Morogoro: Magari sita ya abiria yakamatwa yakiwa na misiba feki

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limekamata mabasi sita yakisafirisha abiria yakiwa na mashada ya maua kuashiria yanasafirisha majeneza yenye miili ya marehemu wakati ni uongo.

Mabasi hayo madogo yalikamtwa usiku wa kuamkia jana katika kizuizi cha polisi kiliyowekwa eneo la Kingolwira katika Manispaa ya Morogoro, Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Juni 21, mwaka huu saa nne usiku basi dogo lililotumia uongo kama huo liligongana na magari mengine mawili eneo Nane Nane katika manispaa hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa.

Ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 689 DUK likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya likagonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T563 ASA na baadaye Coaster likagongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T658 DJZ mali ya Kampuni ya Dangote.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu alisema kati ya mabasi hayo sita manne yalitoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mawili yalitoka Kahama mkoani Shinyanga yakienda Dar es Salaam.

Kamanda Musilimu aliyasema hayo jana katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Kingolwira alipokuwa akitoa taarifa kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroard Mutafungwa.

“Hayakuwa na majeneza wala kitu chochote ila waliweka mashada ya maua na yamezuiliwa na wahusika kuendelea kuhojiwa,” alisema Kamanda Musilimu.

Aliongeza, “Tunawahoji wanakwenda wapi na gari mojawapo lililokutwa na mashada ya maua na abiria wao walidai wanakwenda kwenye msiba…tumelizuia hakuna jeneza la mwili wa marehemu tunataka kudhibiti huu ujanja ujanja waambieni wale wanaotumia magari haya wafuate utaratibu na operesheni hii ni endelevu kwa madereva wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa wenye kubainika na makosa.”

Alisema mabasi mengine madogo sita yaliyokuwa na mashada ya maua yalikaguliwa na kukutwa na majeneza yenye miili na wahusuka waliruhusiwa kuendelea na safari.

Kamanda Mutafungwa alisema kuanzia sasa katika mikoa yote vizuizi vya ukaguzi barabarani vitaongezwa na kuimarishwa hasa usiku.

“Vipo vituo Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, pia vipo Mbeya, Tukuyu, Njombe na Songwe, Kilimanjaro eneo la Himo, Morogoro stendi ya Dodoma na Mikumi, sasa ninawalekeza wamiliki wa magari haya wafuate sheria zote na abiria hasa wafanyabiashara kuanzia leo wasipande haya magari ili kuepuka kusumbuliwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Alimtaka mmiliki wa basi dogo lililosababisha ajali na vifo na dereva aliyekuwa akiliendesha wajisalimishe kituo cha Polisi ndani ya saa 24 kuanzia jana.

Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro, Andrew Mlacha alisema operesheni ya ukaguzi wa mabasi madogo katika wiki moja iliyopita magari zaidi ya 25 yenye makosa yalikamatwa na kulipishwa faini na kutakiwa kurekebisha makosa.

“Kwa sasa tumeongeza operesheni ili kudhibiti ajali, magari lazima yakaguliwe na kufungwa vidhibiti mwendo na iwapo inaharibika abiria anakuwa na haki zake za msingi, lakini kwa sasa magari haya hayatoi risiti, hayana kituo maalumu na hata bima zake ni za mashaka,” alisema Mlacha.
 
... Ok; japo haijaelezwa sababu ya coasters kuweka mashada but i think ni ili yaweze kupiga pesa kwa kuiba route kupeleka waombolezaji feki mikoani. Ila na sisi wananchi sijui tunawazaga nini how can you risk your life kwa negligence ya namna hiyo? Unakutana na ki-Ractis au Fun Cargo kinaitia abiria wa Mbeya tena usiku mnene na wewe unaingia! Dah!
 
Hujakutwa na dharura wewe, watu wanaishia na wanahitaji kutumia mda wa usiku na asubuhi wanakua wamefika. Badala ya kutumia mchana wote kusafiri unafika uendako usiku, unalala tena! Watu we nasafiri kila siku usiku nahivyo hivyo vi fancargo na wanafika salama.
 
... Ok; japo haijaelezwa sababu ya coasters kuweka mashada but i think ni ili yaweze kupiga pesa kwa kuiba route kupeleka waombolezaji feki mikoani. Ila na sisi wananchi sijui tunawazaga nini how can you risk your life kwa negligence ya namna hiyo? Unakutana na ki-Ractis au Fun Cargo kinaitia abiria wa Mbeya tena usiku mnene na wewe unaingia! Dah
Hapo nafikiri hao jamaa watakua walikua wanawasafirisha kwa bei chee ndio maana watu wakavutika kupanda hizo gari.
 
Maisha bwana, yaani leo Muslimu anatoa taarifa kwa Kamanda wa Usalama Barabarani!!
 
Tunajifungafunga na kwa Sheria na Matamko
 
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limekamata mabasi sita yakisafirisha abiria yakiwa na mashada ya maua kuashiria yanasafirisha majeneza yenye miili ya marehemu wakati ni uongo.
Mabasi hayo madogo yalikamtwa usiku wa kuamkia jana katika kizuizi cha polisi kiliyowekwa eneo la Kingolwira katika Manispaa ya Morogoro, Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Juni 21, mwaka huu saa nne usiku basi dogo lililotumia uongo kama huo liligongana na magari mengine mawili eneo Nane Nane katika manispaa hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa.
Ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 689 DUK likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya likagonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T563 ASA na baadaye Coaster likagongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T658 DJZ mali ya Kampuni ya Dangote.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu alisema kati ya mabasi hayo sita manne yalitoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mawili yalitoka Kahama mkoani Shinyanga yakienda Dar es Salaam.

Kamanda Musilimu aliyasema hayo jana katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Kingolwira alipokuwa akitoa taarifa kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroard Mutafungwa.

“Hayakuwa na majeneza wala kitu chochote ila waliweka mashada ya maua na yamezuiliwa na wahusika kuendelea kuhojiwa,” alisema Kamanda Musilimu.

Aliongeza, “Tunawahoji wanakwenda wapi na gari mojawapo lililokutwa na mashada ya maua na abiria wao walidai wanakwenda kwenye msiba…tumelizuia hakuna jeneza la mwili wa marehemu tunataka kudhibiti huu ujanja ujanja waambieni wale wanaotumia magari haya wafuate utaratibu na operesheni hii ni endelevu kwa madereva wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa wenye kubainika na makosa.”

Alisema mabasi mengine madogo sita yaliyokuwa na mashada ya maua yalikaguliwa na kukutwa na majeneza yenye miili na wahusuka waliruhusiwa kuendelea na safari.
Kamanda Mutafungwa alisema kuanzia sasa katika mikoa yote vizuizi vya ukaguzi barabarani vitaongezwa na kuimarishwa hasa usiku.

“Vipo vituo Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, pia vipo Mbeya, Tukuyu, Njombe na Songwe, Kilimanjaro eneo la Himo, Morogoro stendi ya Dodoma na Mikumi...sasa ninawalekeza wamiliki wa magari haya wafuate sheria zote na abiria hasa wafanyabiashara kuanzia leo wasipande haya magari ili kuepuka kusumbuliwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Alimtaka mmiliki wa basi dogo lililosababisha ajali na vifo na dereva aliyekuwa akiliendesha wajisalimishe kituo cha Polisi ndani ya saa 24 kuanzia jana.

Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro, Andrew Mlacha alisema operesheni ya ukaguzi wa mabasi madogo katika wiki moja iliyopita magari zaidi ya 25 yenye makosa yalikamatwa na kulipishwa faini na kutakiwa kurekebisha makosa.

“Kwa sasa tumeongeza operesheni ili kudhibiti ajali, magari lazima yakaguliwe na kufungwa vidhibiti mwendo na iwapo inaharibika abiria anakuwa na haki zake za msingi, lakini kwa sasa magari haya hayatoi risiti, hayana kituo maalumu na hata bima zake ni za mashaka,” alisema Mlacha.
Na polisi waende mbali zaidi , kukagua kuwa waliomo kwenye jeneza wamekufa kweli au gelesha tu!
 
Mpaka wanafanya yote hayo wanakwepa nini ama kuficha kitu gani?

... Ok; japo haijaelezwa sababu ya coasters kuweka mashada but i think ni ili yaweze kupiga pesa kwa kuiba route kupeleka waombolezaji feki mikoani. Ila na sisi wananchi sijui tunawazaga nini how can you risk your life kwa negligence ya namna hiyo? Unakutana na ki-Ractis au Fun Cargo kinaitia abiria wa Mbeya tena usiku mnene na wewe unaingia! Dah!

Hapo nafikiri hao jamaa watakua walikua wanawasafirisha kwa bei chee ndio maana watu wakavutika kupanda hizo gari.
Haya magari kazi yake huwa ni kusafirisha wafanyabiashara usiku(Hakuna kulala) mara nyingi wanaelekea mikoa ya nyanda za juu kununua mazao kama viazi,mchele no

Ila toka wiki hii ianze LATRA(SUMATRA ya zamani) walikua na oparesheni ya kuyakamata kwakua hayana vibali vya kubeba abiria(zaidi ya kukodishwa) walikua na barrier hapo mkoa wa pwani

Ndo watu wa kwanza kujiongeza kuweka mashada na kulia wakizuiwa kwenye berrier wanaachiwa.

Sasa ile iliyopata ajali ndo imekoroga maji
 
Hivi unaweza kum-outsmart askari wa barabarani kweli kwa mauzauza kama haya!??? Labda waamue wenyewe kuwafumbia macho. Eti Infantry Soldier 🙂
 
Kupitia train ya umeme
HATUTAKUWA na mambo kama hayo ali mradi kuharakisha safari

Ndani ya nusu saa upo morogoro
Na ndani ya Saa moja unakua umefika Dodoma. Maisha yanakua marahisi
 
Haya magari kazi yake huwa ni kusafirisha wafanyabiashara usiku(Hakuna kulala) mara nyingi wanaelekea mikoa ya nyanda za juu kununua mazao kama viazi,mchele no

Ila toka wiki hii ianze LATRA(SUMATRA ya zamani) walikua na oparesheni ya kuyakamata kwakua hayana vibali vya kubeba abiria(zaidi ya kukodishwa) walikua na barrier hapo mkoa wa pwani

Ndo watu wa kwanza kujiongeza kuweka mashada na kulia wakizuiwa kwenye berrier wanaachiwa.

Sasa ile iliyopata ajali ndo imekoroga maji
Dah! Watu wanajuwa kufikiria jinsi ya kukwepa usumbufu wa Mamlaka!!
 
Hujakutwa na dharura wewe, watu wanaishia na wanahitaji kutumia mda wa usiku na asubuhi wanakua wamefika. Badala ya kutumia mchana wote kusafiri unafika uendako usiku, unalala tena! Watu we nasafiri kila siku usiku nahivyo hivyo vi fancargo na wanafika salama.
... Coasters 6 zimejaa wote wana dharura na mashada wamewekewa? Kuwa serious Mkuu.
 
Haya magari kazi yake huwa ni kusafirisha wafanyabiashara usiku(Hakuna kulala) mara nyingi wanaelekea mikoa ya nyanda za juu kununua mazao kama viazi,mchele no

Ila toka wiki hii ianze LATRA(SUMATRA ya zamani) walikua na oparesheni ya kuyakamata kwakua hayana vibali vya kubeba abiria(zaidi ya kukodishwa) walikua na barrier hapo mkoa wa pwani

Ndo watu wa kwanza kujiongeza kuweka mashada na kulia wakizuiwa kwenye berrier wanaachiwa.

Sasa ile iliyopata ajali ndo imekoroga maji
Marathon day; hiyo ndio sababu! Hakuna cha dharura japo dharura pia zipo.
 
Back
Top Bottom