Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Kuna sehemu kwenye injili, Yesu anamtoa mapepo jamaa flani hivi, kisha Yesu akayaamuru yale mapepo yawaingie nguruwe waliokuwepo around!

Kwa nilivyoelewa, ni kwamba wale nguruwe walikuwa mali ya raia fulani maeneo hayo.

Sasa, swali langu ni hili, Kwamba kumbe nguruwe walikuwa wanafugwa hata kwenye kipindi kile cha Yesu, tena maeneo yale yale?

Je, walikuwa wanafugwa kwa sababu gani, kama si kwa ajili ya kitoweo?
 
ngoja nikukumbushe kitu..wana wa israel walipokuwa safarin kurud nchi ya ahadi walilishwa mana mpya kila siku,,,,ilikuwa inadondoka kutoka mbinguni mikate ile/mana..... ilikuwa huwezi kutunza mana ya jana ule leo... sasa ni hvyo mpaka sasa mungu aliekataza ndie alieruhusu na sababu amekupa sasa nyny mnang'ang'ania mana ya jana na wakati imeshashuka mpya hio haitakusaidia...... hayo ni mafundisho mapya ya shetan kwakuwa mungu hahubiri hvy tn, tembea na wingu lake anapotembea usikae kwenye jua la jana halitakusidia,,, ujiulizi baada ya kristo na injili kuja kwenye mataifa hakuna mkristo alieshika sabato wala ivyo vyakula kwenye biblia?????
 
Atuachie my wetu.
 
Warumi 14:1-3
[1]Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.

[2]Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.

[3]Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.
 
Msabato wewe eti fungu la 9!
 
Mungu amekataza zinaa pia lakini mnaongoza kuzini ninyi

Hapa nimenunua kilo zangu 4 nikitoka kanisani leo natengeneza roast swaaafi na ugali tunakula familia tena ndani ya familia tuna mhudumu wetu muislamu anakipenda kwelikweli KTM
 
Mungu amekataza zinaa pia lakini mnaongoza kuzini ninyi

Hapa nimenunua kilo zangu 4 nikitoka kanisani leo natengeneza roast swaaafi na ugali tunakula familia tena ndani ya familia tuna mhudumu wetu muislamu anakipenda kwelikweli KTM
Kama kuna mtu anazini anatenda dhambi, Je unayaangalia matendo ya watu kama kundi au kama mtu mmoja mmoja?

Mbinguni hatutaingia kwa matendo ya madhehebi yetu au kwa matendo ya dini zetu bali kwa moyo ulio safi wa kila mcha Mungu.
 
Mungu atakuhukumu kwa kutofata amri zake ayo mengine mnajidanganya tu
 
Hata leo hii Mungu ashuke hapa na afanye miujiza yote na watu waamini yeye kweli Ndiye, bado dhambi itaendelea tu, sisi wanadamu ni viumbe vya ajabu.
 
ujiulizi baada ya kristo na injili kuja kwenye mataifa hakuna mkristo alieshika sabato wala ivyo vyakula kwenye biblia?????
Hili una uhakika nalo? Unajua ibada ya jumapili imekuja siku gani?
 
katika amri zote 10 haipo ya kutokula nguruwe.

maana yake nini??
hii haikuwa dhambi ya kumchukiza Mungu,bali dhambi ya kimila ya watu wa israel.

ni kama amri za kanisa la roma za leo.
 
[3]Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.
Hili fungu ukilibeba kichwa kichwa hakuna dhambi utakemea sababu utaonekana unahukumu watu, na kuhukumu si kwa binadamu bali ni kwa Mungu, Tumejua kuwa kuna dhambi kwa sababu kuna sheria.
 
katika amri zote 10 haipo ya kutokula nguruwe.

maana yake nini??
hii haikuwa dhambi ya kumchukiza Mungu,bali dhambi ya kimila ya watu wa israel.

ni kama amri za kanisa la roma za leo.
Petro alimkatalia Mungu mara tatu kwamba hawezi kula Najisi, na huyu alikuwa mfuasi wa Yesu, Je mafundisho hayo aliyatoa wapi? Na kwanini alikataa ikiwa Mungu ameruhusu tule kila kilicho mbele yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…