Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Profesa wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Christopher Kasanga na mwenzake Linael Makundi mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Mandela mkoani hapo wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro kwa shitaka la madai ya Ugoni dhidi ya malalamikaji Matrida Sigaret.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo jana, wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengulo alisema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 16, 2022 na ilitajwa kwa mara ya kwanza Januari 23, 2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Lukumai.

Aidha, wakili Chengulo amesema katika shitaka hilo Matrida Sigaleti anawashitaki Profesa Kasanga ambaye ni mume wake wa ndoa na Linael kwa kesi ya Ugoni dhidi yao.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Kwa upande wa washitakiwa ambaye ni Profesa Kasanga na Linael Makundi wanatetewa wa wakili Asifiwe Alinanuswe ambaye alipatakiwa kuzungumzia shitaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine, wateja wangu hawajanipa maelekezo ya kuzungumza nanyi," alisema.

Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Hii kesi haihitaji wakili.
Professor alipe 100 m biashara imekwisha
 
Wakili anatakaje kesi isikilizwe faragha anaficha nini wakati tutasoma kila kitu kwenye hukumu pindi itakapotoka?[emoji16][emoji16]


Kama hataki waandishi si angeyamaliza kwa amani tu nyumbani mara baada ya kupokea madai.


Sasa kufunga ndoa kunawezaje kukaitwa UGONI?? Maana ugoni ni ile hali ya mtu aliyeoa au kuolewa kufumaniwa na mwenza wake, akiwa anafanya ngono na mtu mwingine. Kufunga ndoa tayari imekuwa ni ugoni?? Anyways, labda ana ushahidi kuwa hawa watu wamebanjuana, na vipi wakijitetea kuwa walikuwa wanajichunga wakisubiri mpaka NDOA na hata baada ya ndoa hawajabanjua kwa sababu labda mmoja alikuwa mgonjwa nk?



Unaweza kabisa, na kuna mwamba ameweka kesi humu kuonesha mahakama ilivyoamua alipwe fidia, ila sasa lazima uthibitishe kuwa hao unaowadai fidia wamezagamuana. Kama kwenye kesi iliyowekwa, jamaa amempa mimba kabisa yule demu, anarukaje fidia!! Tofauti na mwamba Profesa hapa, haijawekwa wazi kama kuna mizagamuano zaidi ya kusema kuwa kuna ndoa ilifungwa.


Ugoni uthibitisho wake sio ndoa, bali tendo la ndoa. Kama ishu ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja, mke alitakiwa kupinga ndoa ya pili, sio kudai fidia ya ugoni bila kuthibitisha ugoni wenyewe. (Najua ni mapema sana, maana kesi haijaanza kusikilizwa, labda atathibitisha huo ugoni)
Thanks,

Na je Mlalamikaji akipata ushahidi kuwa Mumewe amefunga ndoa na Mwanamke mwingine, hiyo haitoshi kumpa ushindi wa kupata fidia anazotaka?
 
Ndoa zinavunjwa mahakamani tu, Sijui sheria zetu zinasemaje hasa kwenye sababu ya kuvunja ndoa; maana nchi nyingine lazima kuwe na sababu, wengine lazima mtengane kwa muda fulani. Ila hakuna namna unaweza kulazimisha ndoa, kama mmoja hataki mwishowe.
Sababu mbona zinajulikana kama hiyo uzinzi,kufanyiana ukatili,hata kama mmoja wenu Ana matatizo ya akili
Talaka inatoka,kingine pia itoke mmoja wenu kafungwa kifungo cha maisha gerezani ukiomba talaka utapata

Ova
 
Mfano baraza la usuluhishi wa ndoa kushindwa kutatua mgogoro uliyoko
Kwenye ndoa
Hapo ndipo mtaambiwa muende mahakamani sasa!

Ova
Na je kama aidha wanandoa wote au mmoja hayupo tayari kwa masuluhishi?
 
. MUTU kapata mbunye mpya yazamani inaleta kesi mama tilia wewe ni mama wa nyumbani mwenzako mama wa bank huoni TOFAUTI?
Je kama yeye alimwambia atulie nyumbani hapo imekaaje! Mwanzo hakuwaona wasomi wenzie degree ya kwanza mpaka uprof hakuwaona wasomi? Sema tamaa tu hiyo ukute Matilda yupo vizuri tu yeye ndiye kamfuja
 
Back
Top Bottom