Morrison huru kujiunga na Simba SC, kamati yasema mkataba wake na Yanga una mapungufu

Morrison huru kujiunga na Simba SC, kamati yasema mkataba wake na Yanga una mapungufu

Huyo Hanspope siniyule mhaini?sasa tunakwenda cas. Tff wataumbuka,kama mbwai na iwe mbwai. Wamemwaga ugali sisi tunamwaga mboga!
 
Morrison hakuchukua hiyo pesa, GSM ndio waliomuwekea Morrison hiyo pesa kwenye acc yake baada ya kujua anaweza kwenda Simba ili wamshawishi asaini mkataba wa miaka miwili, matokeo yake Morrison akazikataa hizo pesa, na mkataba wao hakusaini.
Mkataba amesaini
 
Kamati haijafanya vizuri kwa sababu hapa kuna kesi ya kufoji mkataba ,ambapo Morrison anadai Yanga wamefoji mkataba hivi hawakuandikishana mkataba na Yanga ,sasa huyu dogo anakosa gani?
Hizo hela zaidi ya mil.69 alizokiri kuchukua zilikuwa za nini? Unachukua mahari ya mtu halafu kesho unasema sitaki kuolewa halafu wakuache tu?
 
Utopolo wamefoji mkataba 100% sema tu TFF imewastahi kuwambia ukweli, tafuteni wadhamini wenye akili huyu wa GSM atawanyoosha mtakuja kulipa trillion 1 ya uwekezaji kwake, amekaa kitaperi sana
 
Hizo hela zaidi ya mil.69 alizokiri kuchukua zilikuwa za nini? Unachukua mahari ya mtu halafu kesho unasema sitaki kuolewa halafu wakuache tu?
Usiwe na akili ya kushikiwa ,ile si kishika uchumba ,hakukuwa na makubaliano kusaini mkataba ,yanga walichofanya ni kumwekea hela kwenye account bila ridhaa yake ili ashawishike huku wakijitapa wamemsainisha
 
Morison afungiwe, amesain mkataba na timu mbili, yanga lazima tumkomeshe, hatacheza mechi hata moja hapa tanzania
 
Kuna njama za wazi kabisa kuwa Kamati ya TFF na maamuzi yake kumhusu Moris, inapanga kuibeba Simba. Hujuma kama hizi dhidi ya baadhi ya vilabu zinaua mpira hivyo ni vema serikali iingilie kati. Halafu nadhani pia Rais wa TFF achunguzwe vizuri malengo yake katika soka letu, simwelewi elewi!

Hebu jaribu kutumia akili japo kidogo basi!

Raisi wa TFF anahusikaje hapa? Mwenyekiti wa hii kamati iliyotoa maamuzi unaijua lakini?

Kwanini usiwalaumu Viongozi wako wa Yanga waliopeleka kwenue Kamati Mkataba uliochanwa Saini?
 
Tumeshapata aka nyengine hapa! MikatabaHewa FC na Fojari FC
 
Unaendaje CAS wakati hata FIFA hamjaenda msiropoke ka manyani

Kuna baadhi ya mashabiki wa Yanga ni wajinga kiwango cha lami kwani nashindwa kuelewa kwa vipi wanaona Morrison ana kesi na wasiione kesi ya Yanga ya kugushi nyaraka za mkataba ambao ndio msingi wa kesi yote?

Mawazo mgando hayo yanafikirisha kidogo ukiunganisha malalamiko ya Kocha wao waliyemfukuza Luc Eymael pale aliposhutumu kuwa
1 - Timu Yanga haikufuata makubaliano katika mkataba wao
2 - Mashabiki hawajaelimika na wanapiga kelele tu etc
3 - Timu haina mwelekeo wowote

Nafikiri kuwasaidia Yanga ni kufumua timu, Viongozi wote na pia kukata mizizi yao wanayoitegemea kufanya upuuzi huu ambao upo pale TFF
 
Hii ni habari nzuri kwa washabiki wajinga wa Simba. Mimi kama shabiki imara wa Simba sishabikii Morrison kuja Simba. Morrison ni LAANA kwa viongozi wote wa Simba waliomleta kwenye Klabu yetu.
Wewe unataka aweje, hiyo laana inasababishwa na nini, kwani soka ni ibada au ni burudani tu.Morison hana shida yoyote mambo mengine ni hali tu yakibinadamu sisi tunachotaka toka kwake ni mpira.Tatizo la haya yote ni mambo yetu yakibabaishaji yaliyoko nchi hii kuanzia vilabu hadi Tff kwenyewe.
 
Huyu mtu haeleweki kabisa hastahili kuwepo kwenye soka letu japo pia club kubwa Kama Yanga inajiharibia kwa kufanya janja janja za namna hii.
Haeleweki nini?.Wabongo tuache ubabaishaji, mambo mengine tunafanya kishabiki kisha mtu akitaka mambo yawe wazi tunamwona mkorofi.
 
Back
Top Bottom