Morogoro: Magari sita ya abiria yakamatwa yakiwa na misiba feki

Mpaka wanafanya yote hayo wanakwepa nini ama kuficha kitu gani?
Kuna harufu ya sembe siku zijazo haya ni maandalizi kama sio ndugu wanaoenda kumzika ndugu yao mikoani na kuamua kuchukua usafiri wa pamoja au wakifanya taratibu za kupeleka msiba nyumbani kwa wasiwa yote yanawezekana.
 
yaani sisi watanzania, au waafrika kwa ujumla, tuna shida sana na kutuongoza sisi ni kazi kubwa mno. kuna mambo mengine binadamu wenzetu wanafanya mpaka unashangaa tuna matatizo gani?!!!!

mfano mwingine unaweza ukaonekana kwenye haya magari ya abiria; dereva anapiga mwendo si wa kawaida na wa hovyo hovyo tu, kuwapita wenzie milimani n.k. askari wa usalama akija kuwauliza baadae kama kuna tatizo au la, wote wanajibu 'HAPANA'! ole wako ujitokeze na kusema kweli, utalaaniwa na abiria wenzio mpaka basi...tena unaweza kupigwa kabisa. mwishowe askari wenyewe wanaamua kujichukulia rushwa tu basi
 
Udanganyifu huu ni syndicate ya Polisi na hao wasafirishaji, ni kwamba hiyo ajali mbaya imewaumbua, ukweli ni kwamba hizo check points zipo siku nyingi na hayo mabasi hukaguliwa kwasababu usiku huwa askari wanasimamisha magari yote na kuyakagua, je ina maana huwa hawaoni hayo yanayofanywa na hao madereva?

Tunaambiwa hayo magari huwekwewa misalaba na mashada yanaposafiri usiku ili yasisumbuliwe, swali ni je humo kwenye check points askari huwa wanaionaje hiyo misalaba na mashada wakati yanapokuja kwa mbele askari hawaioni misalaba na mashada, nikimaanisha huwa wanatambuliwaje? si mpaka wasimamishwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…