Morogoro: Watu takriban 14 wafariki dunia katika ajali ya Lori na Coaster eneo la Mikese

Ajali imetokea jana Lubungo karibu na Mikese majira ya saa moja usiku….it was terrible…..coaster ilikuwa inatokea Dar kwenda Moro..

Ajali hiyo imetokea usiku wa saa mbili, Desemba 17 katika eneo la Mikese kwenye barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam wakati basi dogo ilipokuwa inatokea mkoani Morogoro kuelekea Dar es Salaam na Lori hilo likitokea Dar es Salaam kwenda Mikoani.

Taarifa zinachanganya
 
Screenshot_20241218_091620_Samsung Internet.jpg

Screenshot_20241218_091439_Samsung Internet.jpg
 
Inasemekana kuna ajali imetokea Vigwaza ikihusisha bus dogo Coaster na kuua watu wengi, wenye taarifa zaidi tuambizane

---

MOROGORO - Watu 14 wamefariki dunia papo hapo na wengine nane kujeruhiwa baada ya gari ndogo ya abiria aina ya Coaster kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.

Ajali hiyo imetokea usiku wa saa mbili, Desemba 17 katika eneo la Mikese kwenye barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam wakati basi dogo ilipokuwa inatokea mkoani Morogoro kuelekea Dar es Salaam na Lori hilo likitokea Dar es Salaam kwenda Mikoani.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima amefika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo usiku kuona majeruhi na watu waliofariki kutokana na ajali hiyo.

Malima ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kubwa aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Mganga Mfadhiwi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Dk Daniel Nkungu amethibitisha kupokea miili 14 ya Watu waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo Pamoja na majeruhi wanane.

Mganga Mfadhiwi wa Hospitali hiyo amesema waliofariki wanane ni wanaume na sita ni wanawake miongoni wao ni pamoja na mtoto mwenye kukadiriwa kuwa na umri wa miaka nane.

Dk Nkungu amesema kuwa miili ya wote waliopoteza maisha hadi sasa bado hawajatambulika.

Habari Leo
Ewaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,hayo ndio maneno sasa,hongera kwa kupambana hadi kutukamilishia taarifa,asante sana

Pole sana kwa wafiwa wote na majeruhi.Mwenyezi Mungu awaponye
 
Inasemekana kuna ajali imetokea Vigwaza ikihusisha bus dogo Coaster na kuua watu wengi, wenye taarifa zaidi tuambizane

---
AJALI MBAYA MOROGORO, WATU 14 WAFARIKI, 7 WAJERUHIWA.

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 7 kujeruhiwa baada ya gari kubwa la mizigo kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria leo majira ya saa 2 eneo la Mikese Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu wakati akiongea na waandishi wa Habari Disemba 17, 2024 hospitalini hapo amesema, hospitali hiyo imepokea majeruhi 7 na miili ya watu 14 waliofariki katika ajali hiyo ambapo 8 kati yao ni wanaume na 6 ni wanawake hiyo ikiwa ni taarifa ya awali.

Akifafanua zaidi, Dkt. Nkungu amesema kati ya majeruhi 7 wanaume ni wanne na watatu ni wanawake na kwa upande wa waliofariki Nane ni wanaume na sita ni wanawake kati yao mwili mmoja ni wa mtoto.

".. Hapa Hospitalini tumepokea majeruhi 7 na miili ya watu 14 waliofariki....kati yao miili 8 ya wanaume na miili 6 ya wananwake." Amesema Dkt. Daniel Nkungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima aliyefika hospitalini hapo mara tu baada ya ajali, ametoa pole kwa watanzania wote kwa kuondokewa na watanzania wenzetu 14 kutokana na ajali hiyo, huku akiwasisitiza madereva kufuata sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima kutokea.
Ndugu mtoa mada hebu badilisha heading ya hii taarifa Vigwaza iko Pwani na Mikese ipo Morogoro.
 
Sasa sisi tutajuaje si angemuuliza aliyemskia ndio ingekua rahisi zaidi au?
Kwa Nia njema TU. Hii tabia unayo ionyesha hapa uki ipalilia na kuiendeleza. Itakuchelewesha Sana kupata mafanikio na maendeleo kwa ujumla wote.

Zingatia na uifanyie kazi.

Shukrani 🙏
 
Ndugu mtoa mada hebu badilisha heading ya hii taarifa Vigwaza iko Pwani na Mikese ipo Morogoro.
Asante Mkuu ila hiyo sehemu haibadilishiki mpaka waingie wenyewe JF
 
Badilisha maelezo kwenye uzi yasome kama heading inavyosema mkuu.
Ningetamani kufanya hivyo ila mfumo unamruhusu admin tu mimi sina title editing access
 
Inasemekana kuna ajali imetokea Vigwaza ikihusisha bus dogo Coaster na kuua watu wengi, wenye taarifa zaidi tuambizane

---
AJALI MBAYA MOROGORO, WATU 14 WAFARIKI, 7 WAJERUHIWA.

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 7 kujeruhiwa baada ya gari kubwa la mizigo kugongana uso kwa uso na gari dogo la abiria leo majira ya saa 2 eneo la Mikese Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu wakati akiongea na waandishi wa Habari Disemba 17, 2024 hospitalini hapo amesema, hospitali hiyo imepokea majeruhi 7 na miili ya watu 14 waliofariki katika ajali hiyo ambapo 8 kati yao ni wanaume na 6 ni wanawake hiyo ikiwa ni taarifa ya awali.

Akifafanua zaidi, Dkt. Nkungu amesema kati ya majeruhi 7 wanaume ni wanne na watatu ni wanawake na kwa upande wa waliofariki Nane ni wanaume na sita ni wanawake kati yao mwili mmoja ni wa mtoto.

".. Hapa Hospitalini tumepokea majeruhi 7 na miili ya watu 14 waliofariki....kati yao miili 8 ya wanaume na miili 6 ya wananwake." Amesema Dkt. Daniel Nkungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima aliyefika hospitalini hapo mara tu baada ya ajali, ametoa pole kwa watanzania wote kwa kuondokewa na watanzania wenzetu 14 kutokana na ajali hiyo, huku akiwasisitiza madereva kufuata sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima kutokea.
This is so sad. My condolences to all those involved may God rest their precious souls in eternal peace as they embark eternity.

Magonjwa Mtambuka
 
Ningetamani kufanya hivyo ila mfumo unamruhusu admin tu mimi sina title editing access
Huwezi ku edit tittle. Edit maelezo ya kwenye uzi yaende kama title inavyosema
 
Back
Top Bottom