Morrison huru kujiunga na Simba SC, kamati yasema mkataba wake na Yanga una mapungufu

Morrison huru kujiunga na Simba SC, kamati yasema mkataba wake na Yanga una mapungufu

Yanga inabidi wachukue funzo kupitia morisson,waache janja janja mambo ya kuishi kwa mazoea wakati zama hizo zilishapitwa na wakati
 
Waseme tu Yanga wamefoji mkataba na Morisson,kwanini kufichaficha? Wapewe adhabu stahiki kulingana na kosa lao,hakuna kupindisha maneno.
Adhabu stahiki kama ile ya Singano na Simba?
 
Amesikika Mwenyekiti wa kamati ya hadhi na maadili ya wachezaji akisema kwamba, mkataba kati ya Morrison na Yanga ulikuwa una mapungufu na mapungufu hayo yamempa faida Morrison kushinda kesi aliyoipeleka yeye mwenyewe TFF.

1. Kwanza ikumbukwe aliyeshtaki kwa TFF ni Morrison akiamini hakuingia mkataba na Yanga, hapa naamini aligundua mapema mapungufu yaliyopo kwenye makubaliano yao ambayo Yanga waliamini mkataba, halali wakati huohuo Morrison alitumia mapungufu hayo, kuwamaliza Yanga ndani ya masaa 72.

2. Yanga hawakuwa makini kwenye mkataba husika, ambapo yoyote akiona anapata mashaka, kuanzia kwenye tarehe, saini hadi utunzaji wa karatasi yenyewe ulitia shaka hapo ilikuwa rahisi kwa hoja za Morrison kuonekana zina mashiko kuliko za Yanga.

3. Kamati ya usajili ya Yanga ijiangalie kama jambo hili lilikuwa bahati mbaya wasirudie tena...ni aibu kwa klabu kubwa Afrika kama Yanga kutokuwa makini kwenye mambo muhimu kama haya...tena inasemakana mikataba yote haikuwa na viini vya kimkataba vilivyotimia kuanzia ule wa miezi sita na huu wa miaka miwili, ambapo hukumu imejikita kimkakati bila kuidhuru timu Yanga....maana ikijulikana vizuri kuna adhabu Yanga wanaweza kuipata ikiwemo na kushuka daraja kama walivyowahi kufanyiwa Juventus ingawa mazingira ya kesi husika ni tofauti.


4. Kwa utashi wa hali ya juu.....Yanga watulie na wakubali mapungufu madogo yaliyoficha mustakabali mkubwa wa uzembe wa kamati ya usajili na kwa hili wajifunze ingawa naamini kwa ujio wa Senzo haya mambo yatakuwa safi.


Kila la kheri SOKA LA TANZANIA
 
Yanga inabidi ibebe lawama tu,ila aliyeingia choo cha kike ni matapeli wa GSM wala sio Yanga. hao wachezaji wanaosaini umeona hata mmoja akisaini ofisini kwa Yanga? au mbele ya logo za Yanga na mzamini Sportspesa?
 
Wewe unataka aweje, hiyo laana inasababishwa na nini, kwani soka ni ibada au ni burudani tu.Morison hana shida yoyote mambo mengine ni hali tu yakibinadamu sisi tunachotaka toka kwake ni mpira.Tatizo la haya yote ni mambo yetu yakibabaishaji yaliyoko nchi hii kuanzia vilabu hadi Tff kwenyewe.
Mkuu sio vyema kudandia jambo ambalo hulielewi vyema.
 
Back
Top Bottom