Lazima wahudhurie maana Ndiye muajiri wao na ndie mlipaji wao wa Mishahara na ndiye amewafanya wawe na tabasamu,furaha na matumaini makubwa sana kutokana na kazi kubwa sana aliyoifanya ya kuboresha maslahi yao ikiwepo kupandisha mishahara yao kwa 23% hasa kwa wale wa kima cha chini,kulipaa malimbikizo yote ya madeni,kurejesha nyongeza ya kila mwaka ,kuboreshwa kwa mazingira ya kazi n.k. kwa hiyo wanakwenda kumsikiliza na kupokea maelekezo mbele ya wananchi ili wananchi wajuwe nini kimeagizwa na Rais wao kwa watumishi wao . Kusudi wananchi wakienda kupata huduma na wakatendewa tofauti na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa waweze kutoa taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa