MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU

MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU

Taasisi ya tiba ya mifupa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) imesema Mwanaume aliyeonekana akigongwa na Basi la abiria “mwendokasi” Jijini Dar es salaam jana, amelazwa Hospitalini hapo kwenye chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha MOI Patrick Mvungi ameiambia AyoTV kuwa Mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ kwa sababu mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi.

Mvungi ameongeza kuwa mpaka sasa Mtu huyo ambaye amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani hawezi kuongea lakini anafungua macho.

Pia soma: Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road
Kwa ajali ile nafasi ya kupona kibaolojia ni asilimia 1% nje ya hapo Nguvu za Mungu ziingilie kati uhai wake.. kwenye ajali ile dereva wa RAV 4 ndiye ana hatia ya kujibu duniani na mbinguni.. ile ngoma ya kwake na uzao wake wote..
 
Duh asee huyo jamaa jana tumebishana humu nikawa nasema atakuwa lazima alikufa.

Ila kama hakufa basi ni maajabu yenyewe. Kama hali yake inaendelea poa ni jambo la kushukuru Mungu.

RRONDO Mshana Jr Kasie
Kupona kwake lazima ni serious injuries kugongwa na bus halafu likuminye ukutani si mchezo.
Haya mabasi mbele wameweka fibres kulinda watembea kwa miguu iwapo litamgonga. Ingekuwa yale ya kawaida asingepata hata muda wa kuwa icu
 
Anapaswa kupelekwa Stakishari akanywe chai kwa njia ya haja kubwa pale na mkuu wa upelelezi.
Amesababisha ajali ya kizembe kabisa!

Ona sasa mtu ametoka zake nyumbani, ameenda kukitafutia riziki mjini! Mwisho wa siku anajikuta yuko ICU, kwa uzembe wa mtu.

Hapo hujui hata familia yake inaishije! Usikute yeye ndiyo alikuwa ni kila kitu nyumbani! Siyo haki hata kidogo. Madereva wa vyombo vya moto tunatakiwa kuwa makini kuguata sheria za usalama barabarani.
 
Lazima SHERIA ya barabara ya mwendo kasi ibadilishwe haraka iwezekekanavyo hasa kwenye maeneo ya MJINI sababu hawa MADERVA WA MWENDO KASI huwa wanakwenda speed hasa kwenye maeneo ya MJINI wanashindwa kujua wameingia kwenye maeneo HATARISHI sasa ni wakati wa kuweka sheria katika maeneo ya MJINI SPEED 20 Iwekwe hadi wanapo ingia barabara KUU ndio waendelee na maspeed yao.

Isiwe sababu kuwa mwendo kasi ndio iwe mwendo kasi kila mahala ni Big NO ukitizama hizi ajali za makutano ya barabara za mwendo KASI hasa MJINI ni mwendo kazi tu.

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
 
Amesababisha ajali ya kizembe kabisa!

Ona sasa mtu ametoka zake nyumbani, ameenda kukitafutia riziki mjini! Mwisho wa siku anajikuta yuko ICU, kwa uzembe wa mtu.
Kabisa ile nguruwe inapaswa kukutana na chamtema kuni. Wamkamue mpaka tone la mwisho ajute kuzaliwa hapa duniani. Kamsababishia mwenzie taabu na mahangaiko mazito kwa upumbavu wake.
 
Kupona kwake lazima ni serious injuries kugongwa na bus halafu likuminye ukutani si mchezo.
Haya mabasi mbele wameweka fibres kulinda watembea kwa miguu iwapo litamgonga. Ingekuwa yale ya kawaida asingepata hata muda wa kuwa icu
Sawa mkuu. Hilo la fibres ndio nafahamu hapa leo. Nitafuatilia kujifunza zaidi.
 
Taasisi ya tiba ya mifupa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) imesema Mwanaume aliyeonekana akigongwa na Basi la abiria “mwendokasi” Jijini Dar es salaam jana, amelazwa Hospitalini hapo kwenye chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha MOI Patrick Mvungi ameiambia AyoTV kuwa Mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ kwa sababu mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi.

Mvungi ameongeza kuwa mpaka sasa Mtu huyo ambaye amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani hawezi kuongea lakini anafungua macho.

Pia soma: Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road
Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi apone haraka.
 
Mabasi ya mwendokasi yanakimbizwa sana ajali zake uwa zinakuwa mbaya sana wakati yanapita ktk lane zilizowazi na hiyo ndio maana yake sio kukimbiza mabasi ovyo na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuzuilika au kuleta madhara kidogo sana.
Umeliona la mwendokasi ila haujaliona la mwenye rav4.
 
Ifike muda raia wapewe taarifa kamili dhidi ya yale yanayowahusu na yanayoihusu nchi kwa ujumla.

Huyo bwana possibility ya kupona ni ndogo mno! Ingawa kwa mungu hakuna kubwa. Hebu waache utoto na waongee ukweli.

Kama sikosei mwenye gari ndogo (RAV 4) alikumbwa na kitete cha ghafla baada ya kuingia na kushtukia chombo imeshakaribia na imechochea kwenye njia yake.
 
Back
Top Bottom