Morogoro Day Trip: Kwa Wakazi wa Dar & Pwani

Hahaaa eti nilikurupuka baada ya kupata kampani, wallahi usipokuwa na mazoezi unaweza jiuliza hivi ni nini kilinileta huku, hapo kwenye kushuka acha kabisa unaweza tamani ushuke kwa kubiringita tu

Mimi kwa sasa kupanda milima ni hadi nipunguze huu uzito nilionao ndio tatizo, maana kwa kimo changu sitakiwi kuwa na uzito huu, nikiweza hilo tu basi naweza kuwa hiker na climber mzuri sana

Sababu nimi niko vizuri kwenye Kutembea ila milima mikubwa tu ndio tabu kupanda, niliwahi jaribu na Mlima Loleza Mbeya nikaishia njiani, ila eneo tambarare ukiniambia tutembee ushindwe wewe tu
 
Hii kitu ni nzuri sana kwa couple, inaimarisha bond.

Surely mkuu G… mm kuna mdada ofsn alikuwa just a co worker.. ila ikaanza natoka nae tu tumeenda kula, mara tumesindikizana pale, wkend tumeenda wapi, mara hivi… sahivi bond imekomaa kaja kuwa best of the besties…

Kaka angu Certified Hater achukue desa
Ajikute tu eti hapendi heka heka za kuzurula.
Mimi kama dada mkuu nitahakikisha wifi anakutembezaaa
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Mkuu msituni nyoka si ndio nyumbani kwake?
Aisee hapana,kwahyo nawe ulikutana nao?Sitakaa nithubutu huo utalii kama mambo yenyewe ni hayo,Bora vinipite[emoji16]
 
Mimi kwetu moro huko nimenunua eneo lina kama heka 3 hivi lina muonekano mzuri sana, nimeshajenga kibanda ila soon naenda kutusua mjengo wa maana mixer makuku, mbuzi n.k
 
Yaani ilikuwa ni ile "kesho tunakwenda hiking milima ya Uluguru hadi Morning site, Atoto are you inn?" sasa sijui nilifikiria ni kakichuguu naenda kupanda🙆🙆🙆 si nikakurupuka!!

Nilifika mahali morning site napaona paleeee ila nguvu za kuendelea sina🤣🤣🤣
Nikawaambia waende tu watanikuta.

Kurudi saaaasa na kunyeshewa juu, niliumwaaa. Kesho yake asubuhi nikaamshwa tukakimbie lasivyo nitalazwa, nikawaambia nendeni tu niko tayari mnizike ila sio kwenda kukimbia.
 
Uduzungwa naionaga imekaa shagalabagala haivutii kupanda eti[emoji134][emoji134][emoji134]
Mmhh sijajua labda inategemea unaview kutokea wapi maana ile milima safu yake iko Morogoro na Iringa, sisi tuliingia kule kwenye national park kabisa kisha tukapanda ule upande wenye waterfalls ambao ni upande wa Moro, panavutia maana kuna sehemu kwenye yale maporomoko pametengeneza kitu kama ramani ya Africa
 
....hahah masister wengine nuksi sana sasa shida zangu zimekua taarifa ya habari.. Siendi sasa Mchukue mmeo Plan Master mkatembezane huko.
 
Hahaa.. Sanje unafikia wapi? Ruaha pale kwenye kiwanda cha Sukari au? Nataka nijaribu siku.
No unasogea mbele zaidi unaipita hadi Kidatu, ni national park kabisa kuna Geti unaingia nadhani ukiulizia watakuelekeza zaidi huko njiani then wale tour guides ndio watakuelekeza pa kuikuta Sanje Trail, sijajua ukitaka kupanda mwenyewe inakuwaje maana sisi tulipanda na tour guides
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kichuguu..
Kwakweli hiyo ya kutakiwa uendelee kufanya tena zoezi jingine ili usiumwe baada ya kutoka kufanya zoezi fulani kubwa huwa inakera sema basi tu ni vile ndio tiba
 
Nilifanya huko Mikumi Sia sahau nilirudi naumwa siku 3 na dawa za maumivu juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…