Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Mimi hata kama sikua na cha kuanzia ningeachana navyo maana saa nyingine unaweza hata kuuawa. Na mahakama zetu hizi mhh
Hakuna kitu kama hicho wanaume Baba mmoja unaenda kwa mwingine nako wanakuswaga hivyo hivyo ndugu si utafia njiapanda, mtu kakuoa mbishi unaita umefikisha 40---- akwambie sikutaki nikung"ute tu mavumbi kama mtume Paul weee mie sio Mama yake buana kwanini kutesana hivyo? Labda kama ulikuta anavyo lakini tumeanzia 0 no.
 
Hakuna kitu kama hicho wanaume Baba mmoja unaenda kwa mwingine nako wanakuswaga hivyo hivyo ndugu si utafia njiapanda, mtu kakuoa mbishi unaita umefikisha 40---- akwambie sikutaki nikung"ute tu mavumbi kama mtume Paul weee mie sio Mama yake buana kwanini kutesana hivyo? Labda kama ulikuta anavyo lakini tumeanzia 0 no.
Mimi nimejisemea maana najua kupambana na kupata vyangu binafsi. Kama wewe unaona uaweza kupambana, well and good na una haki kabisa ya kufanya hivyo.
 
Yes... kwenye cheti cha ndoa, unasema ndoa yako ni ya aina gani; monogamy, polygamy au potential polygamy. Sasa kama ulisema ndoa yako ni ya mke na mme mmoja; ukiongeza mke bila kuvunja ndoa ya kwanza ni kesi hiyo
Hivi Process za kuvunja ndoa zikoje? Na si inavunjwa Mahakamani? Na si ni lazima Wanandoa wote wakubali au hata Mwanandoa mmoja anaweza kuivunja?
 
-hujui Sheria ya ndoa, Ugoni adhabu yake ni Fidia, haina haja ya kufika huko, labda tabia ya Ugoni iwe ni repetitive despite protest
Wewe hujafuatilia huyo Mama anacholilia 100M sio ugoni anacholilia ni ndoa ya pili kwamba Prof amefunga ndoa ya pili amlipe 100M, rudia tena kusoma acha kukaza fuvu hilo la ugoni limemuongezea uzito tu Ila anacholilia ni kwamba Prof kafunga ndoa ya pili amlipe 100M, elewa ndio ukosoe, yaan unataka kusema amemfuma ugoni ndio amlipe 100M? Jichunguze
 
Hivi Process za kuvunja ndoa zikoje? Na si inavunjwa Mahakamani? Na si ni lazima Wanandoa wote wakubali au hata Mwanandoa mmoja anaweza kuivunja?
Ndoa zinavunjwa mahakamani tu, Sijui sheria zetu zinasemaje hasa kwenye sababu ya kuvunja ndoa; maana nchi nyingine lazima kuwe na sababu, wengine lazima mtengane kwa muda fulani. Ila hakuna namna unaweza kulazimisha ndoa, kama mmoja hataki mwishowe.
 
Profesa wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Christopher Kasanga na mwenzake Linael Makundi mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Mandela mkoani hapo wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro kwa shitaka la madai ya Ugoni dhidi ya malalamikaji Matrida Sigaret.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo jana, wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengulo alisema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 16, 2022 na ilitajwa kwa mara ya kwanza Januari 23, 2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Lukumai.

Aidha, wakili Chengulo amesema katika shitaka hilo Matrida Sigaleti anawashitaki Profesa Kasanga ambaye ni mume wake wa ndoa na Linael kwa kesi ya Ugoni dhidi yao.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Kwa upande wa washitakiwa ambaye ni Profesa Kasanga na Linael Makundi wanatetewa wa wakili Asifiwe Alinanuswe ambaye alipatakiwa kuzungumzia shitaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine, wateja wangu hawajanipa maelekezo ya kuzungumza nanyi," alisema.

Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Professor Mgeni wa SUA aliuwawa kwa kula Watoto wa shule na wake Za watu. SUA ni chuo cha wapemba Chu…p
 
Back
Top Bottom