MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU

MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU

Taasisi ya tiba ya mifupa kwenye Hospitali ya Muhimbili (MOI) imesema Mwanaume aliyeonekana akigongwa na Basi la abiria “mwendokasi” Jijini Dar es salaam jana, amelazwa Hospitalini hapo kwenye chumba cha ICU.

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha MOI Patrick Mvungi ameiambia AyoTV kuwa Mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ kwa sababu mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi.

Mvungi ameongeza kuwa mpaka sasa Mtu huyo ambaye amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani hawezi kuongea lakini anafungua macho

Sout. #MillardAyoUPDA
Mungu nimwema atapona aendelee na majukumu yake
 
Kuendesha gari city center sio kazi rahisi kihivyo,kuna watu wana leseni wamesomea veta ukimwambia twende town anaogopa
Ashukuru kupona. Maana kama dereva wa mwendokasi asingemkwepa na kwenda kumgonga mpita njia, basi alikuwa afie eneo la ajali.
 
Ana haki ya kulipwa na Bima. Tumuombee apone akadai fidia yake. Aliesababisha ajali(gari ndogo) ndio atalipa kupitia Bima yake kama anayo.
Mkuu mbona kwa nature ya hii ajali ni kama Mwendokasi ndio watamlipa maana yeye amegongwa na mwendokasi sio gari dogo

Au mimi ndio sijui
 
Maskini daah ,ujinga wa mtu mmoja umehatarisha maisha ya wengi. Dereva atafutwe apewe adhabu kali
 
Huyu miladi ayo sikuhizi kageuka habari maelezo,Jana alipost kuwa jamaa Yuko fresh,kumbe Hana update yoyote,dogo anazingua sikuhizi na mwili wake mdumavu 😅
 
Lile eneo kuna mataa pale ila baadhi ya madereva wa magari ya kawaida wanaletaga dharau sana pale.
Unakuta taa nyekundu imewaka ikimaanisha magari ya kawaida yasimame kupisha ya mwendokasi yapite, lakini ukiangalia kulia na kushoto hakuna gari la DART basi wao wanatumia nafasi hiyo kuvuka
Atakuwa alikuwa anabishana na mke wake
 
Kama sheria ingekuwapo kwenye BARABARA ya mwendo kasi inayo elekeza SPEED ya eneo husika lazima DEREVA wa DART angelifata sababu asingeweza kuupuza kama MADERVA wa usafiri mwingine na IMPACT YAKE isinge kuwa kubwa kama ilivyo kuwa kama BUS LA MWENDO KASI linge kuwa linakwenda 20MPH impact ingekuwa kidogo sana.

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
Kwa nilivoona basi lilikua na mwendo mdogo wa kawaida ila baada ya kugonga ile gari ndogo iliongeza mwendo Sana nadhan dereva wa mwendo Kasi alijichganya akachochea badala ya breks
 
Kwani wakisema ukweli kwamba amefariki kuna tatizo? Huo si ndiyo ukweli? Wewe kubamizwa vile ukutani na gari utatoka mzima?
 
Hii ndio taarifa rasmi hawana sababu ya kusema uongo

Wanabuy time tu ,hawezi kupona kwa ile impact.....wanatuliza tu kusiwe na kelele za raia mitandaoni ,wananchi wakishatulia ndiyo watatoa taarifa au umesahau kifo cha mchezaji aliyetokea Ghana Atsu?
 
Back
Top Bottom