Morogoro mjini: Mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA Bi Devotha Minja arejeshwa rasmi na NEC

Morogoro mjini: Mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA Bi Devotha Minja arejeshwa rasmi na NEC

Ndugu zangu wa Morogoro wamerogwa na basi la bure la Abood la kuzikia. Niliongea na watu kadhaa wa Moro kuhusu siasa za upinzani. Hawakutaka kabisa kunielewa. Sababu kubwa ni Abood kawapa basi la bure la kuzika pindi wapatwapo na msiba.
Sababu nyingine ni hile Roho ya Kazopata Waruguru ndugu zangu inawasumbua sana. Waliniambia wakichagua mswahili mwenzao akipata Ubunge atawavimbia sana. Hivyo ni bora wampe Mwarabu tu.
 
Aaagh Mkuu Kwani Ni kweli?!!!

Tuwekee Ushahidi Mkuu ili Taifa liwe Bora zaidi...

Ungetaka Taifa liwe bora usingefanya yale uliyofanya ya kuwanunua wapinzani hasa wabunge wa Chadema ili boss wako apite kwa urahisi!!! Ile ilikuwa RUSHWA ya wazi wazi, sasa unauliza ushahidi wa huyo tajiri wa Morogoro kama alihonga!!
 
Utanzania ni kabila. Nyerere alimpa uwaziri Jamal matokeo yake akaukana Utanzanja na kuwa m-Canada hadi kazikwa huko.

Narudi tena mhindi siyo mtanzania kamwe. Labda awe mwarabu siyo Mhindi. Wahindi karibu wote wa Tanzania wana uraia pacha ama wa India/Pakistan, UK au Canada.
Wanajibanza ccm ili waibe na kulindwa. Hawana jema kwa nchi hii.
Utarudia Tena na tena..huo ni msimamo wako na una haki..

Umemtaja Jamal,wataje na kina Prof.Issa Shivji na wengine...

Nyerere Kama Mandela,alikuwa kinyume na wahafidhina mzee Mtemvu na "AILA" yako...
Mbona uko kinyume na mgombea wenu TAL ambaye anawahubiria UHURU HAKI NA MAENDELEO?!!!

Naweka kumbukumbu sahihi,kuwa Abood si "mhindi unayewachukia"...
Abood Ni Mtanzania,mwenye asili ya YEMEN..Kama Yemen Ni GUJARAT,sawa.....

No hard feelings kiongozi wangu!
Jah Bless
 
Wachaga wakagombee kwao waache kutusumbua
Huyo kanjibahi Abood(muarabu) ccm ni mluguru au ni mpogoro?acha kuleta ukabila,,ukienda mikumi Jose haule(mngoni)cdm ni mpogoro au ni mluguru?je gairo shabibi(muarabu)ccm ni mpogoro?je kabudi (mgogo)mgombea ccm kilosa ni mpogoro?na je Assenga(mchaga) mgombea ccm wa kilombero ni mpogoro ni mluguru?
 
Pressure toka kwa Tundu Lissu na nguvu ya umma ya Morogoro imefanikisha jambo hili.

Tujikumbushe : video
Agosti 25 , 2020
Morogoro, Tanzania

Live : mgombea wa CHADEMA , Devota Minja alivyozuiwa na 'mabaunsa' kibabe ktk ofisi ya umma kuingi ktk Ofisi ya mkurugenzi kurejesha fomu
 
11 Sep 2020
Morogoro, Tanzania

#LIVE TUNDU LISSU AUNGURUMA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2020 URAIS
Tundu Lissu alaani wagombea wa ubunge na udiwani wa CHADEMA kuenguliwa kihuni na kutaka warejeshwe :
Mgombea wa ubunge Morogoro mjini kupitia CHADEMA Devota Minja akisimulia mbele ya mgombea urais na umma wa wananchi alivyofanyiwa vituko na mabaunsa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri / Mji wa Morogoro
 
Back
Top Bottom