Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
Unajua mnachonifurahisha humu ni kwamba mnayoandika ni tofauti kabisa na mnayoyatenda, yani huku kwenye maisha halisi kila siku wanaume wanalalamikia tabia mbovu za wanawake, ila bado wengine wanaendelea kuoa halafu humu eti mnajitutumua hatuoi wa hivi tunaoa wa vileHao wanaokubaliana na wewe wana trauma tu za mahusiano yao yaliyopita bado wanaishi na vinyongo vya kuachika au kupigwa matukio na maex wao. Na wale wanawake wenye ujeuri wa asili tu wanakubaliana na wewe ku-justify ujeuri wao. Narudia tena hakuna mwanamke mwenye maadili na ndoa imara na dhamira ya kuilinda anaweza ku-apply unayoyaubiri wewe. Mawazo yako ni typically na yale ya joyce kiria kwenye kipindi chake cha wanawake live na wote tunajua historia yake kimahusiano ipoje, hakuna mwanaume timamu anaweza kuvulimia huo ujinga.
Hii ndio hoja yenyewe sasa au wewe unataka hoja mpaka iwe ligi
Kusema kwamba tukubaliane na hali siyo hoja, kwa sababu wanawake nao ni binadamu wenye utashi kama wanaume kwahiyo lazima wahoji, kwanini iwe hivi na isiwe vile na ni haki yao kupata majibu yasiyo na utata na yanayoridhisha
Yani kwa mfano watu weupe walivyowaaminisha vizazi na vizazi kuwa wao ndio wanameumbwa kuwatawala watu weusi, kwa sababu wao ndio wana akili na maarifa kuliko watu weusi kwahiyo unataka watu weusi wakubali tu, wasihoji kwa sababu tu ni kitu ambacho kipo toka enzi na enzi siyo