Morogoro: Magari sita ya abiria yakamatwa yakiwa na misiba feki

Morogoro: Magari sita ya abiria yakamatwa yakiwa na misiba feki

Watanzania hamueleweki mnataka nini. Magumashi na ujanja ujanja ukidhibitiwa mnapiga kelele na ukiachiwa mnapiga kelele.
... huyo jamaa uliyem-quote ni bonge la pro-jiwe! Alichoandika ni kebehi msome between the lines.
 
Kupitia train ya umeme
HATUTAKUWA na mambo kama hayo ali mradi kuharakisha safari

Ndani ya nusu saa upo morogoro
Na ndani ya Saa moja unakua umefika Dodoma. Maisha yanakua marahisi
... wengi wa wafanyabiashara wa usiku wanaelekea Nyanda za Juu; SGR inaelekea Kanda ya Kati na Ziwa.
 
Hayo magari ukishapanda yan unalipa nauli yako na ukisimamishwa na polisi mnatakiwa mlie bila sababu
... duh! Mateso yote ya nini! Halafu kwa upumbavu wanadhani polisi hawawezi kugundua? Miongoni mwa abiria polisi wamo humo humo!
 
Yale yale ya museven kuzika majeneza tupu.

oooh misafara ya misiba imezidi kumbe maigizo tupu
 
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limekamata mabasi sita yakisafirisha abiria yakiwa na mashada ya maua kuashiria yanasafirisha majeneza yenye miili ya marehemu wakati ni uongo.

Mabasi hayo madogo yalikamtwa usiku wa kuamkia jana katika kizuizi cha polisi kiliyowekwa eneo la Kingolwira katika Manispaa ya Morogoro, Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Juni 21, mwaka huu saa nne usiku basi dogo lililotumia uongo kama huo liligongana na magari mengine mawili eneo Nane Nane katika manispaa hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa.

Ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 689 DUK likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya likagonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T563 ASA na baadaye Coaster likagongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T658 DJZ mali ya Kampuni ya Dangote.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu alisema kati ya mabasi hayo sita manne yalitoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mawili yalitoka Kahama mkoani Shinyanga yakienda Dar es Salaam.

Kamanda Musilimu aliyasema hayo jana katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Kingolwira alipokuwa akitoa taarifa kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroard Mutafungwa.

“Hayakuwa na majeneza wala kitu chochote ila waliweka mashada ya maua na yamezuiliwa na wahusika kuendelea kuhojiwa,” alisema Kamanda Musilimu.

Aliongeza, “Tunawahoji wanakwenda wapi na gari mojawapo lililokutwa na mashada ya maua na abiria wao walidai wanakwenda kwenye msiba…tumelizuia hakuna jeneza la mwili wa marehemu tunataka kudhibiti huu ujanja ujanja waambieni wale wanaotumia magari haya wafuate utaratibu na operesheni hii ni endelevu kwa madereva wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa wenye kubainika na makosa.”

Alisema mabasi mengine madogo sita yaliyokuwa na mashada ya maua yalikaguliwa na kukutwa na majeneza yenye miili na wahusuka waliruhusiwa kuendelea na safari.

Kamanda Mutafungwa alisema kuanzia sasa katika mikoa yote vizuizi vya ukaguzi barabarani vitaongezwa na kuimarishwa hasa usiku.

“Vipo vituo Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, pia vipo Mbeya, Tukuyu, Njombe na Songwe, Kilimanjaro eneo la Himo, Morogoro stendi ya Dodoma na Mikumi, sasa ninawalekeza wamiliki wa magari haya wafuate sheria zote na abiria hasa wafanyabiashara kuanzia leo wasipande haya magari ili kuepuka kusumbuliwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Alimtaka mmiliki wa basi dogo lililosababisha ajali na vifo na dereva aliyekuwa akiliendesha wajisalimishe kituo cha Polisi ndani ya saa 24 kuanzia jana.

Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro, Andrew Mlacha alisema operesheni ya ukaguzi wa mabasi madogo katika wiki moja iliyopita magari zaidi ya 25 yenye makosa yalikamatwa na kulipishwa faini na kutakiwa kurekebisha makosa.

“Kwa sasa tumeongeza operesheni ili kudhibiti ajali, magari lazima yakaguliwe na kufungwa vidhibiti mwendo na iwapo inaharibika abiria anakuwa na haki zake za msingi, lakini kwa sasa magari haya hayatoi risiti, hayana kituo maalumu na hata bima zake ni za mashaka,” alisema Mlacha.
Huu ni upuuzi, what if mwili wa marehemu ulitangulia na ndege, au tu watu wanakwenda msibani mikoa hiyo. Yaani ili uweke maua ni lazima uwe na maiti? Gari inakwenda msibani, basi.
Hawa jamaa bana.
 
Juni 21, mwaka huu saa nne usiku basi dogo lililotumia uongo kama huo liligongana na magari mengine mawili eneo Nane Nane katika manispaa hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa.
Polisi: aibu yenu hiyooooooooo
 
Hivi unaweza kum-outsmart askari wa barabarani kweli kwa mauzauza kama haya!??? Labda waamue wenyewe kuwafumbia macho. Eti Infantry Soldier 🙂
Inawezekana
Juzi dreva alitumia mbinu ya KUMWAMBIA askari tuliomo kwenye coaster ni watalii KWA hiyo hawana tiketi
Tulicheka sana baada ya askari kuturuhusu
Ila askari hawajiongezi kabisa, huwez mkagua hata huyo mtalii ujue amebeba nn na safar yake ya utalii inaanzia wapi na kuishia wapi
Hopeless kabisa
 
... wengi wa wafanyabiashara wa usiku wanaelekea Nyanda za Juu; SGR inaelekea Kanda ya Kati na Ziwa.
Nafahamu hilo.
Wataunganisha usafiri kwa kuanza na usafiri wa reli kisha watamaliza na barabara

Japo sijajua umemaanisha nyanda za juu mikoa gani hasa ?
 
Hivi unaweza kum-outsmart askari wa barabarani kweli kwa mauzauza kama haya!??? Labda waamue wenyewe kuwafumbia macho. Eti Infantry Soldier 🙂
Kwanza naomba uelewe ishu mwanzoni haikua ya polisi Bali LATRA ndo walikua wanzuia. Polisi walikua pale kufacilitate tu

Na YES walikua outsmarted sana tu kwakua watu wamesafiri zaidi ya siku 7 (toka waanze hiyo oparesheni LATRA sio hii ya Polisi)mpaka hiyo juzi ile ilivyogongana na Dangote

Na pia haikua ishu kubwa kwakua kizuizi kilikua ni kimoja tu ukitoka hapo tayari kila sehemu unapita safi tu mradi unafuata sheria za barabarani

Ila kama wakitaka kufuatilia ni ngumu kwakua hata maiti ina document za kuwa nayo watapatikana tu kirahisi. Ila mwanzoni ile ilikua ni kuwakwepa hao LATRA tu ambao walikua hawana mambo mengi kwahiyo mtelezo
 
... duh! Mateso yote ya nini! Halafu kwa upumbavu wanadhani polisi hawawezi kugundua? Miongoni mwa abiria polisi wamo humo humo!
Bahat mbaya watu wa magari huwa wanasahau kuwapanga abiria mwsho wakikamatwa Polisi wanacho kifanya huwa wanachukua mmoja mmoja wanauliza aliekufa ni jinsia gan? Mmoja anasema aliekufa ni mwanaume alaf abiria mwingine anasema aliekufa ni mwanamke na wote kweny gar wanajidai ni ndugu wa marehem wakiulizwa jina la marehem ni nani ? Ndo hapo kila mmoja anaanza kumruka mwenzake
 
Huu ni upuuzi, what if mwili wa marehemu ulitangulia na ndege, au tu watu wanakwenda msibani mikoa hiyo. Yaani ili uweke maua ni lazima uwe na maiti? Gari inakwenda msibani, basi.
Hawa jamaa bana.
... kama maiti imetangulia au itakuja baadaye mbona simple tu! Mtaulizwa swali rahisi tu; abiria aliyekaa kona ya mbele na aliyekaa kona ya nyuma wataulizwa jina la marehemu! Kama mnaenda msibani kweli majibu yenu yata-match; vinginevyo ...! Vitu vingine sio vya kudanganya ndugu!
 
Inawezekana
Juzi dreva alitumia mbinu ya KUMWAMBIA askari tuliomo kwenye coaster ni watalii KWA hiyo hawana tiketi
Tulicheka sana baada ya askari kuturuhusu
Ila askari hawajiongezi kabisa, huwez mkagua hata huyo mtalii ujue amebeba nn na safar yake ya utalii inaanzia wapi na kuishia wapi
Hopeless kabisa
Mtakuwa nyie abiria mlilizwa vya machoni; kwani hamkumwona askari akivua kofia yake akamkabidhi askari, kisha akaichukua tena!??? Amkeni nyie!!!
 
Inawezekana
Juzi dreva alitumia mbinu ya KUMWAMBIA askari tuliomo kwenye coaster ni watalii KWA hiyo hawana tiketi
Tulicheka sana baada ya askari kuturuhusu
Ila askari hawajiongezi kabisa, huwez mkagua hata huyo mtalii ujue amebeba nn na safar yake ya utalii inaanzia wapi na kuishia wapi
Hopeless kabisa
Aliamua kuwapotezea tu huwa wakiamua kukaza barabara zinakua za Moto sana
 
... Coasters 6 zimejaa wote wana dharura na mashada wamewekewa? Kuwa serious Mkuu.
Nijuavyo na nishasafiri mara nyingi na hizi coster. Kutoka mbeya wanapakilia uyole, pale kuna wafanya biashara wanakuja Dar kununua mahitaji ya madukani , wafike asubuhi wananunua wanapakia kwenye mafuso then wanapanda tena Costa Dr wanarudi makwao, hapo Wana save ku lala guest. Ukichanganya na dharura nyingine, mtu unashunguki Dar au Mbeya inakulazimu utembee usiku iki ukifika kesho yake asubuhi unafikia kufanya ulichokijia, kuliko kutembea mchana na ukifika uendako ni usiku unalala tena. Unakua ushapoteza siku nzima bura
 
Bahat mbaya watu wa magari huwa wanasahau kuwapanga abiria mwsho wakikamatwa Polisi wanacho kifanya huwa wanachukua mmoja mmoja wanauliza aliekufa ni jinsia gan? Mmoja anasema aliekufa ni mwanaume alaf abiria mwingine anasema aliekufa ni mwanamke na wote kweny gar wanajidai ni ndugu wa marehem
Kiraka, jibu lingine hilo! Mtapigwa cross-exam mtajichanganya tu! Usijaribu kudanganya visivyodanganyika; never!
 
Inawezekana
Juzi dreva alitumia mbinu ya KUMWAMBIA askari tuliomo kwenye coaster ni watalii KWA hiyo hawana tiketi
Tulicheka sana baada ya askari kuturuhusu
Ila askari hawajiongezi kabisa, huwez mkagua hata huyo mtalii ujue amebeba nn na safar yake ya utalii inaanzia wapi na kuishia wapi
Hopeless kabisa
Sema hii ishu sio ya askari kuwa hopeless. Haya mambo tunayafanya yawezekane sie abiria. Unakuta abiria tushakubaliana na hiyo hali kwahiyo culprits ni zaidi ya dereva na tingo. Askari anahitaji ushirikiano wa abiria kama abiria ndo wanaona hiyo ni njia sahihi askari hana cha kufanya...kikubwa uhai tu mazes😂😂

Ungejaribu kusema pale kwa askari kuwa sie sio watalii ni abiria tu ila hatujapewa ticket uone moto wake(kutoka kwa abiria pia)
 
Uwepo wa mashada haumaanishi wamebeba maiti. Labda kama PDP ni yule wa aliyekwenda zake.
 
Uwepo wa mashada haumaanishi wamebeba maiti. Labda kama PDP ni yule wa aliyekwenda zake.
... sahihi kabisa; kama ndivyo, onesha kibali cha kukuruhusu kwenda ruti hiyo.
 
Back
Top Bottom