Morogoro: Magari sita ya abiria yakamatwa yakiwa na misiba feki

Morogoro: Magari sita ya abiria yakamatwa yakiwa na misiba feki

Mpaka wanafanya yote hayo wanakwepa nini ama kuficha kitu gani?
Kuna harufu ya sembe siku zijazo haya ni maandalizi kama sio ndugu wanaoenda kumzika ndugu yao mikoani na kuamua kuchukua usafiri wa pamoja au wakifanya taratibu za kupeleka msiba nyumbani kwa wasiwa yote yanawezekana.
 
... Ok; japo haijaelezwa sababu ya coasters kuweka mashada but i think ni ili yaweze kupiga pesa kwa kuiba route kupeleka waombolezaji feki mikoani. Ila na sisi wananchi sijui tunawazaga nini how can you risk your life kwa negligence ya namna hiyo? Unakutana na ki-Ractis au Fun Cargo kinaitia abiria wa Mbeya tena usiku mnene na wewe unaingia! Dah!
yaani sisi watanzania, au waafrika kwa ujumla, tuna shida sana na kutuongoza sisi ni kazi kubwa mno. kuna mambo mengine binadamu wenzetu wanafanya mpaka unashangaa tuna matatizo gani?!!!!

mfano mwingine unaweza ukaonekana kwenye haya magari ya abiria; dereva anapiga mwendo si wa kawaida na wa hovyo hovyo tu, kuwapita wenzie milimani n.k. askari wa usalama akija kuwauliza baadae kama kuna tatizo au la, wote wanajibu 'HAPANA'! ole wako ujitokeze na kusema kweli, utalaaniwa na abiria wenzio mpaka basi...tena unaweza kupigwa kabisa. mwishowe askari wenyewe wanaamua kujichukulia rushwa tu basi
 
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limekamata mabasi sita yakisafirisha abiria yakiwa na mashada ya maua kuashiria yanasafirisha majeneza yenye miili ya marehemu wakati ni uongo.

Mabasi hayo madogo yalikamtwa usiku wa kuamkia jana katika kizuizi cha polisi kiliyowekwa eneo la Kingolwira katika Manispaa ya Morogoro, Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Juni 21, mwaka huu saa nne usiku basi dogo lililotumia uongo kama huo liligongana na magari mengine mawili eneo Nane Nane katika manispaa hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa.

Ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 689 DUK likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya likagonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T563 ASA na baadaye Coaster likagongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T658 DJZ mali ya Kampuni ya Dangote.
Udanganyifu huu ni syndicate ya Polisi na hao wasafirishaji, ni kwamba hiyo ajali mbaya imewaumbua, ukweli ni kwamba hizo check points zipo siku nyingi na hayo mabasi hukaguliwa kwasababu usiku huwa askari wanasimamisha magari yote na kuyakagua, je ina maana huwa hawaoni hayo yanayofanywa na hao madereva?

Tunaambiwa hayo magari huwekwewa misalaba na mashada yanaposafiri usiku ili yasisumbuliwe, swali ni je humo kwenye check points askari huwa wanaionaje hiyo misalaba na mashada wakati yanapokuja kwa mbele askari hawaioni misalaba na mashada, nikimaanisha huwa wanatambuliwaje? si mpaka wasimamishwe?
 
Back
Top Bottom