Morogoro: Atuhumiwa kula njama kumuua mumewe ili ale raha na bodaboda

Morogoro: Atuhumiwa kula njama kumuua mumewe ili ale raha na bodaboda

Alikuwa NICE GUY kwake yeye ni mkewe tu.

Mwanamke akishachange kachange, huwa hasikii, haoni, haambiliki na hana hata chembe ya huruma. Ikishafikia hatua hiyo usalama wako ni kuachana nae tu ila ukisema unakomaa nae umbadilishe jua fika umekwisha.
To all loyal guys out there kung’ang’ania kitu kisicho kutaka mwishowe itakueletea shida either kiafya au utaish maisha ya mateso for so long
na pia usiwe nice guy sana, as the gambler said “know when to walk, when to run”
 
Utamrudia 😄

Ova
Kaka haiwezekani, licha ya kuwa malaya ni wale watu wa matumizi makubwa, watunzaji sana shereheni na akiwa na wenzake atajigamba nimempata boya, hakujua mhuni taarifa zake zote napata moja kwa moja
Nilimtema kistaarabu hivyo ili hata angeenda popote asingeweza niharibia vidili vyangu kipindi kile
 
Kaka haiwezekani, licha ya kuwa malaya ni wale watu wa matumizi makubwa, watunzaji sana shereheni na akiwa na wenzake atajigamba nimempata boya, hakujua mhuni taarifa zake zote napata moja kwa moja
Nilimtema kistaarabu hivyo ili hata angeenda popote asingeweza niharibia vidili vyangu kipindi kile
Ulitumia akili na utulivu sana

Ukitumia hivyo vitu viwili lazima

Ushinde vita

Ova
 
Mimi niliacha nimemlipia pango la mwaka mzima gf yule, baada ya miezi miwili anauliza mbona hurud nikamwambia tumeshaachana, kodi ya miez 10 inatosha wewe kujipanga na samani zote za ndani ni zako, nikampa na kifuta jasho cha tubiashara, leo mwaka wa sita alishachoka omba msamaha
Hii njia uliyotumia itamuumiza zaidi ya ile ya kumfukuza kwa mateke na matusi.
 
Mimi niliacha nimemlipia pango la mwaka mzima gf yule, baada ya miezi miwili anauliza mbona hurud nikamwambia tumeshaachana, kodi ya miez 10 inatosha wewe kujipanga na samani zote za ndani ni zako, nikampa na kifuta jasho cha tubiashara, leo mwaka wa sita alishachoka omba msamaha
Yani umefanya vizuri Sana yani mwanamke akichepuka ni dharau kubwa Sana" alafu akiwa anapigwa miti na mchepuko wake hua wanasema. Yule baba fulani yani hana lolote nyumbani walinifosi tu kuolewa nae mimi nakupenda wewe Tu😄😄
 
To all loyal guys out there kung’ang’ania kitu kisicho kutaka mwishowe itakueletea shida either kiafya au utaish maisha ya mateso for so long
na pia usiwe nice guy sana, as the gambler said “know when to walk, when to run”
well said mkuu, wasipoelewa basi.
 
Yani umefanya vizuri Sana yani mwanamke akichepuka ni dharau kubwa Sana" alafu akiwa anapigwa miti na mchepuko wake hua wanasema. Yule baba fulani yani hana lolote nyumbani walinifosi tu kuolewa nae mimi nakupenda wewe Tu😄😄
Kama ulikuwepo. Yaani wanawake wa aina hii wakiwa na mchepuko wake wanatoa kashfa sana kwa waume zao.
 
Ungekua umeoa wala usingeongea hii kauli
Ukijazwa unajazwa haijalishi nimeoa au sijaoa, HIO sababu ndio iliyomfanya bro wangu azae na wanawake 7 tofauti mikoa tofauti tofauti akikanyaga Singida anaacha mtoto, Tabora anaacha mtoto, Mwanza anaacha mtoto, Mbeya anaacha mtoto, Sumbawanga anaacha mtoto, Morogoro anaacha mtoto, Ntwara anaacha mtoto, Ruvuma anaacha mtoto, yaan hivyo kila Mkoa akikanyaga anaacha na mtoto huko huko sasa idadi ya watoto imekua nyingi mpaka haelewi itakuaje na mke wake kazaa nae watoto 6 kamili, usiniulize maswali mengine ya kipumbavu najua ninachokiandika
 
Hapo utakuwa huna familia na utadharauka sana. NB: kuna jamaa namjua anafanya hivi hivi unavyosema.
Mfano Hai ninao Mimi kwa HIO najua ninachokiandika Dawa ya Mwanamke anaekitembeza kigozi ni kwenda nae Sawa tu akiwe Mguu unaweka Jiwe hapo mtaenda Sawa yaan hamtogombana wala vurugu zingine sababu yeye mwenyewe anajua na anaelewa hakutendei haki kwa HIO hata akisikia una watoto huko nje hawezi kushangaa sababu anajua watoto wengine aliokuzalia sio wa kwako wewe ni Baba mlezi tu Baba halisi yupo huko nje
 
Ingekua na Polisi wanachukulia mambo kirahisi kama ulivyochukulia wewe,Basi kusingekua hata na uchunguzi,
Mtu anaweza kuonekana kua ameua na kila mtu kaona kua ameua ila lazima kuwe na uchunguzi coz hua kuna mambo mengi behind na pia kuna wahusika wengine japo itakua ndio walichora ramani ya mauaji hayo.
Kwani hayo maelezo ya mwanamke kuhusika na kifo cha mumewe ni yakwangu? Hayo ni maelezo ya polisi
 
ila nisijue, nikijua nitachukua maamuzi magumu
Kuchapiwa ni Siri ya Ndani Wahuni wana msemo wao unaonekana wa kijinga Ila inamaana sana unaambiwa "ukiona Kausha" yaan ukiona mkeo anagongwa Kausha acha kelele mingi usije ikawa unajichimbia Kaburi mwenyewe na mikono yako
 
Halafu watu huwa wanajidanganya jamaniii hata uwe na jidudee kubwaaa kama la punda kama umeoa Mwanamke ambaye si muaminifu ni kazi bure 😁😁
Tatizo sisi wanaume tunajiona tunawafahamu sana wanawake! Upo sahihi na kwa vile wewe ni mama! Halafu dunia hii ya ajabu. Ukiwa na jidude mkeo atatamani kibamia. Ukiwa na kibamia mkeo atatamani jidude!
 
Huyo ni mwalimu hapa Mang’ula kauawa kikatili na mkewe kapigwa na kitu kizito kichwani ubongo ukamwagika. Ni ukatili mkubwa na lengo lake awe huru kujivinjari na kijana wa nje ambaye ni Bodaboda. Na amezaa na huyo Boda mtoto mmoja wa mwisho katika watatu. Jana mwili umesafirishwa kwenda Ukerewe kwa mazishi. Mwanamke yupo police Morogoro kala kipigo kaeleza upuuzi wake wote na alioshiriki nao katika uhalifu huu!


===
Wakati Jeshi la Polisi mkoani Morogoro likiendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Signal, Christian Tungaraza, mdogo wa marehemu, Clavery Tungaraza amesema mara ya mwisho kaka yake alimtumia picha yake na kumwelekeza kwamba itumike kwenye mazishi yake atakapokuwa amekufa.

Clavery amebainisha kwamba hadi sasa hafahamu mauaji hayo yametokana na nini kwa kuwa marehemu kaka yake hakuwahi kumueleza kama alikuwa na mgogoro au ugomvi na mtu yeyote.

Wakati uchunguzi huo ukiendelea, mke wa mwalimu wake Jovina Mwakiyee (33), mkazi wa Kijiji cha Mang'ula A, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kula njama na kumuua mume wake.

Akizungumzia na Mwananchi Digital, mdogo wa marehemu amesema alipata taarifa za mauaji ya kaka yake Juni Mosi, 2024 usiku kutoka kwa shemeji yake (Jovina) ambapo alielezwa kuwa walivamiwa usiku huo na watu wasiojulikana na kuanza kumshambulia kaka yake.

“Baada ya kupata taarifa hizo nikiwa nyumbani Simiyu, nilianza kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa karibu na kaka huku Morogoro na ilipofika asubuhi tukapata taarifa kuwa kaka amefariki akiwa hospitali Ifakara, basi nikiwa na ndugu wengine tulikwenda Morogoro na kuchukua mwili wa mpendwa wetu,” amesema Clavery.

Ameongeza kuwa baada ya kufika Morogoro kwa ajili ya kuchukua mwili wa kaka yake, hakuweza kupata nguvu na muda wa kuuliza chanzo cha mauaji hayo na wala kujua nani amehusika, bali waliweza kuwasiliana na polisi na kukabidhiwa mwili na kuusafirisha hadi Simiyu kwa ajili mazishi.

“Hata hivyo, baada ya kufika Ifakara tulipata taarifa kutoka polisi kuwa yule shemeji amekamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kaka na kula njama, sisi kama familia hatuwezi kuthibitisha kama kweli shemeji amefanya hivyo ama la, wenye uwezo wa kuthibitisha hilo ni polisi baada ya kukamilisha uchunguzi,” amesema Clavery.

Kuhusu maisha aliyokuwa akiishi kaka yake na mke wake, Clavery amesema hana uhakika kama yalikuwa ni maisha mazuri na furaha ama ya migogoro kwa kuwa katika kipindi chote walichoishi, hakuwahi kusikia kesi wala malalamiko kutoka kwa wanandoa hao.

“Enzi za uhai wake, kaka yangu alikuwa ni mtu mcheshi, hakuwa mgomvi, yawezekana alikuwa akipita kwenye migogoro ya ndoa lakini mimi kama mdogo wake na hata ndugu wengine hawajawahi kusikia alilalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili na mke wake, hivyo kama alikuwa akipita kwenye magumu basi alichagua kuvumilia,” amesema Clavery.

Akieleza kauli ya mwisho aliyoongea na kaka yake, Clavery amesema wamekuwa na mazungumzo ya kawaida lakini mara ya mwisho alimtumia picha na kumuandikia ujumbe kuwa picha hiyo itumike kwenye jeneza endapo atafariki siku yoyote.

“Nakumbuka kuna picha moja alinitumia na kuniambia kama atakufa basi ndiyo itumike kwenye jeneza, sikujua alikuwa anamaanisha nini, mimi niliitunza ile picha na siku ya msiba tuliamua kuitumia ile picha kama alivyousia na hiki ndio kitu kinachoniuma zaidi,” amesema Clavery.

Amesema kaka yake ni mtoto wa tatu kati ya watoto sita waliozaliwa kwenye familia ya mzee Tungaraza ambapo naye ameacha watoto watatu aliozaa na mke wake huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Amesema tayari watoto wawili kati ya hao watatu wamechukuliwa na ndugu zao na mmoja mdogo mwenye umri chini ya miaka miwili alichukuliwa na akiwa na mama yake polisi walipokuja kukamata.

Mmoja wa walimu ambao ni marafiki wa karibu wa marehemu Tungaraza ambaye hakutaka kutaja jina lake, amesema taarifa alizopata ni kwamba wanandoa hao walikuwa kwenye mgogoro ambao unaelezwa kuwa ulitokea baada ya mke kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake.

“Mwalimu Tungaraza enzi za uhai wake alisumbuana na mke wake hasa kwa kile kinachodaiwa kuwa mke wake hakuwa mwaminifu na zipo taarifa kuwa alikuwa na uhusiano na kijana mmoja ambaye tunasikia tayari ameshakamatwa,” amesema mwalimu huyo.

Jirani wa marehemu Tungaraza ambaye pia ni katibu wa Kitongoji cha Gendeni, Kijiji cha Mang'ula A, Fahamia Abdallah amesema Aprili 2024, Tungaraza alifika kwenye Serikali ya kitongoji hicho na kueleza mgogoro uliopo baina yake na mke wake, huku akitaja sababu kubwa ya mgogoro huo kuwa ni mke wake kutokuwa mwaminifu katika ndoa na kumtaja kijana mmoja kuwa alikuwa na mahusiano na mke wake.

Katibu huyo wa kitongoji amesema kuwa baada ya kupokea madai hayo mke wa Tungaraza aliitwa katika ofisi hizo na viongozi akiwemo yeye katibu na baada ya kuelezwa kile anachotuhumiwa mwanamke huyo alimuomba radhi mume wake (Tungaraza) na kumuahidi kujirekebisha hasa kitabia na hivyo wanandoa hao waliondoka na kwenda kuendelea na maisha kama kawaida.

“Wiki mbili kabla ya Mwalimu Tungaraza hajauawa, alinipigia na kunipa taarifa kuwa kijana aliyekuwa akimtuhumu kujihusisha kimapemzi na mke wake aliendelea kufika nyumbani kwake. Hivyo aliniomba nizungumze na mke wake na nimuonye kwa kuwa jambo hilo halipendi, sikuwahi kumuita huyu mwanamke kwa kuwa na mimi nilianguka na kuvunjika mguu. Nilitamani kabla ya kumuita nifanye uchunguzi wangu ili nijiridhishe lakini ndo hivyo kama sijakamilisha uchunguzi ndipo tukio hilo likatokea," amesema Fahamia.

Akizungumzia marehemu Tungaraza, katibu huyo amesema tangu amemfahamu hajawahi kumuona akigombana na mtu yeyote na mara zote amekuwa akicheka na watu na pia hajawahi kupelekwa kwenye Serikali ya kijiji kwa tuhuma zozote, hivyo kifo chake kimeacha maswali mengi kwa wananchi wa Mang'ula na hata maeneo ya jirani.

Kufuatia tukio hilo, katibu huyo amesema Serikali ya kijiji imepanga kuitisha mkutano mkubwa wa wananchi kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya kuepukana na matukio kama hayo ambayo yanaweza kutokea, pia ameliomba Jeshi la Polisi kutenda haki ili wote waliohusika na mauaji hayo wakamatwe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama akizungumza na waandishi wa habari, amesema mwalimu huyo akiwa amelala na mtuhumiwa (mke wake) na watoto wao wawili, alivamiwa ndani na kuuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani.

Kamanda Mkama amesema baada ya mauaji hayo, jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kuwapata watuhumiwa wengine ambao wanatuhumiwa kushirikiana na mwanamke huyo.
Boda wanaendelea kutafuna vinono Mbozi: Mke amuua Mume Wake akishirikiana na Mchepuko
 
Back
Top Bottom