Duh asee huyo jamaa jana tumebishana humu nikawa nasema atakuwa lazima alikufa.
Ila kama hakufa basi ni maajabu yenyewe. Kama hali yake inaendelea poa ni jambo la kushukuru Mungu.
RRONDO Mshana Jr Kasie
Nashukuru kwa taarifa,maombi ya wengi yamesikika bado anapumua hata kama hajitambui.
Ila ndo hawajamtambua hadi kumsema unknown....!!!!
Jamani, hakuwa hata na kitambulisho, simu pia ilipasuka pasuka.....
Kwenye ile picha aliyolazwa chini baada ya ajali anaonekana kwenye mfuko wake wa suruali kulikuwa na kitu kimetuna.....
Najaribu kuwaza kama amgekuwa na trace yoyote ili kupata hata majirani wa mahali alipokuwa anaishi.....😔😔😔
Hivi hapa Dar, hakuna mtu ambaye aidha ndugu au jirani hamjamuona kwa siku mbili tatu hizi? Mwenye rangi na kimo kile?
Au hata yawezekana alitoka mkoani....
Pengine hakuaga.....😔😔😔
All in all, natumai anapata huduma sahihi chini ya uangalizi wa serikali maana hakuna wanaomfahamu waliojitokeza.
Hata waumini wenzie wa dini kama alikuwa muumini..... hata kama alikiwa machinga, machinga wenzake wangejitokeza iwapo wangefahamu ni yeye....
Until then, hali na nia ya kusaidia walio nyuma yake bado ipo, japo kibaba cha unga wa siku moja, kutoa ni moyo hasa kwa wahitaji....
Kuna wazo linanijia labda hana wanaomtegemea.... alikuwa anaishi solo....🤷♀️🤷♀️🤷♀️🤷♀️
Kikubwa nia inatoka moyoni, God knows more 🙏🙏🙏
Namuombea afueni njema na ya haraka.