1). Basi la kampuni ya Ahmed Coach linalofanya safari Kati ya Tanga kuelekea Mbeya, limepata ajali maeneo ya Sangasanga Mkoani Morogoro muda si Mrefu, chanzo na Habari zingine tutatoa baada ya uchunguzi kufanyika.
UPDATES;
2). Watu 13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ahmeed baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likisafirishwa kwenda nje ya nchi lenye namba za IT 2816 katika eneo la Melela Kibaoni Barabara kuu ya Morogoro-Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Fortunatus Muslim amethibitisha kutokea kwa ajalim hiyo.
UPDATES;
3). Morogoro. Vilio na simanzi vimesikika kila kona katika eneo la Malela Kibaoni wilayani Mvomero, Morogoro kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria na lori la mizigo.
Katika ajali hiyo, watu kadhaa wamejeruhiwa wakati lori lenye namba za usajili za IT 2816 lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda DR Congo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ahmeed lenye namba za usajili T732 ATH.
Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema ajali hiyo imetokea leo saa 10.30 jioni na kusababisha vifo vya watu 16.
Kamanda Muslim amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki maarufu bodaboda hivyo, kupoteza mwelekeo na kukutana na basi hilo uso kwa uso.
Kwa mujibu wa Kamanda Muslim, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Hata hivyo, Kamanda Muslim ametahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa, kazi ya uokoaji bado inaendelea kwenye eneo hilo.
---
Rais Samia Suluhu kupitia akaunti yake rasmi ya Twitter ametoa salamu za rambirambi kufuatia ajali hiyo.
Ameandika
Nimesikitishwa na vifo vya watu 22 vilivyosababishwa na ajali ya basi kugongana na lori katika eneo la Melea Kibaoni, Morogoro.
Nawapa pole wafiwa, nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka.
Nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani.
Duuh inaonyesha ni hatari mpaka umeshindwa kupiga oicha...wapumzike kwa amani tusisahau kifo ni chetu sote...ila waangalizi wa usalama msizembee mkatutanguliza
Basi la Ahmed linalofanya safari zake Tanga - Mbeya limegongana na lori maeneo ya Sangasanga na inasemekana kuna watu wamepoteza maisha. Picha ni mbaya haizfai
Basi la Ahmed linalofanya safari zake Tanga - Mbeya limegongana na lori maeneo ya Mzumbe na inasemekana kuna watu wamepoteza maisha. Picha ni mbaya haizfai
Basi la Ahmed linalofanya safari zake Tanga - Mbeya limegongana na lori maeneo ya Mzumbe na inasemekana kuna watu wamepoteza maisha. Picha ni mbaya haizfai