Morogoro ni Mkoa mzuri namba Moja wa kuishi Tanzania

Morogoro ni Mkoa mzuri namba Moja wa kuishi Tanzania

Morogoro inaizidi Arusha wahamiaji.
Hao wote uliowataja wapo Morogoro,

Arusha hakuna Wandendereko, Wazaramo, Wakwere, hayo makabila nilioyataja Yana msemo usemao hawawezi kuvuka Daraja la Wami kwenda Moshi au Arusha.
Na hawawezi kuvuka Morogoro.

Ikitoka DSM Mkoa unaofuata Kwa wahamiaji wengi ni Morogoro
Arusha labda wageni WA nchi za nje
Wewe unazungumzia idadi au variety?.... hali ya mkoa kuwa na wageni wengi inakuwa reflected kwenye uchumi wake, uchumi mkubwa unavutia wageni wengi Morogoro haina lolote kulinganisha na Arusha au Mwanza
 
Wewe unazungumzia idadi au variety?.... hali ya mkoa kuwa na wageni wengi inakuwa reflected kwenye uchumi wake, uchumi mkubwa unavutia wageni wengi Morogoro haina lolote kulinganisha na Arusha au Mwanza

Uchumi mkubwa Kwa nchi za Afrika Inategemea na Serikali Kama imeamua kufanya eneo Hilo kuwa uchumi mkubwa au Laah!

Ni Kama vile unavyoona Dodoma, bila serikali hakuna jiji la Dodoma,

Serikali iliona angalau kila ukanda kuwe na Jiji Moja ndio unaona hali hiyo uionayo.
Vinginevyo Kama sio serikali amini kuwa Mji wa Kahama tuu Kasi yake ya ukuaji unazidi mpaka hiyo Arusha
 
Wewe unazungumzia idadi au variety?.... hali ya mkoa kuwa na wageni wengi inakuwa reflected kwenye uchumi wake, uchumi mkubwa unavutia wageni wengi Morogoro haina lolote kulinganisha na Arusha au Mwanza
Kiuchumi arusha haifikii hata tanga ndo ulinganishe na morogoro?
 
Naamini kibiashara ukitaka utoboe haraka

kama una mtaji wa kuanzia 20M kafungue duka la madawa ya mimea na mifugo Moro.

Ila u base hasa kwenye madawa ya mimea una weza piga sana pesa Moro.

Wana lima sana, ardhi na tabia ya nchi morogoro ina waruhusu kulima watakavyo.

kwahiyo wewe muuza madawa ya mime una weza kuwa tajiri mkubwa kwa kuwauzia madawa.


Hili wazo lina weza kumfaa mtu yeyote mwenye mtaji mzuri, hasa wa staafu, Pia hata kijana mungu aki bless ukawa na mtaji una weza lifanyia kazi hili wazo.
Mm nimekusoma Sana mkuu nilikuwa natafuta hi comment mnk nin wazo la kwenda kufungua duka Hilo uko
 
Uchumi mkubwa Kwa nchi za Afrika Inategemea na Serikali Kama imeamua kufanya eneo Hilo kuwa uchumi mkubwa au Laah!

Ni Kama vile unavyoona Dodoma, bila serikali hakuna jiji la Dodoma,

Serikali iliona angalau kila ukanda kuwe na Jiji Moja ndio unaona hali hiyo uionayo.
Vinginevyo Kama sio serikali amini kuwa Mji wa Kahama tuu Kasi yake ya ukuaji unazidi mpaka hiyo Arusha
Kwa hiyo Morogoro kuna nini kinachovuta watu wageni pale? Morogoro mjini nimeishi mji una watu wacheche tu
 
Kumbe... Morogoro kuna nini cha kuvutia wageni? Maana pale mjini tu ambapo ndio wageni wengi wanakuwa, hakuna watu
Huko vijijini mostly ni wazawa tu na wageni wachache wanaoweza kulima kilimo kikubwa
Waulize wageni wamefata nini Moro



Ni dar na morogoro tu ndo utakuta wageni wengi kuliko wenyeji

Huko arusha bado mnaongea kichaga mjini kabisaa
 
Kwema Wakuu!

Licha ya Tanzania kuwa na mikoa mingi lakini Mkoa wa Morogoro ndio mkoa namba moja kwa uzuri kwa kuishi. Nitaeleza sababu kama ifuatavyo;

1. Tabia ya nchi na Hali ya Hewa
Mkoa wa Morogoro tabia yake ya nchi na hali ya hewa ni nzuri. Hakuna joto sana wala hakuna baridi sana.

Jua lake ni la kawaida ingawaje nyakati za kiangazi huongezeka kuwa kali lakini ni afadhali zaidi kuliko jua la mikoa mingine.

Kuna msimu miwili ya mvua, masika na kiangazi ambapo hutoa fursa kwa kilimo kuvuna mara mbili kwa mwaka.

Tofauti na baadhi ya mikoa ambayo wanavuna mara moja kutokana na Baridi Kali au Ukame (joto kali).

Vumbi lake sio kali ukilinganisha na baadhi ya mikoa mingine kama Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa kipindi cha kipupwe hasa maeneo ya Mufindi.

Maeneo yenye baridi ni milimani huko Mgeta Matombo, Kibati kwenye kilele cha Mlima Muscat huko Turiani.

Tabia ya nchi na hali ya hewa inaufanya mkoa huu kuwa moja ya mikoa tegemezi kwa uzalishaji wa chakula hasa maeneo ya Ifakara, Kilosa, Mvomero na Bonde la Mlali.

2. USO wa nchi(landscape) na Ardhi yenye Rutuba.
Morogoro ni moja Kati ya Mkoa wenye uzuri wa tambarare nzuri na safu ya milima Uluguru.

Tambarare yenye udongo mzuri wenye rutuba ambao unasaidia zaidi kwenye kilimo.
Morogoro hakuna tatizo la chakula na ndio Mkoa unaolisha Mikoa inayoizunguka ikiwemo Dodoma, na Dar es Salaam.

3. Connectivity (miundombinu ya barabara)
Morogoro ndio Mkoa pekee ambao magari yote yanayoenda nchi za nje yanapitia hapo, yakitokea Dar kwenda Zambia, Malawi, South Africa, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na wakati mwingine Kenya.

Ndio mkoa pekee ambao ukitoka Mkoani huwezi kulala njiani, iwe unatoka Bukoba, Musoma, Mtwara, Songea, Rukwa au Kigoma. Ukienda Morogoro lazima ufike siku hiyohiyo.

Hii ni fursa ya kibiashara iwe kwa usafirishaji wa mizigo inayoingia au kutoka.

Morogoro ndio mkoa pekee ambao huwezi kukosa usafiri muda wowote kwenda Dar es Salaam, kwani usiku kuna mabasi yatokayo mikoa ya mbali ambayo hufika usiku wa saa tano mpaka saa saba.

Pia kuna IT na malori.

Reli ya Tazara, reli ya Kati na sasa SGR zote zimepita hapo Morogoro.

Pia Morogoro ndio Mkoa pekee uliokatikati ya majiji mawili makubwa ambayo ni Dar na Dodoma. Hii kwa watu wenye akili za mbele wanaweza jua fursa hasa kwa nyakati zijazo.

Morogoro ni mkoa wa pili baada ya Dar ambao hakuna basi kutoka mkoa wowote lisiloenda Morogoro au kupita huko.

Hii ni tofauti na mikoa mingine mfano, hakuna gari kutoka Mtwara to Mwanza,
Sumbawanga to Mwanza, hii ni tofauti na mikoa mingi.

4. Unafuu wa Maisha.
Morogoro ni moja ya Mkoa wenye unafuu mkubwa wa maisha kutokana na kuwa na chakula cha kutosha, matunda ya Aina yote.
Vyumba na nyumba za kupanga Morogoro ni nafuu na ni nzuri.

Vipo vyumba kuanzia Tsh 25 vyenye umeme na nyumba za laki na hamsini

Usafiri wa kwenda mjini sio shida na nafuu.
Viwanja na ujenzi wa nyumba ni gharama nafuu.

5. Huduma za kijamii.
Mkoa WA Morogoro unajitahidi Kwa Huduma za kijamii Kama Hospitali, shule, Huduma za kibenki, vyuo vikuu, veta na vyuo vya Kati, Makanisa na Misikiti ya kuabudia ipo.

Huduma ya maji ipo ingawaje Maeneo ya Kihonda na Mkundi bado kuna uhaba kutokana na miundombinu ya maji.

Vituo vya Mafuta ya magari,
Viwanda ambavyo Vijana wengi wamepatiwa Ajira.

Vituo vya kisasa vya Ma Mabasi na abiria, Msamvu Bus Terminal ni moja Kati ya vituo vya mabasi vikubwa Kwa hapa Tanzania baada ya kile cha Magufuli Bus Terminal cha Dar.

Viwanja vya mpira, Kama ulikuwa hujui Kwa Tanzania Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kutoa wachezaji wengi WA mpira wenye kipaji na wanaocheza katika timu kubwa hapa nchini.

Masoko ya nguo na vyakula Morogoro sio tatizo.

Vituo vya redio na televisheni sio ajabu ndio Mkoa unaoshika nafasi ya pili baada ya Dar es salaam.

6. Vivutio
Morogoro ni Mkoa namba mbili Kwa vivutio vya mbuga na hifadhi baada ya Mkoa wa Arusha, Mbuga ya Mikumi na Hifadhi kubwa zaidi Duniani ya Selous inapatikana Morogoro.
Hui ni tofauti na mikoa mingi ambayo haikubahatika kuwa hata na mbuga au hifadhi ya wanyama hata moja, achilia mbali kuwa kubwa.

7. Uwepo wa mito Mingi.
Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kuwa na vyanzo vingi vya maji hasa Mito. Hii ni tofauti na mikoa mingi Tanzania.

8. Ukarimu.
Mkoa WA Morogoro unawatu wenye ukarimu na ndio maana unaweza kumiliki Ardhi Kwa kiwango chochote unachotaka tofauti na baadhi ya mikoa mingi hapa nchi.
Sio ajabu Mkoa wa Morogoro ukakutaba na makabila karibu yote, hasa Waha, Wasukuma, Wachaga, Wapare, Wangoni, wamasai, Wahehe wabena na wakinga, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wabaya na makabila mengine mengi.

Mkoa wa Morogoro ndi9 namba mbili kwa kuwa na wageni wengi WA makabila mengine baada ya Mkoa wa Dar.

Hii ni tofauti na mikoa mingi hapa nchini ambayo mchanganyiko na makabila mengine utakuta ni mdogo.

Kwa kijana anayetaka kuanza maisha na hajui ni Mkoa gani akaanzie basi Morogoro ni moja ya mikoa ambayo unaweza ukaiweka kwenye akili yako.

Karibuni MOROGORO.
dar mpaka moro
 
Sio kweli mkuu..mkoa wa Arusha una watu wengi sana kutoka Kilimanjaro, wamekaba hadi huko vijijini. Pia watu kutoka Singida na Manyara

Mwanza nako kuna watu wengi sana kutoka mkoa wa Mara, Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora

Morogoro haina watu wengi pale mjini, na huko vijijini mostly ni wenyeji tu
Wewe nawe vipi. Watu wa Geita kabla ya 2012 Mwanza ilikuwa ndio mkoa wao, utasemaje kwamba ni wageni hapo Mwanza ?
 
Waulize wageni wamefata nini Moro



Ni dar na morogoro tu ndo utakuta wageni wengi kuliko wenyeji

Huko arusha bado mnaongea kichaga mjini kabisaa
Kama unataka kufurahisha JF hongera ila huwezi kulinganisha Arusha na Hiyo Morogoro yako. Mji kasoro bahari bado sana.
 
Kama unataka kufurahisha JF hongera ila huwezi kulinganisha Arusha na Hiyo Morogoro yako. Mji kasoro bahari bado sana.
Morogoro ni manispaa hata kimaendeleo mmetuzidi vitu vichache ambapo kwa kasi hii ya ukuaji WA mji ndani ya miaka miwili tutakuwa tumewazidi
 
Back
Top Bottom