Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Analazimisha kupendwa, ukute yeye ndio chanzo cha mume wake kwenda kuoa mwanamke mwingine. Hakuna mwanaume anaeweza Acha mke mwema. Hadi mwanaume kuoa mke mwingine shida ni kasoro ya mke wa kwanza kashindwa kujua wajibu wake ni nini.
 
Profesa wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Christopher Kasanga na mwenzake Linael Makundi mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Mandela mkoani hapo wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro kwa shitaka la madai ya Ugoni dhidi ya malalamikaji Matrida Sigaret.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo jana, wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengulo alisema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 16, 2022 na ilitajwa kwa mara ya kwanza Januari 23, 2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Lukumai.

Aidha, wakili Chengulo amesema katika shitaka hilo Matrida Sigaleti anawashitaki Profesa Kasanga ambaye ni mume wake wa ndoa na Linael kwa kesi ya Ugoni dhidi yao.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Kwa upande wa washitakiwa ambaye ni Profesa Kasanga na Linael Makundi wanatetewa wa wakili Asifiwe Alinanuswe ambaye alipatakiwa kuzungumzia shitaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine, wateja wangu hawajanipa maelekezo ya kuzungumza nanyi," alisema.

Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
kUNA KESI KUBWA HAPO NA ATALIPWA FIDIA
 
PROFESA MZIMA Hajui sheria ya NDOA
 
Analazimisha kupendwa, ukute yeye ndio chanzo cha mume wake kwenda kuoa mwanamke mwingine. Hakuna mwanaume anaeweza Acha mke mwema. Hadi mwanaume kuoa mke mwingine shida ni kasoro ya mke wa kwanza kashindwa kujua wajibu wake ni nini
Ana haki zake, kisheria kama alioa mke mwingine bila kuvunja ndoa ya kwanza hapo Mmarangu hana ndoa, 'null and void ab initio'
 
Back
Top Bottom