Morogoro: Serikali kumpima mtoto anayedhaniwa kuwa na kipaji cha hesabu

Morogoro: Serikali kumpima mtoto anayedhaniwa kuwa na kipaji cha hesabu

Yani kujua hesabu ndio itoshe na kuwa kigezo cha kurushwa madarasa!! Hayo masomo mengine ni vipi anapiga kama kawa au ndio yaleyale
Hata walimu wameshndwa kuwaelewesha viongoz,kwa mtaala wa sasa hauruhusu mwanafunz kuacha ya nyuma ambayo hajajifunza na kukimbilia ya mbele,kwa vile ana akili sana, apelekwe mbele lakini na ya chekechea aendelee kujifunza akiwa huko mbele wanapotaka kumrusha.

Dogo anajua mahesabu lakini hajui kuandika
 
Mtoto Charles Mathias Mbena(6) mkazi wa Kibungo Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ameonesha kipaji cha hesabu ambapo anaweza kujumlisha na kutoa hesabu za makumi na malaki bila kutumia karatasi.

Mtoto huyo anayesoma darasa la awali katika Shule ya Msingi Nyigwa ametakiwa kufanyiwa majaribio ili kumpeleka katika Shule na darasa analostahili.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuele Kalobelo amesema wamegundua ana kipaji hivyo watamfanyia majaribio.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala ameelezea azma yao ya kuboresha mazingira ya Shule ya Msingi Nyigwa kwa kuijengea madarasa manne mbali na mawili ambayo yanamaliziwa na Mkurugenzi.

View attachment 1722586

Pia soma: Serikali yaagiza mtoto Charles Mathias arushwe darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada


Hawa wanakosea sana, huyo mtoto kwanza hajaweza kusoma na kuandika pili hajui hesabu za kuzidisha na kugawanya, wangemfundidmsha kwanza hayo mambo mawili ndipo kipaji chake kingekuwa zaidi ya hapo na ndipo mambo mengine yangefuata.

Kujua kutoa na kujumlisha kwa kichwa hiyo haitoshi kujua kwa undani kipaji cha mtoto.

Mimi marehemu Babu yangu likuwa mkali sana wa hesabu zote kwa kichwa naye hakwenda shule.

Kujua hesabu za kutoa na kujumlisha kwa kichwa sio kipimo pekee cha uwezo wa mtu kujua hesabu, je akina Euler, Newton , Ramanujan, Einstein nk, katika utoto wao walikuwa wanaweza kufanya mahesabu kwa Kichwa??!.
 
watakuwa wanajiridhisha.
Kama ana akili anazo tu na atawajibu.
Ila anajitahidi sana kwa umri huo wengi tulikuwa hatujui hesabu
Inamaana yale maswali aliyoulizwa hadi kila mtu akaamini dogo ni kipaji hayatoshi?
 
Nikupoteza mudatu, jamboa lamaana hapo nikujenga hiyo shule na kuweka miundombinu rafiki kwa wanafunzi ili huyo mtoto nae aendelee na step zote za madarasa, hana kitu spacial cha kumvusha darasa.
Mtu hajui kusoma wala kuandika unampima nini.
 
nimemuona nafikir asome kwa mfumo huu huu rasmi.maana ninmtoto bado ingawa mjanja.asome na awe anapewa stimulations extra carricular kwa kipaj chake,mana ndio kwanza anajifunza mwandiko..
 
Kumpima ?, Wanampimaje ?, Kwanini hivyo vipimo wasivisambaze kwenye mashule yote ili tupimane wote ?

Hizi Siasa shida sana..., sitashangaa badala ya waalimu na wataalamu kumpima ukashangaa mbunge, mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ndio wapimaji wakuu (bila kusahau makamera na waandishi wa habari)..., Kupeana stress tu, na presha katika umri mdogo
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
huyo mtoto asome hesabu hadi kidato cha sita, kisha aende chuo kusomea computer science, akimaliza aende JESHINI upande wa CYBER WARFARE ( yaani kazi yake iwe kutengeneza ma VIRUS yakupoteza muelekeo wa makombora ya adua na ndege)
 
Back
Top Bottom