Morogoro Day Trip: Kwa Wakazi wa Dar & Pwani

Umenikumbusha mbali. Kwakweli ni ka experience kazuuuri japo nilitaka kufika morning site ila nikakata moto njiani[emoji1787]

Mandhari, hewa saaafi, kaubaridi kwa mbali.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ni experience nzuri sana ila usiombe kukata moto, sisi tulipanda milima ya Udzungwa kule Sanje waterfalls kuna top na bottom, unachagua uende wapi

Yani ile tumefika tu top, nilijitupa chali huku nahema juu juu nikasema sirudii tena, Sasa hivi mlima pekee ninaoutamani ni Kilimanjaro tu mingine sitaki kuisikia
 
🤣🤣🤣🤣🤣Vimilima vya Goba tu vinanitoaga jasho vya huko naweza Anza kulia bureee
Basi anza mazoezi kabla ya kupanda milima mikubwa, kama vimiinuko vya Goba, Makabe, Msumi huviwezi basi kauzito kaangaliwe upya🤣
 
Hongera sana mkuu. kuna siku nilenda hapo nikiwa na babe wangu. tulitoka mjini moro kwa taxi, ilipoishia tukapanda boda, mpaka kwenye maporomoko fulani hivi
Katika ku enjoy hapo kulikuwa na kundi la watu wamekuja kushangaa sisi. Bwanaeeeh ,dogo mmoja akajirusha kwenye maji, akawa hatokezi juu tena. alipopatikana akawa amekata moto, haonyeshi dalili za kupumua.
Shughuli ilikuwa kumtoa huko mlimani na kumfikisha town ili apate msaada
Baadae nasikia alikata moto. ni pazuri ila kupata msaada ndo changamoto
 
Safi sana chief umenikumbusha mwaka 2014 nilipanda huko na group la majamaa ,mabonge yenye vitambi hayakutoboa tuliyaacha katikati huko juu Kuna campsite Moja wanahuduma poa sana tulinunua mbuzi na kuku wakutosha tukaacha mabonge yasimamie nyama choma na supu tukishuka kileleni tuishi vizuri na gambe kiufupi Mzee wakaz umeelezea vizuri sana uzoefu wako
 
Aaaah ile siku sitakaa niisahau maana nilikurupuka tu baada ya kupata kampani na by then sikuwa na mazoezi yoyote.
Shughuli kubwa ikawa kushuka sasa, miguu haitaki, nilitamani nikae chini nijiburuze🤣🤣🤣🤣

Kilimanjaro yenyewe nilishindwa🤣
Hebu tuanze kwanza na hii ya Morning site then tujipange kwa kilimanjaro baby.
 
Uduzungwa naionaga imekaa shagalabagala haivutii kupanda eti🙆🙆🙆
 
Dah ndio mitaa yenu nini? Kuzuri sana aisee kipindi cha mvua kuna hali ya hewa moja amazing.
 
Hahaa.. Sanje unafikia wapi? Ruaha pale kwenye kiwanda cha Sukari au? Nataka nijaribu siku.
 
Dah pole kwa familia ya dogo ila ndio maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…