Moja ya makosa utafanya ni kuolewa na Mwanaume wa miaka 50+. Walioingia huko wengi wanalia

Moja ya makosa utafanya ni kuolewa na Mwanaume wa miaka 50+. Walioingia huko wengi wanalia

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
1781604770703.png

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Chunguzi zangu za kina zinanionyesha haya. Nitazungumza ukweli mwingi ili kuwaponya ambao wanataka kujaribu kujiingiza huko.

2. Wadada wengi baada ya kuumizwa na mapenzi kutoka kwa vijana wenzao. Hufikiri kwamba suluhisho ni kuolewa na wababa watu wazima wale 50+ huko.

3. Ukweli ni kuwa Hakuna suluhu ya namna hiyo. Mtibeli nikuambie wazi hakuna watu wanaoteswa na mapenzi kama walioolewa na Wababa watu wazima.

4. Katika simu za wanawake kumi nitakazopokea zinazohusu mambo ya ndoa, simu sita ni wanawake walioolewa au wanaoishi kindoa na wanaume watu wazima. Na malalamiko yao yanafanana kwa asilimia 90%.

5. Nilipojaribu kuuliza kwa nini waliolewa na Wanaume watu wazima majibu yao yalikuwa hivi;
a) Watu wazima wanajua kupenda na wanajali.

b) Watu wazima walishavuka ujana hivyo hawana matukio.
c) Watu wazima wanajua thamani ya mwanamke na familia.
d) Watu wazima wanajua kutunza nakuhudumia kwani wengi wao wamejipata.

Hayo ni mawazo yao makuu karibu wote walizungumza mambo yanayoelekeana na hayo.

6. Na mitazamo hiyo ni Kabla ya wao kuishi au kuolewa na Wanaume hao watu wazima.

7. Baada ya kuolewa, mitazamo yao ilibadilika na walikuwa very dissapointed

8. Matokeo na malalamiko yao yako hivi;
a) Watu wazima wanapenda tuu mwanzoni lakini baada ya miezi kadhaa wanabadilika ni bora hata vijana.

b) Watu wazima ni wabinafsi na wanyanyasaji. Maneno kama ya kukusaidia, nilikutoa huna mbele wala nyuma, huna pakwenda ni kawaida.

c) Watu wazima wengi huwazuia Wake zao hawa wadogo kutokufanya kazi kwa kuonyesha wanawivu. Lakini Mtibeli najua hiyo ni njia ya kuwadhibiti na kuwatawala hao mabinti kirahisi.

d) Changamoto za Mke aliyetangulia na Watoto aliowakuta.
Bado mke na watoto aliowakuta ananguvu kubwa kwenye maisha ya Mwanaume mtu mzima.
Hii inafanya binti aliyeolewa na mtu mzima kuwa hana mamlaka wala nguvu yoyote.

e) Watu wazima bado hawajaacha tabia za kutembea na wanawake na wengi Bar na kazi ndio muhimu kuliko mke mpya.

f) Hakuna Kampani wala attension kutoka kwa Baba mtu mzima. Hii inawafanya wadada waishi kwa stresa. Zingatia mwanamke anathamini attention kuliko kula.

g) Mitazamo potofu kutoka kwa Mwanaume na jamii kuwa mwanamke kafuata pesa.
Wadada karibu wote waliniambia moja ya kero zinazowafanya wajute ni kasumba hiyo kwamba mpaka mwanaume anahisi kwamba alimfuata kwa sababu ya pesa.
Ndugu wa mume na majirani wanamtazamo huu jambo ambalo mwanamke hata kama anamapenzi ya kweli anaonekana kaja kuchuma mali.

9. Kwa kifupi, wadada wengi hujikuta katika hali ya stress na majuto baada ya matarajio yao kwenda kombo.

10. Kama Mtibeli, mara nyingi nashauri. Mabinti hakikisha, fanya ufanyavyo uwe na uwezo wa kujihudumia wewe mwenyewe. Kazi ndio Dini yako.
Maana msingi wa matatizo mengi wanayolalamikia wanawake upo kwenye utegemezi.

11. Mwanamke ukishakuwa unauwezo wa kujihudumia mapenzi hayawezi kukusumbua. Utasumbuliwa na mwanaume mmoja tuu. Yule uliyempenda kwa moyo wako wote. Wanaofuata ni kitonga.

12. Moja ya dalili huna kazi za kufanya ni kuteswa na kila anayekuja kuwa mpenzi wako. Ni kiashiria huna kazi za kufanya.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Wameanza lini? Mbona wako poa tu!

Olewa kwanza alafu utajionea.

Iki hivi,
Kuna wakati unapoaminisha watu jambo fulani ni zuri. Ukaamua kulifanya alafu ukakuta sio zuri unaamua kunyamaza ili kuepuka kuabika.

Ni sawa na mtu aliyeisifia Ulaya, alafu anafika ulaya anakuta ngoma ngumu bora Bongo. Alafu anashindwa kusema ukweli anaamua kufa kikondoo
 
Olewa kwanza alafu utajionea.

Iki hivi,
Kuna wakati unapoaminisha watu jambo fulani ni zuri. Ukaamua kulifanya alafu ukakuta sio zuri unaamua kunyamaza ili kuepuka kuabika.

Ni sawa na mtu aliyeisifia Ulaya, alafu anafika ulaya anakuta ngoma ngumu bora Bongo. Alafu anashindwa kusema ukweli anaamua kufa kikondoo
Hmm ngoja niongee na mubaba wangu tuone kama tutaweza kuwekana ndani, nitaleta mrejesho!
 
Kwani vijana hawana changamoto?

Wanazo ila zinakuwa ndani ya uwezo wa binti
Sasa binti mwenye miaka 25 aolewena kijana wa miaka 35. Hawezi kushindwa kuhimili changamoto za kijana huyo

Lakini binti miaka 25 aolewe na mwanaume wa miaka 50 changamoto zake ni kubwa zaidi.

Ni kama hizo kesi za Single mother na kijana.
Sio kwamba mwanamke asiye single mother hana changamoto.
Tatizo ni ukubwa wa hizo changamoto
 
Back
Top Bottom