Morogoro: Watumishi wa Umma Walazimishwa kwenda kwenye mkutano wa Rais Samia leo hii

Yote haya wanafanya kumpumbaza Rais ili aamini kuwa watu wanampenda sana. Halafu wale punguani utawasikia kuwa eti kwa mafuriko haya ya wananchi hakuna hata haja kampeni mwakani.

Upunguani uliochanganyika na unafiki ni mzigo unaowaelemea viongozi punguani kama huyo mkurugenzi.
 
Kama kawaida ni walimu hakuna wahudumu wa afya wala kilimo
 
Kuna ubaya gani..huyo ndio mwajiri Mkuu..kuna vitu vya kuvisema lakini sio hili
 
Kwa maelezo yake inaonekana huyu ni Mkuu wa Shule....hata haoni aibu na hatambui kwamba Mhe. Rais ndio mwajiri Mkuu.
 
Yaani wewe kama Mkuu wa Shule huna akili na haustahili hiyo nafasi..hiyo ni barua ya ndani na siyo taarifa kwa Umma.
 
Wakati tunaanza mfumo wa Vyama vingi Tulikubaliana kuwa wanafunzi na watumishi wa umma wasisumbuliwe na ziara za wanasiasa. Ila kwa kuwa siaiemu imekosa mvuto wamemua kuvuruga utaratibu. Balafu ndiye huyu huyu anayehubiria Watu wafanye siasa za ustaarabu huku mwenyewe akiukanyaga ustaarabu na kiatu cha matope.
 
Kiitifaki, rais ndiye Afisa Utumishi Mkuu wa nchi.

Kutokwenda kwenye ziara yake ni utovu wa nidhamu.
 
Juzi kuna jamaa alikua na mtoto wa shemeji yake anaesoma darasa la nne shule St kayumba, sasa mwana akaanza kumuuliza kuhusiana na multiplication table, akamwambia dogo unajua table ya 4? Dogo akasema hapana , akamuuliza ya 2 dogo akajing'atang'ata akasema anaweza jamaa akamuuliza 2×1 ngapi? Dogo hajui

Mwana akamwambia haya imba table ya kwanza dogo hata 1×1 hajui ni ngapi ilibidi nicheke tu .
 
Kweli na wasipofanya hivyo itakuwa aibu sana maana watu hawana mpango na ccm
 
Hoja yako ni nini?

Rais ni kiongozi mkubwa kwenye nchi yetu
 
Reactions: BRN
Huo upuuzi sijawahi fanya na siwezi kufanya.
 


Wee mgeni sana katika utumishi wa Umma, hivi usipoenda kumsikiliza Mh. Rais wa nchi, unataka kumsikiliza nani mwingine?
 
Huenda hata kupiga kura wanalazimishwa kwa siri kuchagua ccm bila ridhaa yao. Barua hiyo inaonesha nyomi kwenye mikutano ya rais ni ya kulazimishana, watu hawahudhurii kwa matakwa yao.
Halafu wanajipigisha picha na kujisifia nazo, kumbe watu wamelazimishwa!
 
Mishahara ikichelewa kidogo mnapiga kelele na kulalamika....ohh Mama..leo kwenda kumsikiliza mnalalamika mnalazimishwa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…