Mkuu Dada yangu, nikuzimiaye, Faiza Foxy, kwanza asante kutuletea hii clip ya Redio Kheri, yenye maurongo wa Mzee wetu na member mwenzetu Maalim Mohamned Said, maana bila wewe kuileta humu, akina sisi, tusingejua jinsi mnavyodanganyana humo na kufanya uchochezi kwenye hizo redio zenu za dini!.
Kwa kuanzia tuu, kuanzia headline ya bandiko hili ni urongo, Tanu hakijawahi kuwa ni chama cha Kiislamu, kuanzia kuasisiwa kwake, hakuna Muislamu yoyote aliwahi kuasisi chama chochote cha kupigania uhuru wa Tanganyika, Tanu ilitokana na TAA, ambayo ilitokana na AA. Muasisi wa AA ni Mkristo Cecil Kalaghe, muasisi wa TAA ni Mkristo Dr. Kyaruzi, na muasisi wa Tanu ni Mkristo Mwl. Julius Kambarage Nyerere, tangu AA, TAA hadi TANU, hakuna wakati wowote vyama hivi viliwahi kuwa vya dini fulani, ila kitu ambacho ni kweli, Tanu ilimuwa na members wengi Waislamu kuliko Wakristu, ila nguvu ya chama chochote ni logistical support, mfadhili mkuu wa Tanu ni Mkristo tajiri Mzee John Rupia, na sio wale masikini wa Gerezani japo pia tusiudharau mchango wao wa senti 5 ya samaki, senti 10,senti 20 ya mbuni, thumuni ya sungura, na shilingi ya mwenge, enzi hizo, noti ni ya shilingi 5, 10,20, 50 na noti kubwa ilikuwa Sh.100 ya masai.
Nimeisikiliza yote nikakuta ...Du...!, mnapigwa kamba kweli kweli na Mzee wetu huyu...
huu ni muendelezo wa ule ule urongo wa siku zote wa uchochezi wa udini, kusingizia kitu cha urongo marehemu kina karma kali sana!.
Japo namheshimu sana Maalim Mohammed Said, kitu pekee mimi ninachotofautiana nae ni matumizi ya takwimu za urongo ili kupush forward agenda zake ovu za uchochezi wa udini.
Kwenye mahojiano hayo, ameongopa kuwa 76% ya wabunge wa Bunge la JMT, ni Wakatoliki,18% madhehebu mengine ya Kikristu yaliyobakia, halafu Waislamu ni just 6%!. Huu ni urongo wa kiwango cha lami mchana kweupe. Mtu huhitaji kufanya sensa ya Wabunge Waislamu kujua huu ni urongo, bila hata sensa, Wabunge wote kutoka Zanzibar ni Waislamu ambao kabla hujawajumlisha wabunge Waislamu wa bara, hao Wanzibar tuu wenyewe wanafanya theluthi moja ya Wabunge wote!. Huu ni urongo!.
Hata kwa kutumia tuu just ordinary common sense, inakuja kweli akilini, 76% ya wabunge wakawa ni Wakatoliki?!,this doesnt make sense to me, this is non sense, just bull shit!.
(ashakum for this)
Ukiwa na asilimia 99% ya ukweli, na just 1% ya urongo, huo urongo una nullify ukweli wote wa hoja zake kuzifanya null and void ab initio.
P.