Monalisa ahitimu Chuo Kikuu licha ya kupitia dhihaka na kejeli kisa umri

Monalisa ahitimu Chuo Kikuu licha ya kupitia dhihaka na kejeli kisa umri

Yvonne Cherrie, msanii maarufu wa filamu, Monalisa, ameweka historia baada ya kuhitimu Chuo Kikuu katika fani ya Usimamizi wa Biashara na Miradi, licha ya changamoto za dhihaka na kejeli alizokumbana nazo kutokana na umri wake.
View attachment 3171295
Monalisa, ambaye alikuwa miongoni mwa mwanafunzi waliokula chumvi nyingi katika darasa lake, amesema watu walimcheka na kushangaa kwanini aliamua kurudi shule akiwa na umri mkubwa. Hata hivyo, hakukata tamaa na leo amejivunia kuhitimu akiwa mwanafunzi bora wa darasa lake.
View attachment 3171296
Katika ujumbe wake, Monalisa amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni ushuhuda wa uvumilivu, ujasiri, na uthubutu. Amesema safari yake ni kielelezo kuwa kamwe si kuchelewa kufanikisha ndoto zako, na huu ni mwanzo tu wa mambo makubwa yanayokuja.
View attachment 3171297
“Nilichekwa, lakini leo nimebutua,” alisema Monalisa kwa furaha, akiongeza kuwa hakuna kurudi nyuma, na mashabiki wake waendelee kufuatilia safari yake.
View attachment 3171293
Mastaa na mtoto wake wamiminika kumpongeza mitandaoni.
View attachment 3171294
Jina la chuo?
All the best
Naomba kukazia hapa! Tungejulishwa jina la chuo, na pia kiwango cha elimu alichosoma (mfano Astashahada, Stashahada, Shahada, nk.)
 
Yvonne Cherrie, msanii maarufu wa filamu, Monalisa, ameweka historia baada ya kuhitimu Chuo Kikuu katika fani ya Usimamizi wa Biashara na Miradi, licha ya changamoto za dhihaka na kejeli alizokumbana nazo kutokana na umri wake.
View attachment 3171295
Monalisa, ambaye alikuwa miongoni mwa mwanafunzi waliokula chumvi nyingi katika darasa lake, amesema watu walimcheka na kushangaa kwanini aliamua kurudi shule akiwa na umri mkubwa. Hata hivyo, hakukata tamaa na leo amejivunia kuhitimu akiwa mwanafunzi bora wa darasa lake.
View attachment 3171296
Katika ujumbe wake, Monalisa amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni ushuhuda wa uvumilivu, ujasiri, na uthubutu. Amesema safari yake ni kielelezo kuwa kamwe si kuchelewa kufanikisha ndoto zako, na huu ni mwanzo tu wa mambo makubwa yanayokuja.
View attachment 3171297
“Nilichekwa, lakini leo nimebutua,” alisema Monalisa kwa furaha, akiongeza kuwa hakuna kurudi nyuma, na mashabiki wake waendelee kufuatilia safari yake.
View attachment 3171293
Mastaa na mtoto wake wamiminika kumpongeza mitandaoni.
View attachment 3171294
Hongera nyingi kwake 🌹🌹🌺🌺
 
Yeye bado kijana sana. Kuna waziri mkuu alienda kusoma degree baada ya kustaafu. Aende zaidi👍
 
Hongera sana ,wahenga wanasema elimu haina mwisho....Piga masters and Phd usisikilize maneno ya loosers...Trump anaitafuta 80 na bado anapambana.
 
Kuwa na elimu ni vizuri Ila Kwa age yake 50+ na mazingira ya TZ sifikirii kuna kitu ametoa kama funzo.

Kaanza kuigiza kitambo ,kapata madili kibao , kukosa kuwekeza na kuwa na mipango mizuri ya kiuchumi anabaki kuamini katika karatasi na kuajiriwa.

All in all hongera sana kwake.
 
Wengi mnahangaika kasoma chuo gani.jina la chuo so lipo hapo kwenye joho la juu
 
Attachments

  • Screenshot_20241210-075512.jpg
    Screenshot_20241210-075512.jpg
    126 KB · Views: 5
Huyo Alipo alishaambiwa katafute tu cheti uje ule Uwanja uko wazi... Damu ya kijani Huyo na damu anazunguka nazo hasa wee
Wewe mwenzangu nn a Mimi? [emoji41]Vp Bado yule mfupi anayeng'ang'ania jina la watu..,,
 
Back
Top Bottom