Morogoro ndio mkoa uliotoa vipaji vingi Tanzania kuliko mikoa mingine.

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo.

Hapo Morogoro wametoka akina Albert Mangwea, mbaraka mwinshehe, twaha kiduku, francis Cheka, shomari kapombe n.k.

Huwezi kwa sasa Tanzania kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro

Screenshot_20220922-220459_1.jpg
 
Linapokuja suala la burudani hususani muziki, Kigoma iko sayari ya 7 kutoka sayari ya Tanzania.

Tangu huko nyuma kuna wasanii wengi nguli kama akina Bichuka n.k, hivyo vyovyote utakavyo linganisha, Kigoma hailinganishwi na mkoa wowote.

Ni sawa uilinganishe Mbeya na mkoa wowote kwenye masuala ya Ukristo(uimbaji wa Gospel, idadi ya nyumba za ibada n.k), hapo unakuwa unajilisha upepo maana ina watu ngulii haswaa kibao ambao mikoa mingine hawapo.
 
Kigoma wanavunasaba na congo

Nimekuwekea hapo juu kilwa jazz ilianzishwa mwaka gani ndio ujue kigoma imeibuka juzi juzi! Pia kulikuwa na ile bendi ya cuban huko morogoro
 
Uko sahihi,kigoma,morogoro ba tanga ndio inaongoza kwa talent
Lakini picha ya mbaraka mwinshehe sijajua inafuata nini hapo
Mbaraka alipitia morogoro jazz na super volcano zote za morogoro ila hakuwa mlugulu bali alikuwa mdoe
Kumbuka alifia kenya kwa ajali.
Sasa siku maiti yake inaletwa tanzania msafara kufika chalinze watu wakajua utakunja kulia,badala yake ukakunja kushoto,hakuzikwa morogoro
 
Unaweza ukaanzisha kitu mapema kutokana na uwepo wa nyenzo rafiki zinazokuzunguka, lakini baadae wengine wakafanya hicho ulichofanya kikawa na ubora, ufanisi na ladha ya tofauti kuliko wewe uliyeanza awali.

Mfano rahisi tu, Bob Marley na Lucky Dube wanachukuliwa kuwa ndo miamba ya Regge wa muda wote, lakini kiuhalisia Regge haikuanzia kwao.
Hivyo ndo ilivyo kwa upande wa Kigoma.
 
Aliacha shule akajiunga na moro jazz! Kigoma walikuwa na marijani rajabu naye ilikuwa ni dar kwa sana. Ila miaka hiyo muziki ulikuwa morogoro.
 
Ukimtoa marijani rajabu nitajie mwingine kutoka huko kigoma!
 
Aliacha shule akajiunga na moro jazz! Kigoma walikuwa na marijani rajabu naye ilikuwa ni dar kwa sana. Ila miaka hiyo muziki ulikuwa morogoro.
Morogoro kulikuwa na cuban marimba ya salum abdala,morogoro jazz na baadae super volcano na kwiro jazz kama sikosei.zingine huwezi kuita band bali vikundi tu,ifajara jazz,malinyi jazz,kilombero jazz nk
 
Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo. Hapo Morogoro wametoka akina Albert Mangwea, mbaraka mwinshehe , twaha kiduku, francis Cheka, shomari kapombe n.k. Huwezi kwa sasa Tanzania kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro View attachment 2365081
Ila ndiyo Mkoa uliojaa Majungu, Wivu, Fitina, Chuki kwa wasio Wazawa na Ushirikina uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom