Pia ndiyo mkoa pekee ambao watu wake wanadanganyika kirahsi mno, maji ni changamoto kubwa aeneo mengi ya mji, Kasanga, Lukobe, Lukuyu, Mkundi, Makunganya, Kihonda, Azimio, Kitungwa Tubuyu, Nanenane, n.k huko kote hakuna maji!
Ukipita maeneo ya mafiga, Chamwino, Mazimbu, Misufini, Kingo huko maji yanatoka kwa wiki haizidi mara tatu!
Ni eneo mji uliolala sana kisiasa, ni manispaa pekee ambayo mpaka leo pamoja changamoto zote hizo za maji na miundombinu mibovu ya Barabara ila mbunge wanayemjua ni mmoja tu, ABOOD!
Baraza la madiwani kwa miaka yote, limejaa CCM pekee, hii imerahisha ufujaji mkubwa wa pesa za walipa kodi kwa kujipigia wanavyotaka!
Wanachofurahia kutoka kwa mbunge wao ni Gari (bus) ya kuzikia wanapokufa, hapo wanakenua meno yote nje, na kuona ameajali sanaaa!
Kwa habari ya chakula nakubaliana na wewe kabisa, Morogoro ni pazuri...