Morogoro ndio mkoa uliotoa vipaji vingi Tanzania kuliko mikoa mingine.

Ila ndiyo Mkoa uliojaa Majungu, Wivu, Fitina, Chuki kwa wasio Wazawa na Ushirikina uliopitiliza.
Na hii ndio sababu mkoa huu unadumaa licha ya kuwa na sifa nyingi kama alizoainisha mtoa mda, wenyeji wanapiga vita wawekezaji wageni kila leo..
 
Uko sahihi,kigoma,morogoro ba tanga ndio inaongoza kwa talent
Lakini picha ya mbaraka mwinshehe sijajua inafuata nini hapo
Mbaraka alipitia morogoro jazz na super volcano zote za morogoro ila hakuwa mlugulu bali alikuwa mdoe
Kumbuka alifia kenya kwa ajali.
Sasa siku maiti yake inaletwa tanzania msafara kufika chalinze watu wakajua utakunja kulia,badala yake ukakunja kushoto,hakuzikwa morogoro
Chalinze kukunja kushoto kuelekea wp??
 
Upo sahihi ata kwa upande wa vipaji vya boxing na soccer ,na iyo inatokana na kila mtaa kuwa na uwanja wa michezo na ligi mbalimbali hadi za njiwa😂😂tofauti na mikoa mingine , moro kitu kinachowakutanisha watoto na vijana kila jioni ni mpira wa miguu, tofauti na mikoa mingine, na sa hivi kuna boxing imeongezeka na music, list ya wacheza mpira naowahafu na nimeshuhudia hustle zao

1. Kibwana shomari
2. Dickson Job
3.Mzamiru
4.Nickson kibabage nk
Kuna akina mogella kuna saidi kambi kuna kaburu kina kilambo wapo wengi sana kwenye mpira.
 
Ila ndiyo Mkoa uliojaa Majungu, Wivu, Fitina, Chuki kwa wasio Wazawa na Ushirikina uliopitiliza.
Muongo mkubwa wewe..morogoro ni moja ya mikoa yenye wageni wengi zaidi hapa Tz chunguza hata matajiri wakubwa wa huu mkoa ni wageni...

Mji wa ifakara asilimia kubwa ya maduka makubwa ni ya wachaga na changamoto ni kwamba mchaga mwenzao akifa wanafunga maduka yote wanenda msibani

Ukiingia wilaya ya malinyi ni Kama umeingia usukumani jinsi walivyojaa

Njoo kilosa uone wagogo na wamasai walivyo wengi..

Nenda mahenge ulanga Kuna Kijiji kinaitwa ilonga hapo ni wandindo wa liwale walikuja enzi hizo wamezalia na vizazi vyao vimetapakaa moro yote

Sasa wewe sijiu unasemea morogoro ipi
 
Na wachaga wamejaa pia mahenge na matombo. Huko mgeta waha ndio wanaongoza kwa kilimo cha bangi.
 
Morogoro tumetoka wengi sana.....
Hata kwenye uongozi Dkt Ngasongwa,Martine Lumbanga,Celina Kombani, Profesa Ndulu Dkt Likwelile nk
Bila kumsahau mawakili wasomi kama Kibatala,Kusalika nk.
Morogoro imetoa watu wengi sana wenye vipaji vya hali ya juu anayebisha akale malimao/ndimu ya kutosha sana maana atakuwa na ujauzito mchanga.
 
Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo. Hapo Morogoro wametoka akina Albert Mangwea, mbaraka mwinshehe , twaha kiduku, francis Cheka, shomari kapombe n.k. Huwezi kwa sasa Tanzania kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro View attachment 2365081
Ni mkoa mzuri sana na wenye vipaji lukuki lakini naungana na MINOCYCLINE hapo juu kwa hoja alizotoa maana ni ukweli mtupu,japokuwa vipaji ni kweli vipo aisee maana tukiangalia nyanja hizi tunapata jibu...

1.Kisoka...
Ukiachana na timu za Dar Morogoro inafuatia kuwa na timu nyingu zilizowahi kutwaa taji la ligi kuu nazo ni Mtibwa Sugar na Mseto ukiachana na Tukuyu stars ya Mbeya hakuna mkoa uliowah kufanya hivyo hapa Tz..na kuna timu ilikuwa inaitwa reli "kiboko ya vigogo" Simba na Yanga zilikuwa hazitoki zikicheza na timu hii

Morogoro ni nyumba ya vipaji vya soka tangu zamani Kina Mohamed Msomali,Malota Soma,Zamoyoni Mogella,Charles Boniface Mkwasa(alilelewa na dada yake mtaa wa karume Morogoro tangu akiwa kijana mdogo) na wengineo magwiji wa zamani,kwa sasa wapo kina Mkude kibabage,Dickson Job,Aishi Manula,Kelvin wa Genk,Shomari Kapombe,Kibwana Shomari n.k
2.Ngumi
Hakuna asiyejua kwamba ukitoa Dar Moro ina ufalme wake katika ngumi Francis Cheka,Cosmas Cheka,Twaha Kiduku,Mandonga na wengine kibao wanatoka Moro
3.Muziki
Zamani watu dansi walikuwa wanalifuata Moro kutoka dar kuja kuwaona Cuban Marimba ya Salum abdallah na baadae Juma Kilaza na Moro Jazz ya Mbaraka Mwishehe,,Wasanii wa Moro kwa sasa ni Rich Mavoco,Jay Melody,Belle 9,Dayna,Conboi,Tundaman na wengineo hata Salam, Babu Tale wanatokea Moro

Mwandishi wa comment hii aliishi Moro kuanzia 1982-1993
 
Hata Mzizima pia inaisoma namba kwa Mologolo.
Labda Kigoma na Tabora ndio zinaweza kujibaraguzya angalao.

Lakini wajameni tumeisahau wapi Mwanza?
 
Mbona moro saivi wafanyabiashara ni wengi na waliguru wapo vijijini wengi huko matombo na mgeta. Ukienda gairo kwa wakakuguru. Wafanyabiashara wakubwa moro sio wazawa halisia wengi ni wakuja au wazamiaji. Na ukienda mfano mahenge au matombo wamejaa wachaga balaa.
 
Mwanza sina kumbukumbuku kama hata kulikuwa na band pale.
 
Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo. Hapo Morogoro wametoka akina Albert Mangwea, mbaraka mwinshehe , twaha kiduku, francis Cheka, shomari kapombe n.k. Huwezi kwa sasa Tanzania kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro View attachment 2365081
Hivi wakina Mwasongwe huu uzi wameuona kweli?..[emoji23]

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Mbona moro saivi wafanyabiashara ni wengi na waliguru wapo vijijini wengi huko matombo na mgeta. Ukienda gairo kwa wakakuguru. Wafanyabiashara wakubwa moro sio wazawa halisia wengi ni wakuja au wazamiaji. Na ukienda mfano mahenge au matombo wamejaa wachaga balaa.
Naongelea Moro ya zamani kaka miaka ya 90 kushuka chini.Maendeleo yalitakiwa yaanzie tangu zamani enzi za Shan Cinema,Mango Club n.k zamani ilikuwa wandewa wanaishi pale mjini ukitaka kuwekeza ni lazima watoe idhini wao kama hawakutaki huwezi kuishi utafanyiwa figisu sana kwao ni heri mwarabu au mhindi kuliko mchaga anayetaa kuwekeza Moro,Morogoro ilitakiwa iwe ya pili baada ya Dar sema majungu,fitna,uchawi umepinza mkoa Tanzania kuna viwanda vitanovya sukari viwili vinatoka Moro vikiwakilisha viwamda vingi vilivyokuwepo Moro enzi hizo kina Canvas,Moproco,21 century vilikufa bila sababu ya msingi..kwa sasa naona Moro inachipua sana wawekezaji wamekuwa wengi tofaut na zamani
 
Majiji mengi miaka ya tisini mkuu TADPOLE yalikuwa hovyo sana si mwanza si arusha wala mbeya. Mengi yamechangamka hivi juzi na Moro inadema dema kwasababu ya ukaribu wake na dar. Hivo wafanyabiashara wengi huenda dar kuchukua mizigo na hata biashara za jumla ni changamoto kwa Moro kwasababu wengi huenda dar. Niliwahi peleka tani 60 za karanga Moro wakasema ipo bei juu watu wakaagiza kutoka dar na dodoma. Na mimi nikashusha bei hawatakaa wanisahau wale madalali.
 
Mkoa wa Mara nao unaongoza kwa vipaji vya kupigana Vita.
 
Back
Top Bottom