Poor Brain
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 28,865
- 58,677
Habari wakuu
Natumai wote humu ndani ni wazima wa afya kabisa.
Week mbili hizi nimefanya research ambayo naimani kama ikifanyiwa kazi basi tunaweza pata matokeo chanya kwa taifa letu na hata tutajikomboa katika wombi la ukosefu wa ajira kwa vijana na umaskini kwa ujumla.
Nitangulize pia shukurani kwa mwenyezimungu kwa kunipa uhai na uzima kwa hizi siku zote za research yangu.
Pia nashukuru sana kwa wana jf wenzangu mlionipa ushirikiano kama ndgu yangu Vishu Mtata , kwani umekua pamoja na mimi katika kuandaa research hii.. Bila kusahau kaka angu Vincenzo Jr kwa upande wa management Bila kusahau ndugu yangu Mbaga Jr kwa kunikutanisha na baadhi ya viongozi wa umoja wa wana research hapa tanzania
Sasa naomba niwasilishe kama ifuatavyo.
Mwaka 2015 mpaka 2021 limefumuka wimbi kubwa sana la vijana kukosa ajira.
Kitendo hiki kimefanya vijana kujiingiza katika mambo ya ajabu ajabu moja wapo ni kubeti, Punyeto na mambo mengine ambayo yamekua yakiwapelekesha vijana wenzetu mputa mputa.
Leo hii unakuta watu wanajazana katika nyuzi za kubeti wakisubiri odds kutoa kwa JITU BANDIA ambaye hata yeye mwenyewe kuna mda kanji anamfurahisha maana kanji hacheki na mtu
Haya yote yanatokana na mfumo ambao serikali yetu imeweka, mfumo ambao upo Very unstable kwa vijana na hata wazee wa sasa.
Huu ni mfumo ambao tunaweza kuuita MONEY DOPPER EFFECTOR (MDE) . Mfumo huu ambao umekua chanzo cha yote haya.
Mfumo 1 .
Naomba niende kwa mfano kidogo tuingie kwenye solution yetu
Ili upate huduma X ni lazima utoe Y huu mfumo wa kwanza (MDE)
Means ili upate BIDHAA(X) ni lazima utoe PESA(Y)
Mfumo 2 .
Ili upate huduma X ni lazima upewe Y Then huduma itafata
hapo najua nishakuacha sasa twende mdogo mdogo
Jiulize kwanini ukienda dukani ili upate huduma lazima ulipe ?
Kwanini ukienda hospital ili utibie unalipa ?
Hii yote ni mifumo wakuu ambayo inazumuni la kumdidimiza kijana ambaye leo au kesho anakuja kuwa baba wa kizazi kijacho.
Na yote haya ni serikali imeleta huu mfumo, ambao mwisho wa siku watu watakuja kujutia
Sasa katika kutafakari sana na kufanya research nimekuja na mfumo ambao unaitwa MONEY SUNCTION EFFECTOR (MSE)
Huu mfumo ambao ili upate huduma X ni lazima kwanza upewe Y na sio wewe utoe Y
Let say
Hivi leo hii bakharesa ili apate raw material ya kuzalisha unga. Basi serikali Inapaswa kumpa mahindi na pesa kama trillion 900,
Naaam atapewa hivo ili azalishe unga.
Baada ya yote hayo mtu anayekuja kununua unga itabidi apewe unga kulingana na kiasi anachotaka
Mfano
Akitaka viroba 200 basi atapigiwa hesabu kama kiroba kimoja ni 5000 basi atapewa Million moja 1000,000 na viroba vya unga ili yeye apeleke dukani kwake.
Huku dukani tena mteja anapokuja yeye anataka unga kilo moja Ambayo ni 700.
Basi atapewa kilo moja ya unga na 700 yake.
Hali hii itaenda hivo hivo mpaka kwa walimu ambao ili wafundishe wanafunzi itabidi kila mzazi alipwe pesa na serikali ili mtoto asome.
- Hali hii itaenda hvo hvo mpaka kwa walimu ambao ili wafundishe wanafunzi itabidi kila mzazi alipwe pesa na serikali ili mtoto asome.
- Walimu hawa ni lazima wailipe serikali ili wafanye kazi yao ya kufundisha.
- Mfanya kazi wa serikalini mwisho wa mwezi inabidi alipe kiasi cha pesa kulingana na kazi yake
Lakini hapo hapo hospitali inakua inalipwa na serikali kwa ajili ya kulipa wagonjwa wanaofika hospitalini.> Dactar kila mwisho wa mwezi itabidi awe analipa 800,000 kwa kazi anayofanya.
Konda huyo huyo anapoenda kuweka mafuta anafika sheri wanamlipa pesa ya mafuta aliyoweka.> Leo hii ukipanda gari kutoka chanika mpaka complex unalipa 1000 Huu mfumo unafanya konda awe analipa kila raia buku buku.
Inabidi mda unajiunga ukimaliza tu na muhamala unasoma umepata 2000.> Ili uingie mtandaoni ni lazima upewe MB na pesa ya zile MB ulizonunua mfano lep hii umeingia hapa umelipa bando la 2000 GB 1
"" siwezi kupanda ndege wanalipa pesa kubwa sana"">Lakini pia tukija kwenye usafiri watu watakua wapo katika wakati ambao tunalalamika kuwa
Mda huo wafanyakazi wa airport wanatangaza kuwa kufika mwanza kutokea dar utalipwa laki mbili, mda huo watu wanaona kulipwa laki mbili nipesa nyingi at least walipwe laki na nusu..
Huu ni mfumo ambao utafanya maisha yawe slightly sana kwani hakuna mtu ambaye angelalamika maisha magumu
Maana unaenda kwa mama ntilie, kabla ya kula unaukizwa unataka ulipwe shingapi upewe chakula..
Kariakoo kungechangamka. Winga anakupa lakimbi anakuletea simu safi kabisa..
Mambo ni mengi sana wakuu
Lakini pia nimeambatanisha Company Protofolio na nakala zote za copyright hapo
kwa yoyote ambaye atakua tayari kuinua wazo langu kwenda juu karibuni sana asanteni