

Musa alisema "Mungu ni mmoja"
Isa kasema Mungu ni Mmoja
Muhammed kasema Mungu ni mmoja..

Hiyo ndio maana ya neno "Islam",= kujikubalisha kwa Mungu kwa chochote kile
 
Kwanza napenda ifahamike kuwa dhumuni la kuipandisha clip hii hapa ni kumpinga huyo anaejiita "Sungura Media" aliyeipandisha clip hii youtube na kuandika kuwa eti ni "video ya siri". Haya mafundisho ya historia ya Alama Mohamed Said siyo siri, yapo mtandaoni, yapo kwenye tovuti yake na yameshajadiliwa sana hapa JF.

Mfahamu Alama Mohamed Said:

Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe 25 Februarikatika mwaka wa 1952 huko Gerezani jijini Dar es Salaam - ambapo ndiko kulikokuwa na asili ya upinzani dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini Tanganyika katika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways. Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa Nyerere kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere. Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika Chuo Kikuu cha Wales huko mjini [[Cardiff, Uingereza na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).

Utafiti juu ya historia ya uhuru wa TangayikaEdit

Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi. Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa. Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).

Tazama piaEdit

Viungo vya Nje

Chanzo: https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Mohamed_Said

cc: Mohamed Said
Yaani huu upuuzi umerudi tena!
 
SUALA LA IPI IDADI KUBWA TUIACHE VYENGINEVYO LILETENI KTK SENSA MBN MLIKATAA
JK alikuwa Rais muislam ndie aliekataa Sio Sisi. Ukweli ndio huo waislam ni wachache Tanzania
 
Hivi we dada FaizaFox, kujilipua na mabomu na kuua watu wasio na hatia ndio salama ?
 
Nyerere hakuanzisha chama. Nyerere alikaribishwa na Wazee wa Dar. Akina Sykes. Chama aanzishe Nyerere jina la chama atowe Abdul Wahid Sykes na Ally Sykes?
Nyerere alitaka kuanzisha Chama, ndio akaambiwa kuhusu TAA.

Ni kweli Wazee wako wa Dar walianzisha chama lakini chama kilikuwa dormant, na Mwalimu alialikwa na Mzee Mwangosi baada ya kumshauri asianzishe chama.

Hivi kwa mtazamo tu wa kawaida kama Mwalimu angeanzisha Chama, kile cha Wazee wa Dar kingefua dafu kweli? nadhani Wazee wetu wale walitumia akili sana.

Kuhusu TANU ni baada ya kukaa mezani ndio kina Sykes wakaja na jina la hilo kwa kuwa walishalifikiria awali wakiwa Burma, hivyo wote wakakubaliana.hivyo hapa si chama kilianzishwa bali ni jina yeyote angeweza kutoa wazo na kuungwa mkono.
 
Uchochezi uliopitiliza huo.
Maalim Said ni mdini kweli kweli,keshawapotosha watu wengi kwa mtazamo wake binafsi.
Kwa kweli huwa simfurahii .
 
Nyerere alibebwa na Waislam kufika alipofika kisha akawageuka Bibi Titi Mohammed alimfunga kifungo cha maisha kwa kupingana nae baada kumuona ameageuka.

Jina la Bibi Titi likaondoshwa katika historia ya wanaharakati walio dai UHURU wa Tangannyika.

Mwinyi kwa kuujua ukweli ndio aliekuja kumwachia huru na angalau akapewa jina la Mtaa mmoja kama kumbukumbu ya juhudi yake.

Takadiri (ambae mchonga akampachika jina la MTAKADINI)
Vilevile ni mfano mwengine wa wahanga hawa wapo wengi.
Una uhakika aliye mweka hru Bibi Titi ni Mwinyi,
 
Kama Nyerere aliua Uislam kweli Tanzania
Basi aliona mbali sana

Maana nikiona demand wanazotaka Waislam huku Tz Bara halafu ukilinganisha na wanachowafanyia wasio Waislam kule Zanzibar, utaona kabisa hawa watu wakiwa na nguvu sana lazima amani ya nchi itatetereka tu au watajaribu ku Islamize nchi nzima

Waislam mtaona kama nina chuki na nyie ila huu ni ukweli unaouma mtanisamehe

Mfano, India na Pakistan zilikuwa nchi moja chini ya utawala wa Mwingereza, ila kutokana na demand za Waislam na vurugu zao ikabidi waigawe iwe nchi Mbili, Waislam wakaenda Pakistan, Wahindu wakabaki India

Pakistan leo hii wote tunajua ni nchi ya aina gani
Dini kubwa zote ni siasa za kale zilizogubikwa joho la utakatifu wa Mungu asiyeonekana wala kuthibitishika.

Uislamu ni harakati za kisiasa za kuitawala dunia, zaidi ya dini tu kama inavyoeleweka kawaida. Ndiyo maana kuna mambo ya caliphate wanataka kutawala dunia.

Ukristo nao umejieneza kwa falsafa ya kumhubiri Yesu dunia nzima, sasa Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote kwa nini ahubiriwe ili aeleweke kwa viumbe wake mwenyewe?

Ukristo umeenezwa kwa nguvu ya dola ya Kirumi. Biblia yenyewe ilivyowekwa pamoja imewekwa pamoja katika mkutano unaitwa "The Council of Nicea". Mfalme Constantin wa Roma aliagiza maaskofu waamue kitabu kipi kiwekwe kwenye biblia na kipi kisiwekwe. Vitabu ambavyo havikuwa na habari nzuri kwa mfalme vilitupiliwa mbali, vitabu vilivyokuwa viizuri kwa mfalme na ufalme ndivyo vikawekwa katika biblia, leo hii watu wanasoma Biblia na Quran kama vitabu vya Mungu, wakati vitabu vimeandikwa na watu tu. Na utajua hilo ukiangalia makosa ya kimantiki mengi sana yaliyo katika vitabu hivi.

Ukiangalia hata Asia, kwenye dini ambazo kinadharia zina level ya compassion kubwa zaidi ya Uislamu na Ukristo, dini kama Buddhism, utaona nako dini zinaleta matatizo. Waislamu wa Burma/ Myanmar wanaonewa sana (Rohingya Muslim minority) wanauawa na kufanywa wakimbizi. Wa Buddha wa Myanmar wanawaua vibaya sana, ingawa katika kanuni za U Buddha hutakiwi hata kuua sisimizi.

Ukichunguza sana utaona mwanzo wa dini ni wafalme (Babylon, Egypt, China mfalme alikuwa anabudiwa kama Mungu, maelfu ya miaka kabla Uyahudi Ukristo na Uislamu haujaanza).

Dini kubwa zote ni siasa za kale zilizogubikwa joho la utakatifu wa Mungu asiyeonekana wala kuthibitishika.

Dini ni vyama vya siasa vya zamani sana.

Ukielewa hili, mengine ni detail tu.
 
Saudi Arabia nchi takatifu ya dini ya kiislamu leo kuna watu wana chinjwa kama mbuzi kisa wanatuhumiwa kwamba ni magaidi.Pengine shangazi yetu anapenda na nchi yetu iwe na adhabu kama za huko Mecca.
 
Kama Nyerere peke yake aliweza kuwaburuza waislam katika chama chao, unawategea wangeweza kupambana na mkoloni kwa hoja?!
Ha ha ha ha ha ha ha we jamaa noma sana! Yaani nyerere aliwaburuza kwenye chama chao, alafu hapohapo wanasema wamepigania uhuru kutoka kwa mkolono(mzungu) ambae alikuwa na kila kitu kuliko nyerere! Nyerere aliwawezaje hawa??
 
Agano la kale = Taurat
Una matatizo unahitaji taarifa sahihi si hizo ulizonazo potofu.

Katika Biblia takatifu ya agano la kale kuna vitabu vitano tu vya Torati
(1) Mwanzo
(2) Kumbukumbu la Torati
(3) Mambo ya walawi
(4) kutoka
(5) Malaki

Vilevile kuna vitabu vya manabii vingi sana
(1) Habakuki
(2) Nehemia
(3) Samuel
(4) Hosea
(5) Zaburi
N.k

Tuna vitabu vya mataifa
(1) Wafilipi
(2) Waefeso
N.k
Sasa jifunze kupata taarifa sahibi Biblia ya agano la kale si Torati
 
Ha ha ha ha ha ha ha we jamaa noma sana! Yaani nyerere aliwaburuza kwenye chama chao, alafu hapohapo wanasema wamepigania uhuru kutoka kwa mkolono(mzungu) ambae alikuwa na kila kitu kuliko nyerere! Nyerere aliwawezaje hawa??
Elimu! Elimu! Elimu!
 
Saudi Arabia nchi takatifu ya dini ya kiislamu leo kuna watu wana chinjwa kama mbuzi kisa wanatuhumiwa kwamba ni magaidi.Pengine shangazi yetu anapenda na nchi yetu iwe na adhabu kama za huko Mecca.
Why not ??
 
Dini kubwa zote ni siasa za kale zilizogubikwa joho la utakatifu wa Mungu asiyeonekana wala kuthibitishika.

Uislamu ni harakati za kisiasa za kuitawala dunia, zaidi ya dini tu kama inavyoeleweka kawaida. Ndiyo maana kuna mambo ya caliphate wanataka kutawala dunia.

Ukristo nao umejieneza kwa falsafa ya kumhubiri Yesu dunia nzima, sasa Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote kwa nini ahubiriwe ili aeleweke kwa viumbe wake mwenyewe?

Ukristo umeenezwa kwa nguvu ya dola ya Kirumi. Biblia yenyewe ilivyowekwa pamoja imewekwa pamoja katika mkutano unaitwa "The Council of Nicea". Mfalme Constantin wa Roma aliagiza maaskofu waamue kitabu kipi kiwekwe kwenye biblia na kipi kisiwekwe. Vitabu ambavyo havikuwa na habari nzuri kwa mfalme vilitupiliwa mbali, vitabu vilivyokuwa viizuri kwa mfalme na ufalme ndivyo vikawekwa katika biblia, leo hii watu wanasoma Biblia na Quran kama vitabu vya Mungu, wakati vitabu vimeandikwa na watu tu. Na utajua hilo ukiangalia makosa ya kimantiki mengi sana yaliyo katika vitabu hivi.

Ukiangalia hata Asia, kwenye dini ambazo kinadharia zina level ya compassion kubwa zaidi ya Uislamu na Ukristo, dini kama Buddhism, utaona nako dini zinaleta matatizo. Waislamu wa Burma/ Myanmar wanaonewa sana (Rohingya Muslim minority) wanauawa na kufanywa wakimbizi. Wa Buddha wa Myanmar wanawaua vibaya sana, ingawa katika kanuni za U Buddha hutakiwi hata kuua sisimizi.

Ukichunguza sana utaona mwanzo wa dini ni wafalme (Babylon, Egypt, China mfalme alikuwa anabudiwa kama Mungu, maelfu ya miaka kabla Uyahudi Ukristo na Uislamu haujaanza).

Dini kubwa zote ni siasa za kale zilizogubikwa joho la utakatifu wa Mungu asiyeonekana wala kuthibitishika.

Dini ni vyama vya siasa vya zamani sana.

Ukielewa hili, mengine ni detail tu.
Dini ni sanaa

Biblia /Quran ni magazeti ya zamani Kama Leo tuna mwananchi, uhuru, Tanzania daima n. K
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom