Morogoro: Watu takriban 14 wafariki dunia katika ajali ya Lori na Coaster eneo la Mikese

Morogoro: Watu takriban 14 wafariki dunia katika ajali ya Lori na Coaster eneo la Mikese

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Inasemekana kuna ajali imetokea Mikese ikihusisha bus dogo Coaster na kuua watu wengi, wenye taarifa zaidi tuambizane

---
Ajali.png
AJALI MBAYA MOROGORO, WATU 14 WAFARIKI, 7 WAJERUHIWA.

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 7 kujeruhiwa baada ya gari kubwa la mizigo kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria leo majira ya saa 2 eneo la Mikese Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu wakati akiongea na waandishi wa Habari Disemba 17, 2024 hospitalini hapo amesema, hospitali hiyo imepokea majeruhi 7 na miili ya watu 14 waliofariki katika ajali hiyo ambapo 8 kati yao ni wanaume na 6 ni wanawake hiyo ikiwa ni taarifa ya awali.

Akifafanua zaidi, Dkt. Nkungu amesema kati ya majeruhi 7 wanaume ni wanne na watatu ni wanawake na kwa upande wa waliofariki Nane ni wanaume na sita ni wanawake kati yao mwili mmoja ni wa mtoto.

".. Hapa Hospitalini tumepokea majeruhi 7 na miili ya watu 14 waliofariki....kati yao miili 8 ya wanaume na miili 6 ya wananwake." Amesema Dkt. Daniel Nkungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima aliyefika hospitalini hapo mara tu baada ya ajali, ametoa pole kwa watanzania wote kwa kuondokewa na watanzania wenzetu 14 kutokana na ajali hiyo, huku akiwasisitiza madereva kufuata sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima kutokea.
 
Duh.
tokea kitengo cha udhibiti wa ajali barabarani kimeundwa polisi, ajali zimeongezeka au zimepungua? tunaomba takwimu. Just government bloat.

Madereva wazembe, barabara nyembamba, magari mabovu ndio vyanzo vikuu.. polisi wanahusika na viwili, serikali inahusika na kimoja.. Daini mpangokazi kwenye uchaguzi mwakani wananchi.
 
Back
Top Bottom