Monalisa ahitimu Chuo Kikuu licha ya kupitia dhihaka na kejeli kisa umri

Monalisa ahitimu Chuo Kikuu licha ya kupitia dhihaka na kejeli kisa umri

Yvonne Cherrie, msanii maarufu wa filamu, Monalisa, ameweka historia baada ya kuhitimu Chuo Kikuu katika fani ya Usimamizi wa Biashara na Miradi, licha ya changamoto za dhihaka na kejeli alizokumbana nazo kutokana na umri wake.
View attachment 3171295
Monalisa, ambaye alikuwa miongoni mwa mwanafunzi waliokula chumvi nyingi katika darasa lake, amesema watu walimcheka na kushangaa kwanini aliamua kurudi shule akiwa na umri mkubwa. Hata hivyo, hakukata tamaa na leo amejivunia kuhitimu akiwa mwanafunzi bora wa darasa lake.
View attachment 3171296
Katika ujumbe wake, Monalisa amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni ushuhuda wa uvumilivu, ujasiri, na uthubutu. Amesema safari yake ni kielelezo kuwa kamwe si kuchelewa kufanikisha ndoto zako, na huu ni mwanzo tu wa mambo makubwa yanayokuja.
View attachment 3171297
“Nilichekwa, lakini leo nimebutua,” alisema Monalisa kwa furaha, akiongeza kuwa hakuna kurudi nyuma, na mashabiki wake waendelee kufuatilia safari yake.
View attachment 3171293
Mastaa na mtoto wake wamiminika kumpongeza mitandaoni.
View attachment 3171294

Acha wee, kumbe bado ana mvuto. Hongera zake. Elimu ni bahari
 
Back
Top Bottom