Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Sheria inasema hivyo Ila sijawahi kuona kesi ya mwanaume anaedai fidia kisa kamfuma mkewe na mwanaume mwingine, km umeiona naomba unijulishe
This is a man's world.
Mwanamme akifumaniwa na mkewe Hilo linazungumzika.
Mwanamke akifumaniwa na mumewe Ni habari nyingine....
 
This is a man's world.
Mwanamme akifumaniwa na mkewe Hilo linazungumzika.
Mwanamke akifumaniwa na mumewe Ni habari nyingine....
Mwanamke akifumaniwa anapelekwa mahakamani kudaiwa fidia? Jibu ndio au hapana?

Km una kesi ya namna hio naomba unionyeshe, namaanisha fidia sio talaka

Na kwanini sheria imetungwa kulenga upande mmoja kua utatoa matunzo ya watoto, upande mmoja utaporwa mali ulizozitafuta kwa jasho, upande mmoja utatakiwa kulipa fidia baada ya ugoni?

Kwanini mwanamke akifumwa ugoni asiambiwe kua atatoa matunzo ya watoto ikiwemo pesa za matunzo ya watoto, mali zake alizochuma zitagawa kwa mwanaume pasu kwa pasu mara baada ya talaka kutolewa na mahakama, na fidia atamlipa mwanaume baada ya kumfuma mkewe ugoni?

Kwanini sheria haisemi hivyo?

Kwanini sheria upande wa mwanamke inalenga kwenye uchizi na kurukwa kwa akili kwa mwanamke na sio vinginevyo?

Yaan sheria ni kandamizi kwa upande wa mwanaume tu na sio kwa mwanamke kwanini?

Lakini eti kuna mtu anainuka anasema Sheria ya Ndoa inamkandamiza mwanamke wakati inamnyanyua especially wanawake wajanja wakiisoma sheria ya Ndoa ni sehemu ya kuwapiga vibaya wanaume wakora kupitia sheria ya Ndoa, Sheria ya Ndoa inamuangamiza mwanaume
 
wanawake ni watu wa ajabu tena ajabu sana sana sijakosea narudia tena..........huyu anae lalamika hovyo hivi hajaata kaunyumba ka professor kitambo sasa!!.......

lkn akimchaa nao tuuuu!!! anakuwa mpoleeeee!! hasira zooote kwisha hiyo ndo dawa yao!! ukiona ke analial lia hovyo mara mahakamani mara anatakamkuolewa kalikosa dyudyuuu! tu!

hana lolote huyo!! anataka bakora ka zi miss!! .....mara nyingi hata akisoma hapa!! atasema mmmhii!! wanaumeee? pwiii!! atacheka tuu anaenda zake!!...uongo wadada semeni ukweli wenu!! hata weye uko ivoooo...
 
Mbona kadai pesa kiduchu hivyo? Hili ni swala kuharibiwa hadhi na maisha yake.... Alitakiwa aanzie 0.5bn au hata 1bn .
Ningekuwa mimi ni huyo Kissanga hiyo 0.1bn ningempa bila hata ya kwenda mahakamani.
We unafikiri mtu kuwa profesa ndo kuwa na hela?

Profesa ni mbwembwe tu, we unafikiri angekuwa na pesa angekubali kudhalilika hv?
 
Haya wakigawana 3 each, mapenzi yatarudi? Non sense.... na nakuhakikishia huyo Matrida ataachwa Solemba!!
Ipo hivi ni bora uugulie maumivu ya kuachwa tu lakini sio maumivu hadi ya mlichokichuma
 
Profesa wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Christopher Kasanga na mwenzake Linael Makundi mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Mandela mkoani hapo wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro kwa shtaka la madai ya Ugoni dhidi ya mlalamikaji Matrida Sigaret.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo jana, wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengulo alisema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 16, 2022 na ilitajwa kwa mara ya kwanza Januari 23, 2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Lukumai.

Aidha, wakili Chengulo amesema katika shtaka hilo Matrida Sigaleti anawashtaki Profesa Kasanga ambaye ni mume wake wa ndoa na Linael kwa kesi ya Ugoni dhidi yao.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washtakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Kwa upande wa washtakiwa ambaye ni Profesa Kasanga na Linael Makundi wanatetewa wa wakili Asifiwe Alinanuswe ambaye alipotakiwa kuzungumzia shtaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine, wateja wangu hawajanipa maelekezo ya kuzungumza nanyi," alisema.

Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Mwenye nakala ya hukumu ya kesi hii,angenipatia,ningemshukuru sana
 
Back
Top Bottom