Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukistaafu nn? Bill gate ana miaka 66 haafikirii neno kustaafu, bilionea namba 5 duniani warren buffet ana miaka 90 hajui neno kustaafu lipoje.Nafikiri nikistaafu nitaishi Morogoro, napapenda tu sijui kwanini.
I ant NO Bill Gate, I ain't no Warren Buffet.Ukistaafu nn? Bill gate ana miaka 66 haafikirii neno kustaafu, bilionea namba 5 duniani warren buffet ana miaka 90 hajui neno kustaafu lipoje
Huku Mwalimu wa Shule ya Msingi Majengo anakuambia akistaafu..............
Nenda taratibu naona unachanganya mambo.Yawezekana Moro bado huijui vizuri Mzumbe ipo pembezoni kabisa Wilaya ya Mvomero , ina impact ndogo Sana kwa Moro town . Hebu taja mkoa wako hapa nisijekuwa nabishana na mlughalugha wa huko sitimbi
Kufika Mwanza siyo hoja. Zitaje sifa ili kufananisha na Morogoro.Mwanza umefika?
Katikati kuna faida sana na kuna hasara zake.Mkoa unaongoza kwa ukimwi huu
Hivi Mvuha siyo pale makao makuu ya Morogoro Vijijini? Au nimekosea jina?Mwenda pia, wale wa mwanamtandeni, kingalu, hgg nk wote nawapa salamu.
wazee wa rubasazi,kolelo,lukange,duthumi,mngazi, bwakira, gomelo kisaki,mtamba, mvuha, magogoni turo wote nawapeni salamu zangu.
Kwahiyo point yako ni kwamba Mzumbe Kama ikihamishwa hapa Moro Basi Moro itayumba kwasababu ya shopping za wanachuo wa Mzumbe? Nikajua hoja yako inamaana kumbe zero kabisa.Nenda taratibu naona unachanganya mambo.
MZUMBE ina impact ndogo kwa kuwa iko mbali na mji? Shopping zao wanafanyia Mikumi?
Swala la mkoa wangu nikiliingiza hapa tutachanganya mada. Mkoa unaochambuliwa ni Morogoro.
Kuna Ulaya pia mkuu.Kuna Mbingu pia
Kuna Nazareti pia mkuu.Kuna Mbingu pia
Inaanza lini ndugu??SGR ikianza kazi hili litawezekana.
Sina uhakika inaanza lini.Inaanza lini ndugu??
angalia kwanza idadi ya wachaga, ukiona wapo wengi, huo mkoa ni mzuri kuishi. hata hizi kazi mnaomba, angalia secta hiyo ina wachaga wengi? ukiona wapo, ng'ang'ania, secta hiyo ina pesa.Kwema Wakuu!
Licha ya Tanzania kuwa na mikoa mingi lakini Mkoa wa Morogoro ndio mkoa namba moja kwa uzuri kwa kuishi. Nitaeleza sababu kama ifuatavyo;
1. Tabia ya nchi na Hali ya Hewa
Mkoa wa Morogoro tabia yake ya nchi na hali ya hewa ni nzuri. Hakuna joto sana wala hakuna baridi sana.
Jua lake ni la kawaida ingawaje nyakati za kiangazi huongezeka kuwa kali lakini ni afadhali zaidi kuliko jua la mikoa mingine.
Kuna msimu miwili ya mvua, masika na kiangazi ambapo hutoa fursa kwa kilimo kuvuna mara mbili kwa mwaka.
Tofauti na baadhi ya mikoa ambayo wanavuna mara moja kutokana na Baridi Kali au Ukame (joto kali).
Vumbi lake sio kali ukilinganisha na baadhi ya mikoa mingine kama Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa kipindi cha kipupwe hasa maeneo ya Mufindi.
Maeneo yenye baridi ni milimani huko Mgeta Matombo, Kibati kwenye kilele cha Mlima Muscat huko Turiani.
Tabia ya nchi na hali ya hewa inaufanya mkoa huu kuwa moja ya mikoa tegemezi kwa uzalishaji wa chakula hasa maeneo ya Ifakara, Kilosa, Mvomero na Bonde la Mlali.
2. USO wa nchi(landscape) na Ardhi yenye Rutuba.
Morogoro ni moja Kati ya Mkoa wenye uzuri wa tambarare nzuri na safu ya milima Uluguru.
Tambarare yenye udongo mzuri wenye rutuba ambao unasaidia zaidi kwenye kilimo.
Morogoro hakuna tatizo la chakula na ndio Mkoa unaolisha Mikoa inayoizunguka ikiwemo Dodoma, na Dar es Salaam.
3. Connectivity (miundombinu ya barabara)
Morogoro ndio Mkoa pekee ambao magari yote yanayoenda nchi za nje yanapitia hapo, yakitokea Dar kwenda Zambia, Malawi, South Africa, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na wakati mwingine Kenya.
Ndio mkoa pekee ambao ukitoka Mkoani huwezi kulala njiani, iwe unatoka Bukoba, Musoma, Mtwara, Songea, Rukwa au Kigoma. Ukienda Morogoro lazima ufike siku hiyohiyo.
Hii ni fursa ya kibiashara iwe kwa usafirishaji wa mizigo inayoingia au kutoka.
Morogoro ndio mkoa pekee ambao huwezi kukosa usafiri muda wowote kwenda Dar es Salaam, kwani usiku kuna mabasi yatokayo mikoa ya mbali ambayo hufika usiku wa saa tano mpaka saa saba.
Pia kuna IT na malori.
Reli ya Tazara, reli ya Kati na sasa SGR zote zimepita hapo Morogoro.
Pia Morogoro ndio Mkoa pekee uliokatikati ya majiji mawili makubwa ambayo ni Dar na Dodoma. Hii kwa watu wenye akili za mbele wanaweza jua fursa hasa kwa nyakati zijazo.
Morogoro ni mkoa wa pili baada ya Dar ambao hakuna basi kutoka mkoa wowote lisiloenda Morogoro au kupita huko.
Hii ni tofauti na mikoa mingine mfano, hakuna gari kutoka Mtwara to Mwanza,
Sumbawanga to Mwanza, hii ni tofauti na mikoa mingi.
4. Unafuu wa Maisha.
Morogoro ni moja ya Mkoa wenye unafuu mkubwa wa maisha kutokana na kuwa na chakula cha kutosha, matunda ya Aina yote.
Vyumba na nyumba za kupanga Morogoro ni nafuu na ni nzuri.
Vipo vyumba kuanzia Tsh 25 vyenye umeme na nyumba za laki na hamsini
Usafiri wa kwenda mjini sio shida na nafuu.
Viwanja na ujenzi wa nyumba ni gharama nafuu.
5. Huduma za kijamii.
Mkoa WA Morogoro unajitahidi Kwa Huduma za kijamii Kama Hospitali, shule, Huduma za kibenki, vyuo vikuu, veta na vyuo vya Kati, Makanisa na Misikiti ya kuabudia ipo.
Huduma ya maji ipo ingawaje Maeneo ya Kihonda na Mkundi bado kuna uhaba kutokana na miundombinu ya maji.
Vituo vya Mafuta ya magari,
Viwanda ambavyo Vijana wengi wamepatiwa Ajira.
Vituo vya kisasa vya Ma Mabasi na abiria, Msamvu Bus Terminal ni moja Kati ya vituo vya mabasi vikubwa Kwa hapa Tanzania baada ya kile cha Magufuli Bus Terminal cha Dar.
Viwanja vya mpira, Kama ulikuwa hujui Kwa Tanzania Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kutoa wachezaji wengi WA mpira wenye kipaji na wanaocheza katika timu kubwa hapa nchini.
Masoko ya nguo na vyakula Morogoro sio tatizo.
Vituo vya redio na televisheni sio ajabu ndio Mkoa unaoshika nafasi ya pili baada ya Dar es salaam.
6. Vivutio
Morogoro ni Mkoa namba mbili Kwa vivutio vya mbuga na hifadhi baada ya Mkoa wa Arusha, Mbuga ya Mikumi na Hifadhi kubwa zaidi Duniani ya Selous inapatikana Morogoro.
Hui ni tofauti na mikoa mingi ambayo haikubahatika kuwa hata na mbuga au hifadhi ya wanyama hata moja, achilia mbali kuwa kubwa.
7. Uwepo wa mito Mingi.
Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kuwa na vyanzo vingi vya maji hasa Mito. Hii ni tofauti na mikoa mingi Tanzania.
8. Ukarimu.
Mkoa WA Morogoro unawatu wenye ukarimu na ndio maana unaweza kumiliki Ardhi Kwa kiwango chochote unachotaka tofauti na baadhi ya mikoa mingi hapa nchi.
Sio ajabu Mkoa wa Morogoro ukakutaba na makabila karibu yote, hasa Waha, Wasukuma, Wachaga, Wapare, Wangoni, wamasai, Wahehe wabena na wakinga, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wabaya na makabila mengine mengi.
Mkoa wa Morogoro ndi9 namba mbili kwa kuwa na wageni wengi WA makabila mengine baada ya Mkoa wa Dar.
Hii ni tofauti na mikoa mingi hapa nchini ambayo mchanganyiko na makabila mengine utakuta ni mdogo.
Kwa kijana anayetaka kuanza maisha na hajui ni Mkoa gani akaanzie basi Morogoro ni moja ya mikoa ambayo unaweza ukaiweka kwenye akili yako.
Karibuni MOROGORO.
Nafikiri mtoa mada hana nia ya kukupinga ila ameandika alichokiona/anachokifahamTatizo la maji Morogoro ni la mitaa utabisha hili labda kama ulienda mara moja tu na kurudi lakini sisi tulioishi kwa muda mrefu pale tunakuthibitishia tatizo la maji Morogoro ni la mitaa tu..Uzuri zaidi mimi kwa muda wote wa maisha yangu nimeishi hii mikoa miwili ya Dar na Morogoro,usichokijua chanzo cha maji Morogoro sio bwawa la mindu tu bwawa la Mindu linahudumia tu baadhi ya maeneo kwa mfano mimi niliishi Sabasaba tulihudumiwa na bwawa la Mindu na hatukuwahi kuona shida ya maji kwani maji ya bomba ilikuwa kila siku yanatoka halafu kuna wale ambao wanahudumiwa na maji kutoka mto Ruvu unaohudumia Dar pia kwa mfano maeneo kama bigwa,Kigurunyembe,na Kilakala wanahudumiwa na mto Ruvu hawa ndio kidogo wanaexperience shida ya maji kutokana na mto ruvu sometimes kupungua kina kumbuka unahudumia Dar,na maeneo ya pwani pia..Halafu kuna wale ambao wanaoishi sehemu za makao mapya kama Mkundi,Lukobe na Makunganya hawa nakiri wazi kwamba wanaexperience shida ya maji kama ilivyokuwa kwa maeneo mapya ya jiji la Dar ambao nao pia maji ya bomba wanayasikia kwenye redio
Ndio hapo hapo kwa sasaHivi Mvuha siyo pale makao makuu ya Morogoro Vijijini? Au nimekosea jina?
Mwaka wa 7 huu nipo morogoro na sijawahi kuugua huo ugonjwa, kuugua huo ugonjwa ni umakini wako tu wa kutumia maji, karibu moro, niko KolaMorogoro hapafai na siyo pa kukimbilia kuishi ule mkoa kupata typhoid ni kugusa tu