Morogoro ni Mkoa mzuri namba Moja wa kuishi Tanzania

Comments za humu ni za watu wa Dar. Tuliosomea Moro tunajua shida za Maji na typhoid. Ukihamisha SUA na MZUMBE ujue umeiua Morogoro.
Yawezekana Moro bado huijui vizuri Mzumbe ipo pembezoni kabisa Wilaya ya Mvomero , ina impact ndogo Sana kwa Moro town . Hebu taja mkoa wako hapa nisijekuwa nabishana na mlughalugha wa huko sitimbi
 
Morogoro ndio gateway place nikichoka na mihangaiko ya dar, sometimes naamua tu natoka dar asubuhi nafika asubuhi Moro, nakula na kunywa naweza nikalala au nikarudi usiku kuja dar na nina enjoy sana. It's a blessed city
Makao makuu ya nchi yalitakiwa kuwa morogoro,
 
Kwema Wakuu!

Licha ya Tanzania kuwa na Mikoa mingi lakini Mkoa WA Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa uzuri Kwa kuishi. Nitaeleza sababu Kama ifuatavyo;

1. Tabia ya nchi na Hali ya Hewa.
Mkoa wa Morogoro tabia yake ya nchi na Hali ya hewa ni nzuri. Hakuna joto Sana wala hakuna baridi Sana.
Jua lake ni lakawaida ingawaje nyakati za kiangazi huongezeka kuwa Kali lakini ni afadhali zaidi kuliko jua la mikoa mingine.

Kuna msimu miwili ya Mvua, masika na kiangazi ambapo hutoa fursa Kwa kilimo kuvuna mara mbili Kwa Mwaka.
Tofauti na baadhi ya mikoa ambayo wanavuna mara moja kutokana na Baridi Kali au Ukame(joto Kali).

Vumbi lake sio Kali ukilinganisha na baadhi ya mikoa mingine Kama Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa kipindi cha kipupwe hasa Maeneo ya Mufindi.

Maeneo yenye baridi ni milimani huko Mgeta matombo, Kibati kwenye kilele cha mlima Muscat huko Turiani,

Tabia ya nchi na Hali ya hewa inaufanya Mkoa huu kuwa moja ya mikoa tegemezi Kwa uzalishaji WA chakula hasa Maeneo ya Ifakara, kilosa, Mvomero, Na bonde la Mlali.

2. USO wa nchi(landscape) na Ardhi yenye Rutuba.
Morogoro ni moja Kati ya Mkoa wenye uzuri wa tambarare nzuri na Safu ya milima Uluguru.
Tambarare yenye udongo mzuri wenye rutuba ambao unasaidia zaidi kwenye kilimo.
Morogoro hakuna tatizo la chakula na ndio Mkoa unaolisha Mikoa inayoizunguka ikiwemo Dodoma, na Dar es salaam.

3. Connectivity (miundombinu ya barabara)
Morogoro ndio Mkoa pekee ambao Magari yote yanayoenda nchi za nje yanapitia hapo, yakitokea DAR es salaam kwenda Zambia, Malawi, South Afrika, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na wakati mwingine Kenya.

Ndio Mkoa pekee ambao ukitoka Mkoani huwezi kulala njiani, iwe unatoka Bukoba, Musoma, Mtwara, Songea, Rukwa au Kigoma. Ukienda Morogoro lazima ufike siku hiyohiyo,

Hii ni fursa ya kibiashara iwe Kwa usafirishaji wa mizigo inayoingia au kutoka.

Morogoro ndio Mkoa pekee ambao huwezi kukosa Usafiri muda wowote kwenda Dar es salaam, kwani usiku kuna Mabasi yatokayo mikoa ya mbali ambayo hufika usiku wa saa tano mpaka saa Saba.
Pia kuna IT na malori.

Reli ya Tazara, reli ya Kati, na sasa SGR zote zimepita hapo Morogoro.

Pia Morogoro ndio Mkoa pekee uliokatikati ya Majiji mawili makubwa ambayo ni Dar es salaam na Dodoma. Hii Kwa watu wenye akili za mbele wanaweza jua fursa hasa Kwa nyakati zijazo.

Morogoro ni Mkoa WA pili baada ya Dar ambao hakuna Basi kutoka Mkoa wowote lisiloenda Morogoro au kupita huko.

Hii ni tofauti na mikoa mingine Mfano, Hakuna Gari kutoka Mtwara to Mwanza,
Sumbawanga to Mwanza,
Hii ni tofauti na mikoa mingi.

4. Unafuu wa Maisha.
Morogoro ni moja ya Mkoa wenye unafuu mkubwa wa maisha kutokana na kuwa na chakula cha kutosha, matunda ya Aina yote.
Vyumba na nyumba za kupanga Morogoro ni nafuu na ni nzuri.
Vipo vyumba kuanzia Tsh 25 vyenye umeme na nyumba za laki na hamsini,

Usafiri wa kwenda mjini sio shida na nafuu.
Viwanja na ujenzi wa nyumba ni gharama nafuu.

5. Huduma za kijamii.
Mkoa WA Morogoro unajitahidi Kwa Huduma za kijamii Kama Hospitali, shule, Huduma za kibenki, vyuo vikuu, veta na vyuo vya Kati, Makanisa na Misikiti ya kuabudia ipo.
Huduma ya maji ipo ingawaje Maeneo ya Kihonda na Mkundi bado kuna uhaba kutokana na miundombinu ya maji.

Vituo vya Mafuta ya magari,
Viwanda ambavyo Vijana wengi wamepatiwa Ajira,
Vituo vya kisasa vya Ma Mabasi na abiria, Msamvu Bus Terminal ni moja Kati ya vituo vya mabasi vikubwa Kwa hapa Tanzania baada ya kile cha Magufuli Bus terminal cha Dar es salaam.

Viwanja vya mpira, Kama ulikuwa hujui Kwa Tanzania Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kutoa wachezaji wengi WA mpira wenye kipaji na wanaocheza katika timu kubwa hapa nchini.

Masoko ya nguo na vyakula Morogoro sio tatizo.

Vituo vya redio na televisheni sio ajabu ndio Mkoa unaoshika nafasi ya pili baada ya Dar es salaam.

6. Vivutio
Morogoro ni Mkoa namba mbili Kwa vivutio vya mbuga na hifadhi baada ya Mkoa wa Arusha, Mbuga ya Mikumi na Hifadhi kubwa zaidi Duniani ya Selous inapatikana Morogoro.
Hui ni tofauti na mikoa mingi ambayo haikubahatika kuwa hata na mbuga au hifadhi ya wanyama hata moja, achilia mbali kuwa kubwa.

7. Uwepo wa mito Mingi.
Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kuwa na vyanzo vingi vya maji hasa Mito. Hii ni tofauti na mikoa mingi Tanzania.

8. Ukarimu.
Mkoa WA Morogoro unawatu wenye ukarimu na ndio maana unaweza kumiliki Ardhi Kwa kiwango chochote unachotaka tofauti na baadhi ya mikoa mingi hapa nchi.
Sio ajabu Mkoa wa Morogoro ukakutaba na makabila karibu yote, hasa Waha, Wasukuma, Wachaga, Wapare, Wangoni, wamasai, Wahehe wabena na wakinga, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wabaya na makabila mengine mengi.

Mkoa WA Morogoro ndio Mkoa namba mbili Kwa kuwa na wageni wengi WA makabila mengine baada ya Mkoa WA DAR.

Hii ni tofauti na mikoa mingi hapa nchini ambayo mchanganyiko na makabila mengine utakuta ni mdogo.

Kwa kijana anayetaka kuanza maisha na hajui ni Mkoa gani akaanzie basi Morogoro ni moja ya mikoa ambayo unaweza ukaiweka kwenye Akili yako.

Karibuni MOROGORO.
Huu ndio mkoa wa hovyo kabisa nchini Tanzania maana maji ya kunywa ya mkoa huu yamejaa madini ya ulanga na kusababisha watu wengi wasiozaliwa mkoa huu kuugua magonjwa ya tumbo na wengi hupoteza maisha. Huu mkoa ni wa kingese sana.
 
Morogoro kilichoiponza na kuwa underated ni vile zamani wazawa walikuwa wanapiga vita wageni kuwekeza hapo ndio maana Shughuli nyingi za maendeleo zikasimama na mji ukawa wa hadhi ya kawaida tofauti na ilivyokuwa miaka ya 60 na 70 mpaka early 80 cha kuongezea kuhusu Morogoro
1.Ni moja ya mkoa wenye idadi kubwa ya Taasisi za elimu ya juu tena zile hot kwa mfano Tunajua SUA,MZUMBE,JORDAN UNIVERSITY,MUM UNIVERSITY vyote vipo Morogoro hapo bado hatujataja vyuo vya kati kama LITI na ST Francis
2.Kiburudani na michezo tunajua kwamba Moro is home for talents Diamond platinumz kazungukwa na mamaster mind ambao ni wenyeji wa Morogoro nao ni Salam na Babu Tale,hapo hatujataja wasanii wa sasa lakini zamani Morogoro kulikuwa na Diamond Platinumz wa enzi hizo nadhani wote tunamjua anaitwa Mbaraka Mwishehe pia nani ambaye haijui CUBAN MARIMBA? bendi hii pia ilikuwa na maskani Morogoro zamani ilikuwa watu weekend wanatoka dar wanaenda kuspend Morogoro tuje kwenye michezo kuna timu ilikuwa inaitwa Mseto ndio timu ya kwanza nje ya Dar es salaam kutwaa taji la ligi kuu Bara kabla ya baadae mtibwa kuja kufanya hivyo Kimsingi Mtibwa,Tukuyu stars(Mbeya) na Mseto ndio timu pekee kutoka nje ya mkoa wa Dar kutwaa kombe la ligi kuu,Morogoro ni nyumbani kwa Kina Charles Boniface Mkwassa(japokuwa kiasili si wa morogoro),Mohammed Msomali,Malota Soma hao ni wachezaji wa zamani sitowataja wachezaji wa sasa ambao wamejazana kwenye club za soka za ligi kuu bara
3.Viwanda,hapa Tanzania tuna viwanda visivyozidi vitano vya Sukari na fun fact nusu ya viwanda hivyo(viwili) Kilombero Sugar na Mtibwa sugar vipo Morogoro asante
ROBERT HERIEL
Vyuo vya maana hapo ni viwili tu, SUA na Mzumbe, hivyo vingine ni zaidi ya vyuo vya Kata wanachuo wanachapwa bakora
 
Kwema Wakuu!

Licha ya Tanzania kuwa na Mikoa mingi lakini Mkoa WA Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa uzuri Kwa kuishi. Nitaeleza sababu Kama ifuatavyo;

1. Tabia ya nchi na Hali ya Hewa.
Mkoa wa Morogoro tabia yake ya nchi na Hali ya hewa ni nzuri. Hakuna joto Sana wala hakuna baridi Sana.
Jua lake ni lakawaida ingawaje nyakati za kiangazi huongezeka kuwa Kali lakini ni afadhali zaidi kuliko jua la mikoa mingine.

Kuna msimu miwili ya Mvua, masika na kiangazi ambapo hutoa fursa Kwa kilimo kuvuna mara mbili Kwa Mwaka.
Tofauti na baadhi ya mikoa ambayo wanavuna mara moja kutokana na Baridi Kali au Ukame(joto Kali).

Vumbi lake sio Kali ukilinganisha na baadhi ya mikoa mingine Kama Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa kipindi cha kipupwe hasa Maeneo ya Mufindi.

Maeneo yenye baridi ni milimani huko Mgeta matombo, Kibati kwenye kilele cha mlima Muscat huko Turiani,

Tabia ya nchi na Hali ya hewa inaufanya Mkoa huu kuwa moja ya mikoa tegemezi Kwa uzalishaji WA chakula hasa Maeneo ya Ifakara, kilosa, Mvomero, Na bonde la Mlali.

2. USO wa nchi(landscape) na Ardhi yenye Rutuba.
Morogoro ni moja Kati ya Mkoa wenye uzuri wa tambarare nzuri na Safu ya milima Uluguru.
Tambarare yenye udongo mzuri wenye rutuba ambao unasaidia zaidi kwenye kilimo.
Morogoro hakuna tatizo la chakula na ndio Mkoa unaolisha Mikoa inayoizunguka ikiwemo Dodoma, na Dar es salaam.

3. Connectivity (miundombinu ya barabara)
Morogoro ndio Mkoa pekee ambao Magari yote yanayoenda nchi za nje yanapitia hapo, yakitokea DAR es salaam kwenda Zambia, Malawi, South Afrika, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na wakati mwingine Kenya.

Ndio Mkoa pekee ambao ukitoka Mkoani huwezi kulala njiani, iwe unatoka Bukoba, Musoma, Mtwara, Songea, Rukwa au Kigoma. Ukienda Morogoro lazima ufike siku hiyohiyo,

Hii ni fursa ya kibiashara iwe Kwa usafirishaji wa mizigo inayoingia au kutoka.

Morogoro ndio Mkoa pekee ambao huwezi kukosa Usafiri muda wowote kwenda Dar es salaam, kwani usiku kuna Mabasi yatokayo mikoa ya mbali ambayo hufika usiku wa saa tano mpaka saa Saba.
Pia kuna IT na malori.

Reli ya Tazara, reli ya Kati, na sasa SGR zote zimepita hapo Morogoro.

Pia Morogoro ndio Mkoa pekee uliokatikati ya Majiji mawili makubwa ambayo ni Dar es salaam na Dodoma. Hii Kwa watu wenye akili za mbele wanaweza jua fursa hasa Kwa nyakati zijazo.

Morogoro ni Mkoa WA pili baada ya Dar ambao hakuna Basi kutoka Mkoa wowote lisiloenda Morogoro au kupita huko.

Hii ni tofauti na mikoa mingine Mfano, Hakuna Gari kutoka Mtwara to Mwanza,
Sumbawanga to Mwanza,
Hii ni tofauti na mikoa mingi.

4. Unafuu wa Maisha.
Morogoro ni moja ya Mkoa wenye unafuu mkubwa wa maisha kutokana na kuwa na chakula cha kutosha, matunda ya Aina yote.
Vyumba na nyumba za kupanga Morogoro ni nafuu na ni nzuri.
Vipo vyumba kuanzia Tsh 25 vyenye umeme na nyumba za laki na hamsini,

Usafiri wa kwenda mjini sio shida na nafuu.
Viwanja na ujenzi wa nyumba ni gharama nafuu.

5. Huduma za kijamii.
Mkoa WA Morogoro unajitahidi Kwa Huduma za kijamii Kama Hospitali, shule, Huduma za kibenki, vyuo vikuu, veta na vyuo vya Kati, Makanisa na Misikiti ya kuabudia ipo.
Huduma ya maji ipo ingawaje Maeneo ya Kihonda na Mkundi bado kuna uhaba kutokana na miundombinu ya maji.

Vituo vya Mafuta ya magari,
Viwanda ambavyo Vijana wengi wamepatiwa Ajira,
Vituo vya kisasa vya Ma Mabasi na abiria, Msamvu Bus Terminal ni moja Kati ya vituo vya mabasi vikubwa Kwa hapa Tanzania baada ya kile cha Magufuli Bus terminal cha Dar es salaam.

Viwanja vya mpira, Kama ulikuwa hujui Kwa Tanzania Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kutoa wachezaji wengi WA mpira wenye kipaji na wanaocheza katika timu kubwa hapa nchini.

Masoko ya nguo na vyakula Morogoro sio tatizo.

Vituo vya redio na televisheni sio ajabu ndio Mkoa unaoshika nafasi ya pili baada ya Dar es salaam.

6. Vivutio
Morogoro ni Mkoa namba mbili Kwa vivutio vya mbuga na hifadhi baada ya Mkoa wa Arusha, Mbuga ya Mikumi na Hifadhi kubwa zaidi Duniani ya Selous inapatikana Morogoro.
Hui ni tofauti na mikoa mingi ambayo haikubahatika kuwa hata na mbuga au hifadhi ya wanyama hata moja, achilia mbali kuwa kubwa.

7. Uwepo wa mito Mingi.
Morogoro ndio Mkoa namba moja Kwa kuwa na vyanzo vingi vya maji hasa Mito. Hii ni tofauti na mikoa mingi Tanzania.

8. Ukarimu.
Mkoa WA Morogoro unawatu wenye ukarimu na ndio maana unaweza kumiliki Ardhi Kwa kiwango chochote unachotaka tofauti na baadhi ya mikoa mingi hapa nchi.
Sio ajabu Mkoa wa Morogoro ukakutaba na makabila karibu yote, hasa Waha, Wasukuma, Wachaga, Wapare, Wangoni, wamasai, Wahehe wabena na wakinga, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wabaya na makabila mengine mengi.

Mkoa WA Morogoro ndio Mkoa namba mbili Kwa kuwa na wageni wengi WA makabila mengine baada ya Mkoa WA DAR.

Hii ni tofauti na mikoa mingi hapa nchini ambayo mchanganyiko na makabila mengine utakuta ni mdogo.

Kwa kijana anayetaka kuanza maisha na hajui ni Mkoa gani akaanzie basi Morogoro ni moja ya mikoa ambayo unaweza ukaiweka kwenye Akili yako.

Karibuni MOROGORO.
ila namba 7 sidhani kama ni sahihi, huu mkoa maji yake hata sio ya kuringia na maji ya mito hayatumiki kwa huduma za kawaida kama kunywa na kuoga yako full typod. ukisema mkoa wentr mito nadhani ni kagera na moshi huko hawana shida wale ya maji kwa moro hapa hapana hapana nakataa.mengine yote uliyoelezea uko sawa mia mia ni mkoa mzuri sana na sasa majengo makubwa marrfu yanaanza kujengwa soon linakuwa jiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule pamezidi

Pamezidi sio kidogo inafika time hadi mabomba yanatoa maji machafu

Chakula, hali ya hewa, location na muonekano wa asili ni plus na kama mtu ana ndoto za kufanya kilimo, labda nuvu zimuishie mwenyewe

Ila Morogoro ni mini dar, watu wake na wa dar wametofautiana padogo sana maana hadi uswahili wa dar, moro umeshamiri kiasi kwamba mtu wa dar hawezi struggle kujichanganya

Overall bado sijaona mji ambao upo well balanced kama mwanza. Nimefika pengi Ila hapa ni pazuri zaidi kuishi
 
Shida ya maji ni tatizo mtambuka Tanzania yote hata Dar mimi nimeishi mikoa yote miwili tangu udogo wangu lakini nikiri shida ya maji ya Morogoro ni afadhali ile ya Dar,tuulize sisi tuliokulia mitaa ya kuanzia Kimara Ubungo,Sinza,Tandale ilikuwa ni kawaida sana maji kukaa wiki mbili bila ya kutoka...watu wa maeneo ya Kivile,kitunda na Pugu hawajui maji ya bomba yanafananaje..incase you dont know maji yanayonyweka Dar ni ya mto Ruvu ambayo chanzo chake ni milima ya Uluguru Morogoro
Morogoro tatizo la maji sio la mitaa flani ni tatizo la mji mzima

Dar kuna mitaa ina shida ya maji Ila Morogoro labda uvune maji ya mvua Ila kama unategemea maji ya hilo bwawa sahau.

Nilishuhudia maji machafu yanatoka bombani nikapanyooshea mikono
 
hapana hapana wa dar wamelegea saaaaaaana, na wanrembua mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukikaa na kijana wa dar na Morogoro, walichotofautiana ni location, ukikaa na mluguru na mzaramo walichotofautiana ni ukulima na uchakarikaji wa waluguru Ila vingine vyote ni sawa. Yaani nikimtoa mzaramo sijaona kabila lingine wanapenda ngoma kuliko waluguru, msimu wa mavuno hata birthday ya mtoto wataitisha ngoma ikeshe 😁😁
 
Back
Top Bottom