Morogoro: Serikali kumpima mtoto anayedhaniwa kuwa na kipaji cha hesabu

Morogoro: Serikali kumpima mtoto anayedhaniwa kuwa na kipaji cha hesabu

Wamjengee shule ya pekee yake asome hesabu tu kwakua watafuta kiki hawampimi kwenye masomo mengine
 
Mtoto Charles Mathias Mbena(6) mkazi wa Kibungo Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ameonesha kipaji cha hesabu ambapo anaweza kujumlisha na kutoa hesabu za makumi na malaki bila kutumia karatasi....
Wamuangalie vile vile kama ana kipaji cha mpira akachukuwe nafasi ya sapong pale yanga!
 
Suala hapa unaweza kukuta anaweza hesabu tu, masomo mengine hamna kitu.

Au anaweza kuwa mwepesi wa kukokotoa hesabu lakin akawa mzito kuelewa masomo mengine.

Au akatokea kuwa mwepesi kufundshwa na kuelewa hesabu zote mpaka za Chuo kikuu lakin masomo mengine ikawa wa kawaida tu.

Sasa nini ni nini?

Wampime vizuri uwezo/ kipaji chake (kama kipo) kipo wapi na wamsaidie hata kwa kumpeleka nje kama kwetu hatuna sehemu za kuendeleza watoto kama hao
 
Unaweza kuwa bingwa (kuwa na kipaji) cha jambo fulani lakin lingine ikawa shida.

Kipaji cha hesabu kiko juu lakin baiolojia ni kawaida tu, au

Kipaji cha juu cha fizikia lakin kemia na jiografia wa kawaida tu

Wengine wana bahatika kuwa mavipaji ya vitu vingi

Cha kufanya tuanzishe shule chache maalum za kuendeleza hawa watu, watoto kwa wakubwa. Tukiwa tunza vizuri watakuwa na msaada mkubwa sana kwetu

Nna jamaa yangu mmoja kaishia la saba tu lakin ana uwezo mkubwa sana wa kuangalia kitu na kukiunda kama kilivyokuwa mwanzo. Macho au akili yake utafikir ni kamera
 
Karibu AyoTV uyafahamu maisha ya Charles Mathias Mbena, mtoto alie-trend kwenye mitandao ya kijamii akionekana akijibu maswali ya hesabu ambayo kikweli hesabu ni kubwa kuliko umri wake, bonyeza PLAY hapa chini kutazama maisha yake.
 
Back
Top Bottom