Morogoro ni Mkoa mzuri namba Moja wa kuishi Tanzania



Asante sana mkuu kwa Tarifa hii.
umetutajia maeneo mawili yenye changamoto ya kaji katika mkoa wa Morogoro ambayo ni kihonda na mkundi .
Swali langu kwa uzoefu wako ni maeneo gani ambapo naweza pata nyumba ya kupanga kwa bei rafiki (bei nzuri) na kuna uhakika wa huduma muhimu haswa maji na shule nzuri (za msingi za serikali) kwaajili ya elimu kwa vijana pia uhakika wa usafiri wa uma kufika katikati ya mji.

Asante.
 
Bigwa Kila kitu safi changamoto usafiri tu na tope wakati wa mvua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikifika miaka 60 mda utaobakia nitaenda kumalizia Morogoro au Bukoba-Kagera.
 
Huu mkoa tumepambana sana
Kweli fursa ziko vijijini huko porini

Ova
 
Safi sana mkuu nilikuwa nataka kujua bei za vyumba na frem kwa morogoro mjini na kuzunguka mitaa yake
 
Morogoro ndiyo mkoa pekee ambapo mtu yoyote ambaye hakai Dar akifika atavutiwa kukaa pale.

Morogoro ndiyo mkoa pekee wenye wapiga debe wenye customer care kubwa kuliko ofisi yoyote nchini.

Ukishuka kwenye gari unapokelewa kwa salamu, unabebewa begi, unasindikizwa mpaka lodge na unapelekwa sehemu ya chakula, asubuhi tena anakufuata anakubebea kila kitu tena mpaka kwenye gari anakuonyesha siti kisha anakutakia safari njema. Wanashangaza sana
 
Wilaya gani ya Morogoro unapendekeza kwa mgeni kuanzia maisha kati ya Ifakara,Kilosa,Kilombero na nyinginezo yenye unafuu wa.shida ya maji

Wilaya karibu zote Moro zina fursa tu zakutosha anzia ifakara na kuendelea
 
Wilaya karibu zote Moro zina fursa tu zakutosha anzia ifakara na kuendelea
Nimeona wengi wanasema kuna changamoto ya maji,hivyo najaribu kuangalia yenye unafuu wa upatikanaji maji.....binafsi nilipenda nianze kilosa au ifakara japo sijawahi fika
 
Sijawahi kupenda kuishi miji isiyo kuwa na bahari au ziwa..napenda sana beaches na samaki wale fresh.

Kuhusu moro wanamiwa mitamu sana na milaini huwa nikipita msamvu lazima nichukue yakutosha kula na kupelekea familia.

Uzuri wa moro ni upatikanaji wa chakula kwa wingi.

Makazi huniondoi dsm na kanda ya ziwa especially mwanza na bkb.

#MaendeleoHayanaChama
 

Karibu Sana MKUU.
Mji kasoro bahari
 
Nikiwa kama Mwana Moro, nasema asante sana kwa mkoa wetu kupata nafasi ya kuzungumziwa JF...

Karibu Moro......... Wenyewe tunakula ugali na nguruka, na kachumbari. Siku imepitaaaaaaaaaaa
 
Nimekaa sana hapo sema moro imebadilika sana watani zangu mnachoma sana moto milimani ndo maana panaharibika ..moro ilikua moro kweli asubuhi ukungu km mko rusia mlima kuja kuuona vizuri ni mchana maana ukungu unaifunika milima harafu ukionekana maji yanatililika milimani dah....one of the best enjoyment hua haitoki kichwani ..kwa swala la misosi hapo hela yako tu utakula kuanzia matunda,samaki sema sio wengi km wanavyooagiza nguruka,nyama mpaka yule haram kwa moro utakimbia mwenyewe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…